asante mpenzi.
mi niliposoma tu, niligundua huyu bado ni mdogo sana. mi nina miaka 26 na sijaguswa na mwanume. yeye ana 23 na kishaumizwa zaidi miaka 7 iliyopita na sasa ameandaa kamkataba akidhani ni muarobaini wa kuumizwa! kweli shetani anawatesa watu! kwa kweli niliposoma niliona nisijihangaishe kujibu kitu, ila nilipoona jibu lako nikaona nikuunge mkono.
mdogo wangu umri wako ni mdogo sana. sijui umefika kiwango gani cha elimu na maisha kwa ujumla, lakini kwa umri wako na mipango uliyonayo, ni mapema sana. zingatia alichoshauri dada yetu Gaga na wengine. asante.
nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza.
praise the Lord