Nahitaji kujua kuhusu biashara ya mitumba

Melancholic

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
3,076
Reaction score
5,483
Habari za muda huu wakuu natumai mmeamka vyema sana.

Kwa wale wazoefu wa kuchukua mzigo Karume au Ilala je mabero ya viatu hasa raba na viatu vya shule pamoja na vya kike huwa vinafunguliwa wapi?

Na kuhusu mabero ya nguo pia huwa yanafunguliwa wapi kati ya sehemu hizo mbili?

Pia nasikia kwamba ili upate mzigo mzuri inabidi uwahi saa 9 usiku au 10 alfajili je ni kweli?

Na kama ni kweli je kwa muda huo usafiri unapatikana wapi?

Najua JF ni familia kubwa naamini nitapata msaada wa maswali niliyouliza na kama kuna mengine yenye umuhimu ambayo sijayaorodhesha hapo pia mnaweza kunifahamisha maana mimi ni mgeni kabisa kwenye hii industry.

Note! Mimi natokea Kijitonyama mpakani na Sinza. Natanguliza shukrani na karibuni kwa mchango wenu.
 
Tuko poa sasa bwana ni kweli mzigo upo pale karume Kwa viatu na ilala Boma upande wa nguo sio lazima kuamka saa9 ni maana mizigo wanaanza kufungua saa12 kamili na ni rahisi Sana kitendo cha wewe kufika pale ilala Boma kabla ya huo muda kisha wataalamu wataanza kunadisha nguo moja baada ya nyingine ila Kwa upande wa viatu ambako me ndo nimekuwa nikihusika Napo ni kwamba unakuta vimemwagwa kulingana na bei wewe unachambua mwenyewe kulingana na uhitaji wa wateja wako ahsante
 
Safi sana mkuu Kwa kushare uzoefu wako
 
Ahsante mkuuila kwa upande wa viatu ujasema ni muda gani inabidi ufike ili kupata mzigo mzr
 
Kitu ninachoweza kuongezea..

Japo sijajihuaisha na biashara toka 2021 Ila nipo karibu na wafamya biashara hii..

Ilala Boma nguo za mtumba na karume nguo za mtumba kote wapo vizuri...

Karume viatu vizuri sana.

kwenda alfajiri itasaidia kupata mzigo mzuri na kwabei ya chini kidogo na ushindani unakuwa haupo mkubwa sana.

Kote ilala Boma na karume nafikiri bado wanafungua saa 12 (nilifika saa 11 nikasubiri hadi saa 12)

Chamsingi sana nikushauri uwe na MALENGO YAKO....Uza nguo za mtumba ila jua unataka nini usitake Tu upate hela ya kula haitafika mbali mkuu..
 
Yani jitahidi uwe na lengo mfano unauza nguo za mtumba ukipiga hatua basi unajua hela nitaelezea kwenye shamba la mbuzi kijijini au nitafungua goli la kuuza.mchele, unga na mafuta mtaani

kuwa na malengo kutakufamya uwe grounded muda wote...

Pia naomba ufanye Mtumba wa nguo 1 tu mkuu kama utaweza utakuja kunishukuru...

Uwe na identity yako ya mtumba....kama unauza Koti jeans basi upambanie huko...usiwe unabeba Tu nguo inakuwa ngumu kupata quality unayoitaka...

Nguo zinazotoka ni zakike ndio ila tafuta brand moja upambanie

Koti jeans
Skin jeans
Shiffon blouse
koti Korea
Track suits

Hii itasaidia sana kupata wateja wauhakika pia itakusaidia sana kubobea kwenye nguo husika
 
Kuwa watofauti ukipambana pata sehemu za kumwaga kama wenzio ikiwa ngumu, usiumie.... tafuta sehemu tofauti inayopitika kiasi fuata taratibu weka mzigo wako utafika mkuu....

Siku nyingine unakaa Tu mjini angalia nguo gani zinavaliwa sana..

kama target yako wanachuo basi

pensil skirt
vimini jeans
Skin jeans
Track suits
koti jeans.

Nisiongelee sana hapa pambana alafu uwe na bei special Yan mtu anakuja kwako anajua unauzaga koti jeans Kali 10, au pensil skirt Kali unauzaga 10 (bei usibadikishe Sana)

Kwenye viatu mimi nakwambia
tafuta viatu vya kike changanya na raba za mtumba kali sama za kike chukua hapo karume hata ukikuta raba Kali 5000 chukua wewe utazofua utauza 10 Hadi 15....

Kuwa makini katika bei yani maana lengo ni kufika lakini sio kwa kupaa Ila kwa mwendo wa taratibu...

Viatu na raba zako kali, Uza kwa bei ya kishkaj

alafu pia jitahidi ujenge ukaribu na wateja...siku nyngne huko status unapost wateja wakiwa na bidhaa yako unawasifia na kuengage nao watoto wakike huwa wanafurahi sana na kuwa permanent buyers pia huwaleta wenzao .
 
