Nahitaji mnitie nguvu

Nahitaji mnitie nguvu

Pole sana mkuu.

Iko hivi: kila kitu kina hasi na chanya Kama ni hivyo basi kuna siku mambo yataenda vibaya pia Kuna siku yataenda vizuri.
Pia maisha bila changamoto yangekuwa hayana maana, ila kupambana nazo na kuzishinda ndio kunaleta maana ya maisha.
Hivyo usiogope changamoto bali zikija pambana nazo mpaka ushinde, na hapo ndipo unapopata maana ya maisha.

Maisha ni Mapambano na Hakuna Kukata Tamaa.
 
Poleeee, Ila tafuta ka-shughuli ka kufanya huko. Waone hata wale ma-broo wako wa kitaaa waliojiajiri upige dili. Laa sivyo life na hii corona Ni gumu Sanaa.
 
Pole sana mkuu kwa unayopitia,inaonekana una msongo wa mawazo sana,punguza maana matokeo yake utaishia kupata madonda ya tumbo,kujiua ,kisukari nk.

Ili kuondoa msongo wa mawazo na kuwa mwenye furaha hebu tumia huu mlonge,tafuta majani yake yakaushe juani kisha yasage na upate unga,baada ya hapo chemsha maji kikombe kimoja na tia kijiko kimoja cha unga wa mlonge acha ipoe kisha unywe, kutwa Mara tatu,hadi upate nafuu.

Naandika hivi kwa uzoefu ,nimewahi kupitia kipindi kama chako,matokeo yake niliishia kupata madonda ya tumbo,pia epuka kutumia dawa za kupunguza maumivu kama huwa unazitumi,dawa kama diclodenac na marafiki zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujafanya kosa kwenda kusoma medicine(??pregabaline), utatusaidia baadaye. Ongea na marafiki zako,soma novels
 
Kwanza pole sana mkuu,nimeona nianzie huku japo nimeona pia uzi wako mama!!

Nachotaka kushauri mkuuu ni kama ifuatavyo,[emoji116][emoji116][emoji116]

Moja ya side effect ya lockdown ndio hii,wapo wengi wanaopatwa na shida kama hizi mkuu ila goja nijikite kwako

_ kwa kipindi hiki nakushauri sana ujiepushe kukaa peke yako, kama ikiwezekana naomba (kama ni mpenzi wa kusikiliza nyimbo) sikiliza ukiwa peke yako chumbani au popote,hii itakufanya u relax na kusahau hili.

_pili fanya mazoezi, kimbia ukiwa unachukua tahadhari za corona, unaweza ukawa una tune hata ka muziki kidogo then automatically you will start forgetting this!

_ ongea na wanafunzi wenzako,mbadilishe mawazo wao wanafanya nini kipindi hiki wawapo nyumbani, kufanya vile utajikuta unaona kitu cha kawaida



Kingine kikubwa mkuu punguza kuwaza kuhusu mtihani, hebu kabla hujawaza vile fikiria ni wangapi wamekumbwa na hili tatizo? Je uko peke yako? Hivyo chukulia ni janga la kidunia kikubwa tuzido kuomba kwani ni wengi wamekutana na shida hizi pengine yako ni ndogo!! Labda ni kupe mkasa mmoja though it's not so good to share it here in!!

Kuna mama mmoja anafanya kazi kiwanda fulani stakitaja,alinipigia simu anauliza kama serikali watafunga yaani tutawekwa lockdown, yule mama anasema ndani hana chakula,kodi ya nyumba imeisha,mtoto wake ambaye ni mwanafunzi anazurura hovyo,mama yake mzazi anaumwa sana,then nikampa pole akaniambia ameamua kufunga na kusali ili Rais asifunge yaani kuwekwa lockdown maana hajui ataishije!!!

I was shocked kusikia vile lakini kiukweli yule mama alikuwa analia nikaelewa kiukwel watu wanapitia magumu, coming to the main point, shukuru sana ndg hata kwa hatua hiyo uliyofikia then sali kwani Mungu atatusikia, ni wengi wenye shida ndg!!

MTANGULIZE MOLA WAKO, EPUKA KUSIKIA HABARI MBAYA HASA ZA CORONA IKIWEZEKANA USIFUATILIE TAARIFA KAMA HIZO KWANI ZITAKUONGEZEA STRESS NDG!! MUNGU YU PAMOJA NASI,ATATUVUSHA!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ndo maana mungu hajibu maombi yetu ya lockdown? Wakati tunaomba lockdown kumbe kuna wengine wanafunga lockdown isiwepo? Bora uhai, huyo mama wavumilie kama sisi kuliko kupata hili gonjwa bora kuvumilia hii shida. Huyo mtoto wake bora awe na afya kuliko kupata hili gonjwa.

Mungu tu naomba lockdown kunusuru watu
 
WE SI WAKUTUCHEKA KIVILE NA UKADIRIKI KUSEMA MARA OHH NIKIRUDI MSHAHARA UTAONGEZWA MARA OOH NITABADILISHWA POST SASA KIKO WAPI
 
No pain no gain sir,katika kila kutafuta lazima upate jaribu kama kipimo cha wewe kumudu yanayokuja,usikate tamaa,shikilia hapohapo mpaka kieleweke,hiyo ndio njia ya mafanikio kwa watu wengi kama sio wote,kaa ukijua hakuna mafanikio rahisi,ingawa wengi wakishafanikiwa wanasahau kuwaambia wanaotafuta mafanikio kuwa walipitia njia ngumu sana kufika walipo...
 
  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Kipindi hiki cha Corona kinazidi kunipa mawazo ya kukata tamaa ya kusoma na kuona tutazidi kuchelewa kumaliza nimekuwa ni mtu wa kulala tu na kuamka na kuwa na mawazo yasiyoisha 24 hrs kuhusu kusoma kwangu mbona naona kama mambo yangu hayaendi nimekuwa ni mtu wa huzuni tu naona kama kila mtu ananiangalia mimi mana niliacha kazi na kwenda kusoma saizi nakosa hata ela ya vocha jamani najiona tofauti tu na binadam wengine jamani kuna baadh ya watu nawakimbia naona aibu kuonana nao.
Upo form ngapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom