Mkuu Mwamba028 uzoefu ninao wa kutosha kabisa.
Nimeopt kilimo cha matikiti coz soko lake ni la uhakika na ni favourable kwa mkulima kama atazingatia usimamizi ili apate quality product.
Hakuna mtu alishawahi kuangushwa na kilimo hiki labda ardhi ikatae na timing akosee. Vinginevyo ni uhakika wa kuchuma pesa takatifu kabisa.
kweli wakulima wanatabu sana. mi mwenyewe najitahidi kusave na nimejiunga kwenye saccos fulani hivi. vipi, siku hizi unakopesheka?
Mlishaanza? Mi nahitaji kufanya hiki kilimo unasemaje nikijumuika nanyi?Mkuu Mwamba028 nakukaribisha sana ndg yangu uje tuanzishe mchakamchanga tungali vijana, tusingoje fainali za uzeeni ni majanga na magonjwa ya moyo!
Mkuu Mwamba028 uzoefu ninao wa kutosha kabisa.
Nimeopt kilimo cha matikiti coz soko lake ni la uhakika na ni favourable kwa mkulima kama atazingatia usimamizi ili apate quality product.
Hakuna mtu alishawahi kuangushwa na kilimo hiki labda ardhi ikatae na timing akosee. Vinginevyo ni uhakika wa kuchuma pesa takatifu kabisa.
Mimi ningekushauri hivi:
Mosi, kama kilimo unchokiongelea kinaanza msimu wa mwakani usiwaze mkopo. Jipangie malengo ya unatarajia kulima kiasi gani na bajeti kwa makisio itakuwa kiasi gani kisha anza kufanya saving kwa ajili ya kilimo. Kama kweli unaweza lipa laki sita mkopo kwa mwezi, makadirio ya hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili ni zaidi ya Tshs 4m. Hii pesa inatosha kwa kuanza kilimo na gharama zitakazoongezeka utazicover na mshahara wako wa mwezi. Kumbuka njia hii inafaa zaidi kwa kilimo kidogo na cha kati (chini ya ekari 30).
Pili, kama unalenga kufanya kilimo kikubwa fanya yote niliyokuambia hapo juu uhakikishe angalau una pesa kiasi ya kuanzia kilimo. Kisha mtafute rafiki, ndugu au jamaa ambaye mnaweza unganisha nguvu na kulima angalau ekari 50 na kuendelea na mlimie pamoja. Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye hii njia ni kumpata mtu mwenye commitment ya kweli na malengo yayofanana au kuelekeana. Hii ni nzuri sana mkiifanya kisasa na ikiwa na matokeo chanya utafurahia kilimo lakini pia ikitokea ukapata matokeo hasi shambani basi hautaumia peke yako.
Mwisho, kilimo ni zaidi ya kupata mkopo benki, Kuna mambo mengine muhimu ya kuzingatia na mojawapo ni usimamizi thabiti wa mradi wako wa kilimo. Hii ni changamoto kubwa sana kwa wakulima walioajiriwa, jipange sawia kwenye hili pia sambamba na kupata mtaji wako wa kilimo.
Mkuu unaonaje kama tukiunganisha nguvu ili tugenerate mtaji sisi wenyewe?
Mimi mtaji wangu ni;
1) shamba lenye uhakika wa maji
2) waterpump horsepower5.5, 3" na vifaa vyote vya bustani
3) muda na kujitolea kwa moyo wangu wote kuweza kujikita shamba hata kwa zaidi ya miezi 12
4)Uzoefu wa kilimo cha umwagiliaji
5) rafiki ambaye ni afsa ugani aliye tayari kunisaidia kwenye masuala ya kitaalam kuhusu kilimo cha bustani.
Kama upo tayari nakuomba tuanze kilimo cha MATIKITI MAJI ekari 2, tutatumia mbegu ya HYBRID aina ya SUKARI F1 kwa mchanganuo ufuatao;
1)mbegu kwa ekari2 ni sh 520,000/=
2)spacing: shimo 120cm, mstari 150cm na kila shimo miche 2
3) kila shina litazaa matunda 3 tu.
4) gharama za kulima ni sh 150,000/= plus kununua delively pipe 150metres sh 200,000
5) petrol+oil mpaka kuvuna sh 200,000
6)viuatilifu (pestsides) sh 100,000
Kwakuwa hekta1=10,000sqm
Hekta1=acres 2.5
Then kwenye heka 2 ni mashimo 2*4000sqm/1.8sqm=4444
Kila shimo mashina2. Kila shina matunda3
Grand Total ya matunda ni 2*3*4444=26,664.
Mkuu shamba langu ni jipya lina rutuba ya kutosha kabisa kiasi cha kutohitaji mbolea nyingine. Ndiyo maana sikuona umhimu wa kujumuisha bajeti yake.
Matikiti ni kilimo cha umwagiliaji make linahtaji maji yaliyodhibitiwa hivyo hulimwa kwa timing hasa kipindi hiki mvua hamna.
Kuhusu hofu ya faida ya kimahesabu, usiogope na ndiyo maana nikashauri tu-deduct Tsh 20M kwenye hiyo faida. Kinachobaki bado ni faida nzuri sana ambayo inatumotivate kuendelea na mladi.
Shamba langu lipo Turiani Mvomero 300kms from DSM.
Kama tutaanza mapema, kunauwezekano wa kulima mara3 kabla ya ujio wa mvua kubwa march 2015.
Usiogope mkuu kila kitu kinawezekana ukiwa na nina na moyo wa kujitoa.
TWENDE SHAMBA MKUU.