Mwisho engage sana na wateja jishushe Waite majina yenye staha boss, dada etc....

Katika biashara yako nidhamu, heshima na kuepuka mahusiano viwe mbele

Kwenye biashara hasa hizi za nguo, unaweza pata wateja warembo sana na mkawa mnaengage sana status Ila jitahidi ufocus maana unaweza poteza mteja, rafiki zake, mtaji wako na heshima yako pia.

Ni ngumu ila mhusishe Mungu kwenye biashara yako ushinde tamaa hii ya kutamani wateja.
 
Hongera Kwa information.
 
Mkuu, umeupiga mwingi sn hapa kwny infos kuhusu hii biashara. Hongera sn, nina swali dogo tu hv kwa sisi wenye mitaji yetu ya kuunga unga kwa 200k angalau angalau naweza kuanza?
 
Mkuu, umeupiga mwingi sn hapa kwny infos kuhusu hii biashara. Hongera sn, nina swali dogo tu hv kwa sisi wenye mitaji yetu ya kuunga unga kwa 200k angalau angalau naweza kuanza?
PNdio mkuu hata Mimi nilianza na laki 250..... japo sikufanya muda mrefu sana baada ya kupata ajira

Lakini nguo nilizonunua ilala Boma 500 niliuza 2000, nilizonunua 2k na 3k niliuza 5000/6000 skin jeans nilinunua 3500 nyngne 4000 niliuza 7000 Tu....

Kilasiku jioni nilikuwa nina elfu 10 yangu binafsi nje ya mtaji, mchana nilikuwa sili hahahah....

sema ushauri kwako Kwanza usile matunda ya kazi yako mapema ...Yan utaona faida inakuja na hela inaongezeka ila usiamze spend utakwama

Pili biashara zina siku na siku... Siku ya kwanza nilianza saa 11 jioni ijumaa, sikuuza Hadi saa 1:20 huko mdada alipenda vest moja kali ya maua maua (niliuza 5000 Ila nilinunua 500)
ia kingine jitahidi sana uuze nguo moja coz ukiuza nguo nyingi sana tofauti utashindwa chagua mzigo mzuri....Mimi naona laki 2 unaweza anza na Skin jeans yani Tanzania hii rika la wanachuo asilimia 90 wanavaa skin chagua jeans chambu nzuri, skin jeans tunakagua kiuno kama kikubwa Sana, tunakagua msamba kama umechoka, tunakagua chini (turn up) kusiwe kumepwaya sana iwe inabana chini...pia angalia rangi blue, black zinavaliwa sana.

Kama bei haijabadilika ukiwahi mle ndani na mwanzo wa mnada pale nje ilala boma unaweza pata skin jeans nzuri Kwa elfu 4 had elf 5...wewe utaenda Uza elf 7 tu au inaanzia elfu 8 mwisho elfu 7

Pia Kwa mtaji wako unaweza Uza koti jeans nzuri za kike na kiume (unisex) chagua kali huko ilalaboma au karume kwa elfu 6 Hadi 7 wewe utaenda Uza 10k (japo wengine wanauza 15)
 
Mkuu, umeupiga mwingi sn hapa kwny infos kuhusu hii biashara. Hongera sn, nina swali dogo tu hv kwa sisi wenye mitaji yetu ya kuunga unga kwa 200k angalau angalau naweza kuanza?
So pick kwenye
skin jeans,
Koti jeans
pensil skirt nzuri za darasani na ibadani kwa wanachuo chagua kmoja Uza.

mimi ningeshauri skin jeans Kwanza alafu unavyozidi kwenda unakuwa na bwanga za kutosha nazo zinauza sana naona....

Wewe jiuzie skin jeans, bwanga jeans, koti jeans tu jibrand kilamtu ajue Hilo ndo eneo lako la specialization utafika mbali

Mwisho angalia sana Size ya hizo nguo, mistake moja niliyofanya nilichukua baadhi ya skin jeans size za watoto wa secondary hadi zinatoka zilitoka kwa shida sana

Chagua size za wadada wa chuo, na wadada wa offcn hivo yani watoto wa secondary hawanaga hela.
 
Umeupiga mwingi mwanangu
 
Mtumba mkuu, sijui niufungulie tu thread. Manake nakujua vizur. Ni biashara ambay hutakiw kuingia kichwa kichwa. Unataka kuuza Nn mkuu matisheti /majinzi? Au Nn. Tuanze hapo kwanza
 
 
Mtumba mkuu, sijui niufungulie tu thread. Manake nakujua vizur. Ni biashara ambay hutakiw kuingia kichwa kichwa. Unataka kuuza Nn mkuu matisheti /majinzi? Au Nn. Tuanze hapo kwanza

Viatu vya mtumba vipi?
 
Viatu vya mtumba vipi?
Moja Kati ya biashara yenye competition kubwa mnooo. Nliwahi kufika karume saa 10 na nus asubuhi nikakuta watu wanaondoka. Mpaka Leo sijajuaga wanafunguaga balo usiku wa saa ngap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…