Nahitaji kuwashtaki Vodacom

Sio lazima claimant amjue ni nani aliyeshiriki kumletea hasara negligence inaweza kuwa ya kampuni bila ya kumjua aliefanya kosa exactly hayo ya internal investigation watajijua wenyewe humo ndani ya voda. Mahakama inatambua kosa la mfanyakazi ndio kosa la shirika zima kwenye negligence.

Mahakama inachojali ni kuona ushahidi wa majukumu ya vodacom kuhakikisha wakala asilipe bila ya kupata alert fulani kutoka kwao, ushahidi wa kuwa kuna mtu kafanya breach (ambayo chanzo chake ni ndani kwao), na hasara za mtu. Muhimu hapo kama mtu mwingine awezi kufanya hicho kitu zaidi ya kuwa yupo ndani anashirikiana na wajinga wenzake na ikija bainika hivyo wanatakiwa kula fine ya nguvu sana.

Huo upelelezi wa polisi ni sehemu nyingine kama wanataka kuwakamata wahalifu walioshiriki nje ya shirika lakini hasara za huyu jamaa voda wanatakiwa walipe.

Hiyo situation kama ni kesi basi ina makosa sehemu nyingi sana kiasi kwamba wakili awezi kuwakosa sehemu moja; unaweza kuiwekea product mbovu (maana ya system inayosababisha hasara), unaweza kuiwekea contract ya kuwa wakala anatakiwa kutimiza wajibu a chini ya makubaliano na voda hivyo akishatimiza voda anatakiwa atimize wajibu b kwa njia walizokubaliana whoever interferes with the systems sio tatizo la claimant bali defendant.

Hivi ndio vitu vinafanya nchi za wengine makampuni kuwa makini sana na wafanyakazi na ndio vyanzo vya vitu kama code of conduct na ethics za kazi. Ihis is the one of the many reasons binafsi nimeanza kuona kwanini sisi atuendelei mambo kama haya kuchekewa voda wanatakiwa kupigwa fine kubwa tu hapa serikari lazima iwawajibishe watu kuwa makini kwenye kutoa huduma zao kama tunataka ubora na uadilifu wa makazini.
 
Boss...wala usipoteze muda wako umepigwa...na siku nyingine uwe makini zaidi...usitoe hela kabla huja hakiki kwenye flot yako...usithibitishe kwameseji....zinatengenezwa....
 
Boss...wala usipoteze muda wako umepigwa...na siku nyingine uwe makini zaidi...usitoe hela kabla huja hakiki kwenye flot yako...usithibitishe kwameseji....zinatengenezwa....
Nani anajukumu la kuziba fault processes? na kwanini sheria inataka kuona 'reasonable company/manufacture test' kwenye services au bidhaa zao kuhakikisha zina ubora iwaje huyu afanye vitu vyote anavyofanya kila siku lakini apigwe? Ndugu mahakama inatambua hayo ni majukumu ya kampuni sio wakala kama ndio anavyofanya hila safari hii imekuwa tofauti au ata kama wamebadilisha processes yeye awajamtaarifu wanatakiwa kulipa na kupigwa fine still tena ya nguvu huu ni uzembe tu kutoka kwao.

Hivi vitu rahisi sana tanzania ukienda nchi za watu ukiingia supermarket wakitoka kupiga deki wanaweka kabisa na alama ya slippery flow, wengine wanafunga kabisa na aisle yenyewe isiwe tabu maana akiteleza mtu hapo ujue imekula kwako. Sasa mtu ambaye system za kampuni zimemfanya apoteze chake halafu unasema voda hawausiki ur not serious dunia zingine kuna wanasheria wapo kwa sababu ya shughuli kama hizi tena no win no fee lakini wanasaka fine kubwa sana.
 
Yahusu airtel ;wakuu naomba ushauri nimelipia bill ya maji tangu mwezi uliopita kupitia airtel money mpaka leompesa hazijaingia dawasco nimekatiwa maji kila nikiwasiliana na airtell naambiwa wanashughulikia ndani ya nusu nitakuwa sawa tangu mwezi uliopita hadi leo maji nimekatiwa tayari nifanye nini?au niende polisi ni zaidi ya shs 3000000
 

Utakuwa umeridhika, au we ni Lowassa..? Maana uvumilivu wako umeenda chuo.

Yaan kila siku unaambiwa subir nusu saa na we unaingia line mpaka mwezi umeisha ..? Hahaha
 
Kuna kitu watanzaniatuna lack sana, elim ya teknohama, hili ni tatizo dogo sana, kama ukipata mwanasheria mzuri

Kwa mfano : Naamin ya kuwa kwa system kubwa kama ya Mpesa, operations zote zinazofanyika, weather ni ya mteja, wakala au operator lazima kuna sehem record inahifadhiwa, ya kilichofanyika na nani alikifanya , kitaalam zinaitwa activity log, hizi records huwa hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuzibadilisha au kuzifuta, labda system super administrator ambae ndan ya kampun anakua mmoja au wawili tu ( manager akiwa mmoja wao ) , na hata operators huwa hawawez kuziona, kwa hiyo kama kuna ujanja ulifanyika, labda operator alifuta muamala uliofanyika kwenye account yako, its certain kwamba hiyo operation aliyofanya imerekodiwa, kwa hiyo mtu mwenye access ya kuangalia logs zilizofanyika, akiangalia kwenye system account ya operator lazima ataona huo ujinga tu aliofanya..!

