Barca
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 1,448
- 1,624
Habari za mida hii wanajukwaa. Mimi ni mjasilia Mali nimenunua incubator ni natotoresha mayai ya kware, kuku wa kienyeji na Malawi. Sasa kwa Kipindi tangu nianze hii kazi wateja wanaohitaji vifaranga wa broiler wamekuwa wengi sana. Kuna kampuni nilikuwa naagiza vifaranga kwao ila wamekuwa wasumbufu sana kupata oda ulizoagiza kiasi kwamba hadi wateja wakafikiri ni tapeli. Sasa ili kuondoa hii Dhana nimeona nutafute haya mayai nayapataje na bei gani? Nitashukuru sana kama nitafanikiwa. Incubator yangu ina uwezo wa kubeba tray 30. Kwa hiyo kama yatapatikana nitakuwa na uwezo wa kuchukua kila mwezi tray 30. Natanguliza shukrani