Mkuu pole sana kwa changamoto zilizokukumba,
Kuna muda huwa inafikia tunalazimishwa kujikuta tunaamini katika miujiza.
Usitegemee miujiza, miujiza ni uvunjifu wa kanuni za uhalisia wa dunia.
Hapo utaanza hata kuamini kutembea juu ya maji unaweza, ingawaje hapo ndugu Archmedes alikuja na kanuni yake nzuri kabisa.
Na kanuni kama hii (kanuni za uhalisia wa dunia) kamwe haiwezi kuvunjika.
Hivyo kwa kusema hivyo na mifano hiyo, miujiza inabaki theoretically tu kuwa inawezekana kanuni za ulimwengu huu zinawezekana kuvunjika.
Ila kiuhalisia haiwezekani
Kwahyo, ulipofikia wewe si sahihi kutegemea miujiza ya wachungaji zaidi utakutana na matokeo ya Placebo Na hyo ni psychology tu si reality.
Na watakuibia sadaka hao unaowatafuta.
Suluhisho hapo ni kupambana, omba misaada ya kimawazo na chapa kazi kisawa sawa.
Unaweza tueleza changamoto yako ni ya aina gani tupate kukupa ushauri uliobora na wa kina?