Jambo Jambo,hatujajua umeshafanya lipi na lipi so far,ila inashauriwa kuweka mbolea ya wakati wa kupanda miche hadi siku 20 za kwanza yenye N.P.K ratio ya walau 30.10.10(unaweza kosa madukani yenye mgawanyo huo unaweza changanya mwenyewe mbolea tofauti zikupe huo mgawanyo) kiasi cha 200Kg(mifuko 4) kwa ekari moja,
Alafu kuanzia siku 45-60(kama swali lako linavyo uliza) unaweka mbolea ya pili sasa yenye Nitrogen nyingi peke yake kama Urea..,
ZINGATIA: Weka kilo 80 - 120 kwa ekari 1 za 30%N - 46% N (yaani kati ya (30-0-0) mpaka (46-0-0)) yoyote hapo kati kati, weka kwa kutawanya hakikisha unaweka maji eneo uliloweka mbolea ndani ya siku 5.
Ukabarikiwe upate mavuno mazuri.