Nahitaji kulima Mahindi na Mpunga Msowero-Kilosa, Morogoro. Naomba ushauri toka kwa yeyote mwenye uzoefu huko

Nahitaji kulima Mahindi na Mpunga Msowero-Kilosa, Morogoro. Naomba ushauri toka kwa yeyote mwenye uzoefu huko

Mr simple M

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2020
Posts
2,202
Reaction score
4,653
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu nataka kwenda kuwekeza kwenye kilimo cha mahindi na mpunga huko Msowero.

Swali langu je, nitapata mazao ya kutosha kwa eneo hilo yaani hali ya hewa na rutuba kwa ujumla ipoje hasa kwa kilimo cha mpunga na mahindi?

Natanguliza shukurani.
 
Mkuu wazo zuri sehemu uliyo target ipo vizuri ila naomba nipandikize wazo lingine katika mawazo yako,najua una nia iliyothabiti ila mkuu mimi naona ilikuwa bora zaidi wewe kununua hayo hayo mazao unayo yaitaji kuyalima ili kuepuka hasara huenda labda ukashindwa kuvuna kile kiwango ulichokusudia.
 
Connection ya mashamaba ipoje huko? Bei na hupatikanaji wake.
 
Mkuu nina uzoefu kiasi na kilimo cha mpunga, kiufupi na kwa ushauri, nunua mpunga wakati wakulima wanavuna afu uza au koboa mchele wakati wanaanza kilimo, kulima hakuna faida yoyote zaidi ya hasara na risk kubwa.
 
Mimi nina uzoefu na biashara ya kuuza nyungu. Baada ya kupiga sana hela Corona ya tz Sasa niko Nairobi, napiga hela kwenye Corona phase ll
 
Mkuu nna uzoefu kiasi na kilimo cha mpunga, kiufupi na kwa ushauri, nunua mpunga wakati wakulima wanavuna afu uza au koboa mchele wakati wanaanza kilimo, kulima hakuna faida yoyote zaidi ya hasara na risk kubwa
Wazo zuri mkuu naomba unipe maelezo kwa kirefu zaidi yaani yaani nanua kwa maeneo gani hasa yenye bei poa kwa apo Morogoro
 
Wazo zuri mkuu naomba unipe maelezo kwa kirefu zaidi yaani yaani nanua kwa maeneo gani hasa yenye bei poa kwa apo Morogoro
Mvomero na Kilombero..... Wakati wa mavuno, bei huwa inakua chini, wakati wa kilimo bei huwa inakua juu mana mpunga unakua haupatikani na wakulima wengi Wanahitaji pesa kwa ajili ya kilimo
 
mkuu wazo zuri sehemu uliyo target ipo vizuri ila naomba nipandikize wazo lingine katika mawazo yako,najua una nia iliyothabiti ila mkuu mimi naona ilikuwa bora zaidi wewe kununua hayo hayo mazao unayo yaitaji kuyalima ili kuepuka hasara huenda labda ukashindwa kuvuna kile kiwango ulichokusudia.
Uko sahihi; kukusanya mazao wakati wa mavuno ni bora zaidi kuliko kulima. Kulima ni very risk maana mvua zikizidi mazao yanaenda na mafuriko na zikikataa ushakodi mashamba na kulima ni hasara pia; lakini ukisubiri mavuno yakigoma hela yako inapona unaangalia kingine cha kufanya.

By the way kukusanya mazao process yake ni rahisi na inaokoa muda na gharama kuna muda wakulima wanakuletea ulipopiga kambi we kazi yako ni kupima na kuhifadhi tu mzigo wako.

Kilimo cha umwagiliaji angalau kidogo japo nacho process ni nyingi tena kama unakodi shamba la mtu ujue kila unapotaka kulima unalipia mbaya zaidi mashamba mengi ni machafu full vichaka mtu anakupa ili umsafishie akiona umepata msimu huu ujue msimu ujao anakunyima analima yeye
 
Mkuu nna uzoefu kiasi na kilimo cha mpunga, kiufupi na kwa ushauri, nunua mpunga wakati wakulima wanavuna afu uza au koboa mchele wakati wanaanza kilimo, kulima hakuna faida yoyote zaidi ya hasara na risk kubwa
Mi nilijaribu kulima mahindi mwambao mwa mto wa bwawa la kihansimaeneo ya Chita; kilimo cha umwagiliaji. Initially ilionekana ni rahisi coz maji yapo karibu sana na ardhi ilikua imenona maji, daah from nowhere kina kikapungua likapiga jua la hatari kumbuka mvua ilizidi mwaka jana kuja mwaka huu so majarubani hapakulimika mpunga so wadau tukaona tukaweke mahindi maana ndo kawaida baada ya mavuno ya mpunga tunaweka mahindi tunapiga kilimo cha umwagiliaji.

