Hiyo betri kama nayo imelala kwenye gari miezi 2, itakuwa imeshaisha chaji au imekufa kabisa..Kuna gari imepaki nyumbani muda mrefu hivi kama miezi miwili bila kuguswa likiwa na mafuta kidogo sana.
Leo nikasema ngoja nijaribu kuliwasha nikapige nalo misele. Nikazungusha funguo mpaka pale kwenye on bila kupiga starter halafu nikawasha na AC.
Baada ya kama dk 10 hivi nikaona dashboard inafifia kama battery inaisha na AC ikazima.
Nikajaribu kupiga starter halikuwaka tena.
Hapo kunaweza kukawa na shida gani?
Nimehisi kitu kama hiki, kwamba battery imekufa, nikasema niulize nipate uhakika.Hiyo betri kama nayo imelala kwenye gari miezi 2, itakuwa imeshaisha chaji au imekufa kabisa..
Jaribu kuwasha kwa kutumia betri nyingine ambayo una uhakika inawasha magari mengine..
Hii ikigoma, mwite fundi Maiko afanye yake..[emoji41][emoji41][emoji41]
Nimehisi kitu kama hiki, kwamba battery imekufa, nikasema niulize nipate uhakika.
Shukrani mdau.
Toyota Harrier.