nahitaji kukopa fedha benki na nina miti ya pine 1000

nahitaji kukopa fedha benki na nina miti ya pine 1000

Sadru

Member
Joined
Sep 12, 2011
Posts
23
Reaction score
4
wakuu mi ni mjasiliamali nilio na miti 1000 katika wilaya bukoba vijini sasa nahtaji ushauri jinsi ya kuweza kukopa benki kwa kutumia miti kama dhamana.miti hiyo ina umri wa miaka 10 sasa na ni aina ya pine
 
Ukope pesa za nini? unategemea hata bank wakikufuata nyumani kwako ukatoa maelezo mafupi namna hii utapata pesa zao kweli?
 
Ukope pesa za nini? unategemea hata bank wakikufuata nyumani kwako ukatoa maelezo mafupi namna hii utapata pesa zao kweli?

Je Hilo shamba lina hati hata ile ya kimila (CCRO)? Halafu umeshaandaa mpaka kazi wa hiyo biashara? Hapo ndipo pa kuanzia
 
wakuu mi ni mjasiliamali nilio na miti 1000 katika wilaya bukoba vijini sasa nahtaji ushauri jinsi ya kuweza kukopa benki kwa kutumia miti kama dhamana.miti hiyo ina umri wa miaka 10 sasa na ni aina ya pine

Uza miti mkuu upate pesa isiyokupa mawazo! Kwa umri huo hukosi laki 1 kwa kila mti, hivyo unatengeneza 100 m bila jasho maana wanunuzi wanakufuata mpaka home!
 
Miti ya pine miaka kumi halafu iko 1000, ni michache sana kuishawishi benki, sijui labda kama unataka kukopa milioni moja hivi. Nitatoa sababu,

Bei ya serikali kwa mti uliokomaa wa pine over 20yrs pale Mafinga ni Tsh 50,000/ kama sijakosea sana. Ukija mitaani/vijijini mti huo huo unaweza kuupata kwa Tsh 30,000/, kwa sababu vijijini ni wizi mtupu. Ina maana hiyo yako mtu anaweza kununua kwa Tsh 3500/ mpaka 5,000/ kwa sababu haijafikia umri wa kuvunwa.

Kwa hesabu za miti 500 kwa eka, ina maana una eka mbili. Njia rahisi, ikatie hati hiyo miti au hilo shamba ndio uingie benki.
 
Uza miti mkuu upate pesa isiyokupa mawazo! Kwa umri huo hukosi laki 1 kwa kila mti, hivyo unatengeneza 100 m bila jasho maana wanunuzi wanakufuata mpaka home!

Mkuu ni pines sio mitiki, labda ingekuwa cyprus, kidogo angepata mpunga. Au ingekuwa eucalyptus saligna au acrocarpus, sio pinus patula mkuu, haijafika huko.
 
Uza miti mkuu upate pesa isiyokupa mawazo! Kwa umri huo hukosi laki 1 kwa kila mti, hivyo unatengeneza 100 m bila jasho maana wanunuzi wanakufuata mpaka home!

Miti 1000 kwa bei ya juu utapata 20M... lakini kama unataka mkopo tafuta hati miliki.
 
mkuu ni pm tuongee nikupe amaela au weka namba yako hapa tufanye business
 
Watu wengine bana! Bima ya moto? kijijini? Khaa! nimecheka mbavu sina..........
 
Watu wengine bana! Bima ya moto? kijijini? Khaa! nimecheka mbavu sina..........

Bima ya moto kwenye misitu Tz haipo, makampuni ya kigeni yanaweka Bima kwenye misitu yao huko huko majuu. Hata misitu ya serikali haina bima ya moto.
 
Malila na wataalam wengine, naomba kupata shule kuhusu thinning ya Pinus caribaea inafanyika baada ya umri gani na inatakiwa iwe katika spacing ipi unapopanda na unafanya thining baada ya muda gani na kwa vigezo gani? naambatanisha picha za kishamba changu hapa ambacho nilinunua maeneo ya ziwa victoria.
 
Attachments

  • IMG_1778.JPG
    IMG_1778.JPG
    171 KB · Views: 166
  • IMG_1777.JPG
    IMG_1777.JPG
    161.9 KB · Views: 151
  • IMG_1782.JPG
    IMG_1782.JPG
    144.2 KB · Views: 177
Malila na wataalam wengine, naomba kupata shule kuhusu thinning ya Pinus caribaea inafanyika baada ya umri gani na inatakiwa iwe katika spacing ipi unapopanda na unafanya thining baada ya muda gani na kwa vigezo gani? naambatanisha picha za kishamba changu hapa ambacho nilinunua maeneo ya ziwa victoria.

Kimsingi thinning hufanywa kama shamba lilipandwa kwa kukosea spacing au ni shamba la maotea. Spacing ya miti ndio hutoa matarajio ya product yako, unapokuwa na spacing kubwa utapata miti michache, lakini yenye kutoa mbao za size tofauti tofauti kulingana na soko linasemaje. Unapokuwa na spacing ndogo, unalazimika kuwa size fulani ya mbao tu, sasa size hiyo kama haina soko ndio utakuwa umeumia.

Spacing nzuri kwa pines ( kama pinus patula) ni 3m x 3m, kuna wengine sasa hivi wamekwenda mbali zaidi, 3m x 4m. Lengo ni kupata miti yenye diameter kubwa, na hivyo kuwa na uchaguzi unapokuja kuvuna, hasa size ya ubao. Kwa hiyo kama spacing yako ulitumia 2.5m x 3m, inabidi ufanye thinning,ili ubaki na 3m x 3m kama una lengo la kupata mavuno mazuri.

Ingekuwa eucalyptus tungezungumza kitu tofauti.

Ukifanya thinning mapema ni bora zaidi, hasa chini ya miaka mitano, nimeona wengi wakifanya ktk kipindi hicho. Sababu kubwa ni kupata mavuno mazuri.
 
Ahsante sana Malila, ngoja nitafanya homework vizuri ili nijue exactly spacing ya miti katika shamba lote baada ya baadhi ya miti kushindwa kustawi ili nifanyie kazi mapendekezo yako muda ukifika.

Ahsante
 
Uza miti mkuu upate pesa isiyokupa mawazo! Kwa umri huo hukosi laki 1 kwa kila mti, hivyo unatengeneza 100 m bila jasho maana wanunuzi wanakufuata mpaka home!

Wapi huko?
 
Back
Top Bottom