Nahitaji Mbolea ya kukuzia yenye matokeo chanya kwenye zao la mpunga

Nahitaji Mbolea ya kukuzia yenye matokeo chanya kwenye zao la mpunga

Mhina Martin

Senior Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
144
Reaction score
189
Mbolea gani nzuri ya kukuzia niweke kwenye mpunga Wangu mpaka Sasa tangu kupandwa una Siku 45 itafaa kuleta matokeo chanya ya mavuno mazuri shambani wakulima wazoefu wa kutumia mbolea naomba muongozo
 
Ingefaa kwanza kusema katika hizo siku 45 umeshatumia mbolea gani? Je, ulitumia mbolea ya kupandia? Na pia ingefaa ungesema unalima wapi
 
Jambo Jambo,hatujajua umeshafanya lipi na lipi so far,ila inashauriwa kuweka mbolea ya wakati wa kupanda miche hadi siku 20 za kwanza yenye N.P.K ratio ya walau 30.10.10(unaweza kosa madukani yenye mgawanyo huo unaweza changanya mwenyewe mbolea tofauti zikupe huo mgawanyo) kiasi cha 200Kg(mifuko 4) kwa ekari moja,
Alafu kuanzia siku 45-60(kama swali lako linavyo uliza) unaweka mbolea ya pili sasa yenye Nitrogen nyingi peke yake kama Urea..,
ZINGATIA: Weka kilo 80 - 120 kwa ekari 1 za 30%N - 46% N (yaani kati ya (30-0-0) mpaka (46-0-0)) yoyote hapo kati kati, weka kwa kutawanya hakikisha unaweka maji eneo uliloweka mbolea ndani ya siku 5.

Ukabarikiwe upate mavuno mazuri.
 
Back
Top Bottom