Ipo hivi, ukitoka huko kijijini kwenu hadi panda basi la usiku ili ufike Dasalamu pale Magufuri Bus Terminal asubuhi, kisha panda mabasi hapa Dar tunaita (mwendokasi) japo siku hizi siyo mwendokasi tena, hadi kituo cha (nadhani Azania au posta, nauli ya hilo basi ni 750/-.
Ukishuka hapo muulize muhudumu wa kituoni ukiwa unatoka akuonyeshe ofisi za Kilimanjaro Fast Ferries au Zan Fast Feries -Mwendokasi ya majini.
Pale unakata tiketi kwa kitambulisho ndg Mtanganyika, kisha utafuata utaratibu hadi unaingia chomboni.
Ukifika nchini Zanzibar au kisiwa cha Unguja, utashuka na kukaguliwa utambulisho wako kisha utaibukia barabarani kukutana na boda, tax, bike na waongozaji local kwa wageni kukupeleka unapotaka.
Kule mtu anakupeleka hadi unapotaka hata usipomlipa but kwa utu mpe hata 2000/-.
Sehemu za kulala Unguja; hapa usije dhania ni sawa na hapa Tanganyika asee kule guest ni za kutafuta sana na room ya bei ya chini kabisa ni 25,000 ambapo ukiona hicho chumba ni sawa na room ya elf8 au 10 hapa T/nyika.
Usafiri na Chakula: Usafiri nauli madhani kwa sasa zimepanda but route fupi ni 500 na route ndefu kama kutoka mjini kwenda shamba huko ni 1,400/- hiyo ndo nauli kubwa.
Chakula; asee jiandae kula chips kuku paja nono, supu kwa boflo, juice kwa andazi au ukikosa sana ulojo hivi ndiyo vyakula common sana kule.
Ukitaka sembe au walikwa muda wa mchana inabidi uulize kwenye vijiwe (siyo maskani) kwa eneo utakalokuwepo sababu mama lishe siyo wengi ni wa kutafuta sana, labda jioni pale darajani.
Ila kwa eneo unalotaka kwenda huko site ni full ugali, wali kwa samaki au nyama ng'ombe, sababu wamama kutoka bara wanapiga kazi hasa kupika.
Swali ...