Sijajua upo wapi ila ingekuwa kwa upande wangu wazo la kwanza lingekua ni MICROFINANCE. Kwa mtaji huo ukiuwekeza kwene microfinance ukiwa na usimamizi mzuri, software ya uchakataji wa taarifa, ufuatiliaji mzuri kwa wateja kuanzia kabla ya kukopa na baada ya kukopa basi Una possible ya kudouble hio pesa mara mbili kwa mwaka maana ukiwekeza million 150 una uhakika wa profit ya 10 million kila mwezi kama faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji kama mishahara na kadharika.
Lakini wazo la pili ni ununuzi wa mazao hasa maharage, harage halijawahi kukata kama mimahindi, unaweza ukawa na vyumba vyako hapo hom au ukakodi sehemu, kipindi hiki ni cha mavuno ukachukua million 100 ukanunua maharage na million 50 ukanunua mpunga by mwezi wa 12 bei hupanda sana na utatengeneza faida kwa zaidi ya 35% ya pesa yako.
Wazo la tatu fedha hio fanya passive investment UTT japo return yake ni ndogo but atleast ni safe na security ya kutosha, utakua huna hofu na mtaji wako pamoja na faida.
Kama utashindwa sana basi fungua duka kubwa au kampuni itakayo deal sana na masuala ya angribusiness kama uuzaji wa mbolea, madawa ya kilimo, vifaa vya kilimo cha kisasa na makorokoro mengi yanayohusika na kilimo na mnyororo wa uongezaji thamani wa mazao ya shambani.