Nahitaji kuoa

Nahitaji kuoa

YAHERI MUNGU

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
318
Reaction score
215
Habari za wanaJF?

Mimi ni kijana kitanzania, nipo hapa Dar es Salaam. Baada ya kushughulika na michakato ya maisha, hasa kuweka mikakati mizuri.

Sasa muda wa kuoa ndiyo umefika. Sasa ninahitaji kuoa, kuwa na mwanamke ambaye umri wake siyo zaidi ya miaka 30.

Kuhusu kabila mimi sibagui. Ila mwanamke huyo asiwe mpenda maslahi! Mimi na yeye tutatafuta tukiwa pamoja.

Atakayekuwa tayari, tafadhali tuwasiliane ili tuweze kuelezana zaidi.

Asanteni.
 
Habari za wanaJF? Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 36, nipo hapa Dar es Salaam. Baada ya kushughulika na michakato ya maisha, hasa kuweka mikakati mizuri, sasa muda wa kuoa ndiyo umefika. Sasa ninahitaji kuoa, kuwa na mwanamke ambaye umri wake siyo zaidi ya miaka 30. Kuhusu kabila mimi sibagui. Ila mwanamke huyo asiwe mpenda maslahi! Mimi na yeye tutatafuta tukiwa pamoja. Atakayekuwa tayari, tafadhali tuwasiliane ili tuweze kuelezana zaidi. Asanteni.
umri huo mpaka sasa bado hujaoa mmmh
 
Aiseeeee.....[emoji15] [emoji15]
Yaani miaka 36 ndio unataka kuoa...[emoji47] [emoji47]
 
Heeeee !! Mtafute nae maisha?? Siyo Wa humu jf[emoji2]
 
Kama umeshaweka maisha mzuri sawa haina haja ya kupata wa kutafuta nae maisha. Ww oa yoyote utakayeona anafaa maana maisha ushayapata.
 
unataka asiezidi miaka 30 inaonekana umri wako umesogea kidogo.... i doubt 35above... alafu kuna sharti umeweka hela mtatafuta wote, nikwambie kitu wadada wa siku hizi wanapenda mteremko, umuoe walau akukute umepiga hatua kadhaa,hata akikutambulisha kwao au kwa best zake watamuuliza jamaa anafanya kazi gani ? at that age unaonekana hujajipanga kabisa yan aje muanzie point A.. pole sana pengine ulijipa moyo mambo yatajipa, unajikuta umri unakimbia na vyuma vimeumana kisawasawa
 
Back
Top Bottom