kancher
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 472
- 472
Habari wakuu! Pooleni na majukumu ya kazi, bila kupoteza muda ningependa kuandika ujumbe wangu moja kwa moja.
Ninapitia changamoto kubwa ya kipato kwa sasa, huku nikiwa na familia inayonitegemea ya mke na mtoto mmoja. Najua maisha ni kupambana, na ndiyo maana najitokeza kwa unyenyekevu kuomba nafasi yoyote ya kazi halali – iwe ni kazi ya kutumia nguvu au akili.
Elimu yangu ni certificate ya custom anda tax management, lkn Nina ujuzi wa kufundisha mazoezi ya viungo (physical fitness) na huduma kwa wateja (customer care). Pia nina uzoefu katika kazi za ofisini, ukusanyaji wa mapato, na kazi za ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli ndogondogo za kiserikali na kibinafsi, pia nina uzoefu wa kufanya kazi za kusimamia na kuendeleza miradi na kukuza miradi kwa kutumia nguvu na akili.
Nipo tayari kufanya kazi sehemu yoyote, hata mazingira magumu – mradi ni kazi halali. Hii ni sauti ya mtu ambaye yuko tayari kufanya chochote ili ajikomboe kimaisha na kuijenga familia yake kwa heshima na bidii.
Kama unafahamu fursa yoyote au uko tayari kunisaidia kwa namna yoyote, tafadhali nitafute inbox kwa maelezo zaidi. Ujumbe huu unaweza kumgusa mtu sahihi – tafadhali saidia kusambaza.
Asante sana kwa moyo wa huruma.