Kwanza pole sana mkuu,nimeona nianzie huku japo nimeona pia uzi wako mama!!
Nachotaka kushauri mkuuu ni kama ifuatavyo,[emoji116][emoji116][emoji116]
Moja ya side effect ya lockdown ndio hii,wapo wengi wanaopatwa na shida kama hizi mkuu ila goja nijikite kwako
_ kwa kipindi hiki nakushauri sana ujiepushe kukaa peke yako, kama ikiwezekana naomba (kama ni mpenzi wa kusikiliza nyimbo) sikiliza ukiwa peke yako chumbani au popote,hii itakufanya u relax na kusahau hili.
_pili fanya mazoezi, kimbia ukiwa unachukua tahadhari za corona, unaweza ukawa una tune hata ka muziki kidogo then automatically you will start forgetting this!
_ ongea na wanafunzi wenzako,mbadilishe mawazo wao wanafanya nini kipindi hiki wawapo nyumbani, kufanya vile utajikuta unaona kitu cha kawaida
Kingine kikubwa mkuu punguza kuwaza kuhusu mtihani, hebu kabla hujawaza vile fikiria ni wangapi wamekumbwa na hili tatizo? Je uko peke yako? Hivyo chukulia ni janga la kidunia kikubwa tuzido kuomba kwani ni wengi wamekutana na shida hizi pengine yako ni ndogo!! Labda ni kupe mkasa mmoja though it's not so good to share it here in!!
Kuna mama mmoja anafanya kazi kiwanda fulani stakitaja,alinipigia simu anauliza kama serikali watafunga yaani tutawekwa lockdown, yule mama anasema ndani hana chakula,kodi ya nyumba imeisha,mtoto wake ambaye ni mwanafunzi anazurura hovyo,mama yake mzazi anaumwa sana,then nikampa pole akaniambia ameamua kufunga na kusali ili Rais asifunge yaani kuwekwa lockdown maana hajui ataishije!!!
I was shocked kusikia vile lakini kiukweli yule mama alikuwa analia nikaelewa kiukwel watu wanapitia magumu, coming to the main point, shukuru sana ndg hata kwa hatua hiyo uliyofikia then sali kwani Mungu atatusikia, ni wengi wenye shida ndg!!
MTANGULIZE MOLA WAKO, EPUKA KUSIKIA HABARI MBAYA HASA ZA CORONA IKIWEZEKANA USIFUATILIE TAARIFA KAMA HIZO KWANI ZITAKUONGEZEA STRESS NDG!! MUNGU YU PAMOJA NASI,ATATUVUSHA!!
Sent using
Jamii Forums mobile app