In short vurugu zilikua nyingi mara mashine za maji zisumbue mara boko wavamie mazao usiku wale; mara wafugaji walishe mifugo yao mashambani; yani kila siku ni majanga tu hamuishi kupelekana mahakamani na wafugaji. Nimeambulia gunia 2 kwenye ekari 5 mategemeo yakiwa kupata gunia 50-100.

Umekodi shamba; kulimiwa; umenunua mashine ya kumwagilia;mbolea; dawa; palizi; mafuta ya mashine na takataka zingine kibao; stressful!!!
 
Mi nilijaribu kulima mahindi mwambao mwa mto wa bwawa la kihansimaeneo ya Chita; kilimo cha umwagiliaji. Initially ilionekana ni rahisi coz maji yapo karibu sana na ardhi ilikua imenona maji, daah from nowhere kina kikapungua likapiga jua la hatari kumbuka mvua ilizidi mwaka jana kuja mwaka huu so majarubani hapakulimika mpunga so wadau tukaona tukaweke mahindi maana ndo kawaida baada ya mavuno ya mpunga tunaweka mahindi tunapiga kilimo cha umwagiliaji...
Vipi mkuu kiongozi huwezi kufanya kilimo tena
 
Vp mkuu kiongozi huwezi kufanya kilimo tena
Siwezi acha kufanya kilimo coz sio mara ya kwanza kuangukia pua hua inatokea mara moja moja; lakini nataka nijipange km mwaka hivi niwe na mashamba yangu mwenyewe in future Mungu akijaalia niwe hata trekta dogo itasaidia kidogo kupunguza gharama za uendeshaji; ila kwa msimu huu unaokuja nitakusanya tu mpunga kwanza japo bei mwaka huu imekataa sana;

Mwaka jana mwezi kama huu gunia la mpunga debe 10 lilikua linasimamia laki na elfu 10 na lilifika adi laki na 30 mwezi wa 12 ila mwaka huu adi huu muda tunaongea hata 70 wateja ni wa kubembeleza just imagine tumekusanya kwa elfu 50-65 by June....ila hakuna kukata tamaa tunakaza tu adi kieleweke uzuri mpunga hauozi hata miaka mi5 unakaa ndani [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Msowero mahindi na mpunga utapata, suala hapo upate wenyeji wenye uchungu na wewe, wakupeleke kwenye mashamba yenye tija, Kiboko asali, kwa Rames, kwa Lilah, kwa Slim, mikongeni n.k.

Shida ya hicho kijiji na vijiji vingi vya Kilosa ni utapeli mwingi, ardhi yenye rutuba na mabonde yenye maji yapo, ila hivyo vijiji vya Kilosa vina laana ya ulozi, unafiki, fitina na utapeli, uwe makini!

Kila la heri mkuu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Vp kwa mashamba ya mambegwa yana rutuba mkuu
 
Vp kwa mashamba ya mambegwa yana rutuba mkuu
Mambegwa ndiko kwenyewe, ila kama huna mwenyeji, unaweza kupewa shamba kumbe ni bwawa au ndiyo njia ya maji, msimu wa mvua.

Tulishahama huko, ule mto, unahama kila mwaka! Mara maji yameenda Karadasi, mara maji yameenda shuleni, mara maji yapo kwa Rames...

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Tahadhari,
Uwe makini sana kilosa ni wilaya iliojaa matapeli wengi sana.Nilishapata tatizo huko na taarifa hizi nilizipata kituo cha polisi kimamba.
Nakutakia kila la kheri.
 
Mkuu wazo zuri sehemu uliyo target ipo vizuri ila naomba nipandikize wazo lingine katika mawazo yako,najua una nia iliyothabiti ila mkuu mimi naona ilikuwa bora zaidi wewe kununua hayo hayo mazao unayo yaitaji kuyalima ili kuepuka hasara huenda labda ukashindwa kuvuna kile kiwango ulichokusudia.
Hafu akishanunua afanyeje boss
 
Msowero mahindi na mpunga utapata, suala hapo upate wenyeji wenye uchungu na wewe, wakupeleke kwenye mashamba yenye tija, Kiboko asali, kwa Rames, kwa Lilah, kwa Slim, mikongeni n.k.

Shida ya hicho kijiji na vijiji vingi vya Kilosa ni utapeli mwingi, ardhi yenye rutuba na mabonde yenye maji yapo, ila hivyo vijiji vya Kilosa vina laana ya ulozi, unafiki, fitina na utapeli, uwe makini!

Kila la heri mkuu!

Everyday is Saturday............................... 😎
Laana ya asili kabisa[emoji16]
 
Back
Top Bottom