Hivi hii huduma Shirika la Reli huwa hawana? Na kama hawana, wanaweza kushauriwa ili wawe nayo especially SGR itakapoanza kufanya kazi? Kwa sababu wakiweka angalau Behewa moja tu la aina hiyo kwa kila Trip ya treni Dar-Mwanza, na watu wakawa wanajua kuwa wanayo huduma hiyo, hili behewa lazima lijae. Nashauri SGR itakapoanza kufanya kazi, TRC waweke Behewa moja kwa ajili ya magari kama mzigo. Na itawalipa kwa sababu mtu kuendesha gari Dar Mwanza inaghraimu mafuta ambayo si chini ya laki moja na hii ni kwa gari ndogo zinzotumia mafuta vizuri kama vile Toyta IST. Sasa wao wakiweka fee ya laki moja kwa kila gari, ina maana behewa moja kwa safari moja linaweza kuwalipa angalau million 1, na hata likienda Mwanza halafu likarudi tupu bado litakuwa limewalipa