Nahitaji kuuza Vocha za Jumla,nitazipata wapi?

Nahitaji kuuza Vocha za Jumla,nitazipata wapi?

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
1,691
Reaction score
640
Wakuu nipo Mbeya mjini,kuna mtu wangu wa karibu anahitaji kuuza vocha za simu kwa bei ya jumla ila anashindwa kujua wapi atazipata.Amekwenda ofisi za Voda,Airtel na Tigo hapa Mbeya mjini lakini amekuwa akielekezwa kwenda kwa wauzaji wengine ambao hata kama akichukuwa kwao hawezi kuuza akapata faida.

Niliwahi kuambiwa kwamba kwa vodacom vocha zao zinapatikana Simbacom hapa town,lakini inaonekana hawa simbacom ni kama hawaoperate tena hapa mjini kama mwanzo.So,najua kuna watu wana ufahamu wa hili naombeni msaada tafadhali.
 
Waheshimiwa naona mnapita kimya kimya tu,ndio kusema hakuna mwenye idea ya hiki kitu kweli?
 
Ulizia Shivacom au Alphatel au Planetel hao ndio dealers wa Vodacom.Pia nenda Voda waombe wakuambie wapi utapata vocha kwa jumla!
 
Back
Top Bottom