Tatizo sasa linapokuja ni endapo kama watasema, wao kwenye sheria zao za kazi wanaweza kumwadhibu muhusika, lakin kamwe usitegemee kuwa watakubal icho kitendo kilifanyika, hii ni kwa ajili ya kulinda reputation ya kampuni yao..!

Kwa mimi ningekushaur kwanza uende HQ kupeleka madai yako, then kule wakijichanganya either hata kusema " inaonyesha kuna sehem kuna tatizo" au kalugha chochote cha kuonyesha uko sahihi, then you can take it from there if you need to sue them, if you win a lawsuit against a company like voda we ni bilionea hata kama kosa ni dogo kias gan..!

But ukijifanya unaenda polisi kwanza, bro itakula kwako
 
Hii nchi ina watu wa ajabu sana. Kuna watu hapa wanalazimisha hili liwe kosa la vodacom wakati ni kosa la mtoa huduma kwa kukosa umakini.

Mkuu amini nnachokuambia,mimi pia ni wakala,lkn kwa tatizo lako umeibiwa! Ipo hivi,kwa nyie mlio na mazoea ya kuwapa wateja simu wa-type namba zao wanapo-deposit hapo ndo kosa huwa lianzia. Huwa wanaangalia namba ya simu ya TILL akishachukua namba anafanyakazi ya kutafuta ujanja wa kuona salio lako. Na kwa vile una mazoea ya kutoa simu ya kazi,ataliona tu. Baada ya hapo atasave number yake kwenye simu yako na kuipa jina MPESA.
Baadae kati ya massage anazokuja kutoa hela hapo kwako,ataedit mojawapo na kukuforwadia.

Na kwakweli unaweza kuamini km ni muamala halali lkn ni sms ya kawaida. Fuatilia vizuri hiyo sms utakuta ni ya kawaida. Ndo maana ukiwauliza watu wa mpesa hawawezi kuona. Lkn ukiuwauliza sms za siku huyo za kawaida watakuambia. Pole sana mkuu UMEIBIWA!!
 
Basi Voda kuna tatizo! Tatizo hili limemtokea jamaa yangu ingawa yeye si wakala!. Ilikuwa hivi alinunua tiketi ya ndege. Baadaye shirika la ndege wakasema tiketi zimeisha wakaamua kumrudishia ela kupitia voda. Voda wakamtumie Sms ela yako imerudi .baadaye anafanya manunuzi, voda wakamwambia hauna salio. Akacheki salio lipolakini akifanya muamala wowote hamna salio. Akawatwangia 100. Wakamjibu fedha zako ziko hewani kuna mambo hayajakaa sawa asubiri siku tatu. Akawatwangia shirika la ndege. Wakasema walishatuma ela hizo .Atarudi voda kwa 100, Wakamjibu kijeuri kwamba hawana la kufanya asubiri siku tatu. Rafiki yangu akaamua kuweka issue public! Akawapandia kwenye account zao zote za mitandao kuhusu suala hilo. Ndani ya nusu saa ela zake zilikuwa tayari zilisharudi.
 
Kweli ni upumbavu sana wa haya makampuni ya simu kutoa siku tatu wakati ni issue ya kuingia kwenye system na ku credit muhamala tu,jamaa alifanya Poa ni kuwachana kuanzia JF,Facebook,Instagram na Twitter.
 
nenda kwenye vodashop zao na vithibitisho vyote wanaweza wakakusaidia, hela inawezekana ilirudi tena kwa mteja (hii hutokea) hawa customer care hawaaminiki saa nyingine ni vilaza balaa
kwenda kuwashitaki kwa tshs 300,000 japokua hata ni hela ndefu kwako, it's not worth it
 
milioni 3 ukalipia kwa kutumia airtel money?.......ila hapa we wafuate kwenye makao makuu yao, wakikuzingua washitaki, it's worth it
 
papiso, vipi kale kamgomo baridi mlikokaandaa hapo vodacom hq customer care wote kwamba erolink wanawanyonya maana feb. ndo hii. nahisi hii ndio sababu mnatupiga sana kwenye M-PESA sio?!
 
Mimi nilikamisha laki tatu na hamsini tangu mwaka jana kwenda bank zile hela hazijafika bank na wao kila siku wananiambia linashughulikiwa. Vodacom ni wezi sana.
 
Kaka wajanja wameshakupiga hakuna mtu anayeweza kuhack mpesa never never.na hiyo sms haijatoka vodacoma kama huamini angalia message centre number ya hiyo sms na linganisha na message centre number ya mpesa
 
Njia iliyotumika kukutapeli ni hii, yawezekana kuna siku ulimpatia mteja handset yako unayotumia kutuma pesa akaingiza codes fulani ambazo kila unapofanya muhamala taarifa anazipata, au anaweza kusave number yake kwa jina la M-PESA kwenye simu yako, so kilichotokea baada ya kujua kiasi kilichopo kwa account yako anatengeneza message ambayo itaendana na salio lako, akifanikiwa tu kukutumia message hiyo na wewe ukaipokea ukimpa pesa tu imekula kwako!
Ushauri wangu kwako siku nyingine usimpe mteja kuweka number yake unapomtumia pesa na badala yake aandike number yake kwenye karatasi au kwenye daftari then ndio ufanye muhamala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…