Nahitaji kushona masikio na kuweka jino moja la bandia.

Joined
Mar 16, 2018
Posts
9
Reaction score
6
Kwanza habari za wakati huu,
Mimi ni kijana kutoka jamii ya kimasai, wazazi wangu walinitoga masikio na kung'oa jino la chini kama mila na desturi za kabila letu. Sasa walinifanya hivyo nikiwa mdogo sana, sasa baada ya kukuwa nikaja kutambua kuwa waliniaribu sana,
.1. Je kuna uwezekano wa kushona ? Na je hospitali zipi ziko vizuri kwa kushona? Na inaweza kunigharimu shilingi ngapi?

2. Je jino la bandia ambalo sitoi wakati wa kula nyama nitapata kwa bei gani? Na je hilo jino la bandia lina madhara yeyote?

3. Na nimekuwa nikipata shida kutamka baadhi ya maneno mfano ( ZA VA THA n.k) je nikiweka hilo jino nitaweza kuyatamka vizuri?
 
Ndugu, badala ya kusikitikia sikio ungeweza kujivunia utamaduni wako. Kwamba umeweza kuhimili yote hayo katika umri mdogo (siku hizi wanaita kovu la thamani).

Kati ya makabila ambayo yanapaswa kuheshimiwa ni wamasai. Kwa sababu ni watu wanaomudu mazingira magumu kuliko labda watanzania wengine wote. Wewe ni mshindi, survivor. Hilo sikio na jino lina Historia ambayo mkeo na watoto wako watafurahia sana kuisikiliza kwa upendo.

Kuhusu jino, unaweza kuweka hospitali. Jino la kudumu ni kama sh laki 5 hivi, lakini nakushauri ongea na clinic kadhaa kama hauna insurance ili ulinganishe gharama. Sidhani kama lina madhara, kwa sababu nawajua watu kadhaa ambao wameweka na hawana tatizo.
 
Kuna jamaa mmoja aliwekewagwa jino akalimeza kesho yake tu
Kila la kheri mkuu
 
Ndugu, badala ya kusikitikia sikio ungeweza kujivunia utamaduni wako. Kwamba umeweza kuhimili yote hayo katika umri mdogo (siku hizi wanaita kovu la thamani).

Kati ya makabila ambayo yanapaswa kuheshimiwa ni wamasai. Kwa sababu ni watu wanaomudu mazingira magumu kuliko labda watanzania wengine wote. Wewe ni mshindi, survivor. Hilo sikio na jino lina Historia ambayo mkeo na watoto wako watafurahia sana kuisikiliza kwa upendo.

Kuhusu jino, unaweza kuweka hospitali. Jino la kudumu ni kama sh laki 5 hivi, lakini nakushauri ongea na clinic kadhaa kama hauna insurance ili ulinganishe gharama. Sidhani kama lina madhara, kwa sababu nawajua watu kadhaa ambao wameweka na hawana tatizo.
Asante kwa ushauri wako, nitafanya hivyo
 
Jivunie utamaduni wako. Hakuna ulazima wa wewe kufanana na kila mtu, ona fahari kwa kuwa tofauti
 
Back
Top Bottom