ben mjukuu
Member
- Apr 27, 2015
- 59
- 8
Wakuu habar zenu
Twende kwenye mada mimi ni kijana, nilipenda sana siku moja niishe katika ndoto zangu ambapo nilipenda nije niwe mtu fulani katika jamii yangu nisaidie watanzania wenzangu na hata familia yangu, nilisoma kwa bidii sana mchepuo wa biashara niliamini ungenipeleka katika fani niipendayo ya uhasibu, matokeo ya kidato cha nne hayakuniruhusu niendelee hivyo nikapata fomu ya kujiunga na chuo baada ya hapo nikafaulu vizuri sana nilikaa mtaani mwaka mzima kisha kuajiriwa serikalini.
Sasa kila mara wazo la kutimiza ndoto yangu ya kuwa mhasibu linanijia mara kwa mara kiukweli naipenda hiyo kazi toka moyoni kabisa tangu nikiwa fomu 1 nilinuia kuja kuwa mhasibu ila kwa sasa ni muajiriwa serkalini. Nashindwa nianzie wapi kutimiza malengo yangu wakati mwingine nawaza kurist ili nisome advance au nitafute chuo kwa ngazi ya cheti nije diploma na hatimae digrii na wakati huo nikitaka kusoma fani tofauti na niliyo nayo hairuhusiwi hapo pana nipa ugumu sana sijajua nifanye nini, kazi inakuwa ngumu sana kama sio chaguo lako.
Shida za nyumbani zilinisukuma kusoma hiyo kozi sikuwa na jinsi sasa nataka kurudi katika fani niipendayo. Ombi kwenu vijana wenzangu na wakubwa zangu nisaidieni kimawazo nyie mlifanikiwa vipi kufikia ndoto zenu na kuziishi, msaada wenu ni muhimu sana kwangu wadau.
Natanguliza shukrani zangu, asanteni sana.