Nahitaji kununua kuku kwa bei rahisi

Nahitaji kununua kuku kwa bei rahisi

Mdusi94

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2017
Posts
3,657
Reaction score
3,391
Habarini wana jamvi letu pendwa,

Nauhitaji wa kununua kuku wa kienyeji kwa bei rahisi (chini ya Tsh 10,000/=) kama kuna mdau anafahamu sehemu (kijiji/kata, wilaya au mkoa) basi naomba anitajie, nina access ya kufika popote pale Tanzania.

AHSANTENI
 
Hakunaga kitu kinaitwa bei rahisi kabla ya mkataba wa manunuzi au mauziano.

Bei ambayo kwako unasema ni rahisi kwa mwenzako inaweza kuwa ni kubwa na ngumu kumudu.

Nadhani ungeweka ofa yako mezani kwa maana ya unatafuta kuku wa uzito gani na jinsia gani hata rangi kama unapendelea iwe pekee then chagua halafu weka offer yako mezani wauzaji watakutafuta.
 
Ni kweli kama alivyosema Zemanda maelezo yako hayajajitosheleza.

Anyway, umesema una access ya kufika kokote Tz! Basi tembelea maeneo yafuatayo kuku wanapatikana kwa urahisi sana (ila sijajua bei yake);

Moshi (v) vijiji vya Kata za Kahe, Kyomu, Chekereni mpaka Mwanga... Makambako; vijiji vya ubena, utengule na kule mlowa... Kondoa kata za Darabi, Masange, Mnenia, Chungai, Bambare... Pia Dodoma wilaya ya Mpwapwa, vijiji vingi kuku wa kienyeji wanapatikana kwa urahisi sana, Kila la kheri.
 
Ahsante , chini ya Tsh 10,000/=
 
nayajua hayo maeneo huyu ndug yetu afike huko atakushukuru sana
 
Back
Top Bottom