Nahitaji msaada nasumbuliwa na hili tatizo

Mr Yes

Senior Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
153
Reaction score
29
Nimekuwa nikisumbuliwa na vipele vidogo vidogo vingi sana usoni,kifuani na mgongoni kwa muda mrefu sana,vipele hivi vinakuwa kama ngozi ya kuku,nimekuwa nikishauliwa kutumia mafuta na vitu mbalimbali bila mafanikio,sasa naomba mnisaidie niepukane na hali hii kwani inanikosesha raha sana.
 
mkuu pole
mtafute daktari wa ngozi, ushauri wangu ndio huo. Matibabu yana challenge nyingi kwani lazima ihusishe kupima n.k
 
Nimekuwa nikisumbuliwa na vipele vidogo vidogo vingi sana usoni,kifuani na mgongoni kwa muda mrefu sana,vipele hivi vinakuwa kama ngozi ya kuku,nimekuwa nikishauliwa kutumia mafuta na vitu mbalimbali bila mafanikio,sasa naomba mnisaidie niepukane na hali hii kwani inanikosesha raha sana.

Ushauri mzuri ni kwenda hospitalini kucheki afya yako ndiyo utaweza kugundua tatizo linasababishwa na nini na nini tiba yake.
 
Au umerogwa?? Ngozi ina vipele kama kuku!! That's so serious.. Anza kwa mganga wa jadi uchungulie labda kuna mtu anakuchezea..

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ungeweza kumuona Doctor MGonda ni doctor mzuri sana wa ngozi,pia kama ungeweza kumtafuta mansoor daya anaicheck ngozi yako pale pale anatengenezea dawa na mwisho kuna skin clinic ipo hapa namanga juu kidogo ya best bite inaitwa premier cafe kuna skin proffesional mzuri sema uwe na mfuko mzuri guarantee ya kupona ipo.
 
ahsante sna mkuu,tiba yake hapo namanga inaweza fika sh ngapi ili nijipange
 
Au umerogwa?? Ngozi ina vipele kama kuku!! That's so serious.. Anza kwa mganga wa jadi uchungulie labda kuna mtu anakuchezea..

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

no thank you
 
ahsante sna mkuu,tiba yake hapo namanga inaweza fika sh ngapi ili nijipange

Kwa namanga nadhani appointment ya kumuona ni kama 30-40,huko kwenye dawa haizidi 60 so piga hesabu
 
Back
Top Bottom