Nahitaji msaada wa kisheria ndugu zangu

Asante kwa ushauri ,nikweli kwa waswahili aina yoyote ya ukaribu hutafsrika kama kufanya mahusiano namke wa mtu,kwahyo kesi niachane nayo tu mkuu.
 
Watu wapwani wanamabifu sana sana
 
Asante kwa ushauri ,nikweli kwa waswahili aina yoyote ya ukaribu hutafsrika kama kufanya mahusiano namke wa mtu,kwahyo kesi niachane nayo tu mkuu.
Achana nayo,wakati mwingine usipende sana kutafuta haki haki mengine achilia nature ifanye kazi.
Suala lako ukimwambia mwajiri kwa ushahidi atalipa uzito atakuhamisha hata ndani ya mkoa.
 
Naelewa the situation! Onyo usitafute haki kabisa ukiwa maeneo hayo unless unataka Uifate hiyo Haki watu waseme "Umetangulia Mbele ya Haki"..

Huwezi kuipata Haki kwa mtu alinuia Kisasi,Huwezi kuipata suluhu kwa Mtu mwenye Hasira huwezi kupata Msaada hapo na wala usiitafute vinginevyo wakikushindwa huko watakutafutia Zengwe na nakuApia kuwa Hilo zengwe hautachomoka na ndo itakuwa mwisho wako..

Utapoteza kazi yako,Heshima yako na hata utu wako...

Umri wako ni Mdogo sana bado kijana mdogo Bado unasafari ndefu sana usiharibu safari yako kwa kiburi cha kushawishiwa na watu..

Wengi walioharibu Future zao ukiuliza watakuambia "niliambiwa na watu nisiachie mpaka nipate haki yangu" lakini wote sasa ndo wanaipata Haki kwenye Magereza na jela..

Nikuulize hivi unafikri wanaopakaziwa kesi za kuiba madawa ya Hospitali sio watu?
Wanaambiwa wamebaka wajawazito sio watu?
Wanaoambiwa mtoto kashindwa kupata huduma na kafia Hospitali sio watu?
Wanaopewa kesi za kitaaluma zinazopelekwa kuamriwa na Baraza la madiwani (Humo ambamo Mbaya wako yumo) sio watu?..

Kijana kabla hujafanya maamuzi yenye "Ego" ndani yake Fikiri kwanza umefikaje huko Lindi, fikiri Muda uliosoma ,Fikiri kama una watoto au mke fikiri kama una future yako..

Fikiri watu wanaokutazamia au kukutegemea..
Ukishafikir Vyote hivyo ndyo ufanye maamuzi..

Kesi zote hutengenezwa mitego huwekwa bhasi jihadhari usiwe mmoja ya walio kwenye mitego na kesi maana hutatoka..
 
Achana nayo,wakati mwingine usipende sana kutafuta haki haki mengine achilia nature ifanye kazi.
Suala lako ukimwambia mwajiri kwa ushahidi atalipa uzito atakuhamisha hata ndani ya mkoa.
Hii coment nzuri sana isikilize na inabdi upeleke malalamiko kbla huyo diwani (Mwanasiasa) hajakupeleka Kwenye baraza la madiwani kwa utovu wa Nidhamu
 
Dahhhh,umenisema snaa hapa mkuu hadi nimetoa chozi hapa,suluhu nikuondoka nakuwithdaral case kutoka police
 
Hii ndiyo Tz,unakufa unajiona
 
UKISema watu wa Lindi wana roho mbaya sikuelewi kabisa,mimi msukuma wa kanda ya ziwa,huu ni mwaka wa kumi niko liwale kwa wangindo nafundisha huku mpigamiti shule ya msingi,watu hawa si wagomvi hata kidogo,ni watu wema sana ,ila kwa kesi ya mke wa mtu nakupa pole,

Nimekaa huku sijawahi ona wala kusikia mtu kauawa kwa kucharangwa mapanga wala ugomvi wowote.
 
Ukiona hal ya hatarish kwa ufanis wa kaz zako na uhai wako nenda direct kwa mkurugenz wako mwambie na ukumbuke serkal ina work on paper bila maandsh apo sku sio nying pengo lako ltazibika kiutendaj na kwenye familia yako ndio pengo litabak mwambie nia yako ya kuomba kuamishwa imedtly kutokana na hal hatarish akigoma omba kuacha kaz au ondoka halmashaur iyo nenda tume ya utumish wa umma dodoma waeleze jambo lako kwa maandish uamisho utakukuta nyumban ukiwa salama sasa we lelux apo kijijin usipozkwa bila kuagwa
 
Kukubali kuwa umeshindwa napo pia ni ushindi ndugu.

Hakimu wa kweli ni Mungu, muachie akuhukumie. As long as wewe mwenyewe unajua ukweli katika nafsi yako basi usiwe na haja na mengine.

Mwenye dhamira yake haachi mpaka itimie. Dhamira ya huyo mtu ni kukuangamiza, hatotulia mpaka atimize jambo lake.

Nusuru nafsi yako na weka imani kuwa Mungu atakulipia.
Huo uongo aliokuzulia hauna mashiko nje ya hapo ulipo. Ukiondoka hapo utaacha mabaya yote hapo hapo.

Kila la heri na Mungu akusimamie.
 
Omba kuhamishwa haraka sana.
Onesha kuwa una dharura nyingi kuzidi muda wa kazi kila siku.
 
Suluhu ni kuhama hapa,naona ndio jambo la muhimu hata nduguzangu wameniambia nihame
 
Ina maana Mke wa Diwani mna mawasiliano? Ya kikazi? Ni mwajiriwa mwenzio? If not, mmekutana wapi hadi mkaanza kupigiana simu?? Sitaki kuwa biased
 
Kaka sijamkula wala kuwaza tu hizo mambo ,hapo Nikua alikua anatumia namba ngeni napia namba ambazo zilikua anaitumia nnazo kwa maswala ya kiusalama zaidi ndio maana nimekuja hapa kuomba ushauri .jambo nizito sana
Namba za Mke wa Diwani zinakusaidiaje kiusalama?? Something is not adding up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…