Nahitaji kurudishiwa pesa ya installment

Kweli mkuu kweli ni KIPAJI...kwa kuwaamini watu nimepoteza sana na hadi kupoteza marafiki...natamani kuwa na roho mbaya nisikopeshe tena ila ninashindwa

Japo ni kazi na ni vigumu lakini nimeanza kujifunza kusema sina pale nnapoombwa mkopo, watu wanafikiri unapomsaidia kwa kumkopesha una pesa ya ziada kumbe umejibana kwa kujali tatizo lake. Yeye anataka aje akurudishie akipata hela ya ziada ambayo hata hajui ataipata lini na hana uhakika nayo. Mbaya zaidi wewe unashindwa kufanya mambo yako ambayo mdai wako anayafanya na pesa yako hakupi huku msmbo yake yanaendelea.
Ni bora kuvunja urafiki kwa kumwambia mtu sina kuliko hii ya kumpa alaf madai inakua ugomvi. Usamaria kazi sana.
Kuna jamaa ni wa nchi nyingine tunafanya nae kazi, kuna siku nilimwazima pesa yani yeye ndio ananiambia tuandikishane contract anasema ili hata kama akifa kabla ndugu zake hawajachukua mwili wake niwaambie namdai marehem.
Ila kutokana na mazoea yetu ya kuaminiana nikajisikia vibaya kama ataona simwamini
 
Du...dada!!!!?!😡

Ha ha haa nimecheka sana, huenda ni kwa vile ameona Mbuni anakufukuza na yuko kwa ukaribu sana akajua hii sio kidume! natania mkuu, unajua hizi ID zetu inabidi kua makini sana kwa sababu hazionyeshi kama mtu ni kijana, mzee, mama, dada, au kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…