Nahitaji mchumba (Mke)

Nahitaji mchumba (Mke)

Habari, jina langu halisi ni Baraka, nina miaka 39.
Kwa sasa, niko katika hali ngumu maishani. Sina makazi wala mali, na bado najitahidi kujenga maisha yangu upya. Hata hivyo, nina imani kwamba hali yangu itabadilika kwa wakati na mimi nitakuwa sawa baada ya muda.

Natafuta mwanamke mwenye moyo wa huruma, ambaye atakuwa tayari kushirikiana nami katika kipindi hiki cha changamoto. Ninahitaji mtu ambaye atakubaliana na mimi katika hali yangu ya sasa, na ambaye atakuwa na imani na mimi wakati nikijitahidi kusimama tena.

Ninajua kwamba maishani kuna changamoto, lakini pia kuna matumaini. Kama utakuwa tayari kupokea mapenzi yangu na kuwa sehemu ya safari yangu ya kujitafuta, nitashukuru sana.

Tafadhali, ikiwa unajiona kuwa na uwezo wa kuwa pamoja katika safari hii, usisite kuwasiliana nami. Ningependa kujua zaidi kuhusu wewe na kuona kama tunaweza kuwa na uhusiano wa maana.

Asante kwa kusoma ujumbe wangu, na natumai tutapata fursa ya kuzungumza zaidi.
Pole sana broo, achana na habari za mapenzi focus kwenye nyeto huna vigezo vya kumiliki mwanamke 🥶
By the way hii ni chai
 
King focus on you right now,
huna kazi mambo yako sio mazuri, huyo mchumba utamlisha nini?
Mchumba atapata mimba mzae utajipa stress ngumu sana...
Focus baba focus
 
King focus on you right now,
huna kazi mambo yako sio mazuri, huyo mchumba utamlisha nini?
Mchumba atapata mimba mzae utajipa stress ngumu sana...
Focus baba focus
Kwani MCHUMBA unaishi nae?
 
Kwani MCHUMBA unaishi nae?
Usimpotoshe huyo kijana..... unaishi na mchumba or not
huwezi kuwa na mchumba na huwezi kumnunulia hata body lotion na chupi, taking her out here n there
Atakuwa na unnecessary stress right now what he should be looking is job/ au njia ya kutengeneza pesa
PERIOD!!
 
Mumuoneeni huruma jamaa sababu cha kwanza jamaa ni Yatima chapili anapokaa ni mbali sana.

Kuhusu pesa msiwaze mtakula kiapo na pia mtakula Jeuri yenu.
 
Back
Top Bottom