Nahitaji Kulima Wilaya ya Kilosa, Naombeni Ushauri Wa maeneo yasiyo na mafuriko

Nahitaji Kulima Wilaya ya Kilosa, Naombeni Ushauri Wa maeneo yasiyo na mafuriko

Kilosa ni kubwa sana. Mikumi, kidodi, magubike, dumila, vidunda yote kilosa. Upo kilosa ipi? Unatarajia kulima mazao gani?
Sipo kilosa mkuu, nahitaji kulima mahindi na mpunga ila nina wasiwasi na mafuriko

Wapi mafuriko hayasumbui kwa maeneo uliyotaja?
 
Wazee bado hamjanijibu...

Wenyeji wa kilosa na viunga vyake nawasubiri wazee...
 
Uko serious au unajaribu, kama uko serious mpunga unaweza lima maeneo ya Kilangali, Mvumi, Mlegeni, Kimamba n.k. mahindi yanalimwa karibia vijiji vyote.
Niko serious sana mkuu ila nahitaji maeneo ambayo hayana mafuriko kwasababu nakwenda na familia
 
Uko serious au unajaribu, kama uko serious mpunga unaweza lima maeneo ya Kilangali, Mvumi, Mlegeni, Kimamba n.k. mahindi yanalimwa karibia vijiji vyote.
Mvumi huwa kuna mafuriko?
 
Mawasiliano ya ofisi hayo. Nilipewa namba ya mdau wa kilimo nikamuuliza kuhusu details ulizonipa akawa anataka pesa kwanza so nikampotezea.
  • Halmashauri ya Wilaya Kilosa
  • Telephone: 023 2623093
  • Mobile: 0737847880
  • Fax: 023 2623333
  • Email: [email protected]
Asante sana mkuu, nashukuru kwa muda wako
 
Back
Top Bottom