Ni kweli i'm 31 near to celebrate my 32 birthday ...kuna jamaa mmoja nilikua nnamsimulia faragha hii inshu akanishauri the same as you ila sasa kwa upande wake alisema endapo haujafanya nakweli unakiri haujafanya komaa upate haki yako,ila kama umemto-m-mba kimbia mara moja,kusema ukweli mm sijafanya kabisa sina haja ya kuficha hapa ndio maana roho inaniuma , nahili nitukio lakutengeeneza kufuatia kudorola kwa mapato katika pharmacy yajamaa aliyekua anahudumu pale kijijini kabla ya ujio wangu katika kile kituo kwayo mm ndio kama nekua barrier yayy kuuza dukani kwake badala yake wagonjwa wanakuja kituo cha afya/zahanati kupata huduma
Naelewa the situation! Onyo usitafute haki kabisa ukiwa maeneo hayo unless unataka Uifate hiyo Haki watu waseme "Umetangulia Mbele ya Haki"..
Huwezi kuipata Haki kwa mtu alinuia Kisasi,Huwezi kuipata suluhu kwa Mtu mwenye Hasira huwezi kupata Msaada hapo na wala usiitafute vinginevyo wakikushindwa huko watakutafutia Zengwe na nakuApia kuwa Hilo zengwe hautachomoka na ndo itakuwa mwisho wako..
Utapoteza kazi yako,Heshima yako na hata utu wako...
Umri wako ni Mdogo sana bado kijana mdogo Bado unasafari ndefu sana usiharibu safari yako kwa kiburi cha kushawishiwa na watu..
Wengi walioharibu Future zao ukiuliza watakuambia "niliambiwa na watu nisiachie mpaka nipate haki yangu" lakini wote sasa ndo wanaipata Haki kwenye Magereza na jela..
Nikuulize hivi unafikri wanaopakaziwa kesi za kuiba madawa ya Hospitali sio watu?
Wanaambiwa wamebaka wajawazito sio watu?
Wanaoambiwa mtoto kashindwa kupata huduma na kafia Hospitali sio watu?
Wanaopewa kesi za kitaaluma zinazopelekwa kuamriwa na Baraza la madiwani (Humo ambamo Mbaya wako yumo) sio watu?..
Kijana kabla hujafanya maamuzi yenye "Ego" ndani yake Fikiri kwanza umefikaje huko Lindi, fikiri Muda uliosoma ,Fikiri kama una watoto au mke fikiri kama una future yako..
Fikiri watu wanaokutazamia au kukutegemea..
Ukishafikir Vyote hivyo ndyo ufanye maamuzi..
Kesi zote hutengenezwa mitego huwekwa bhasi jihadhari usiwe mmoja ya walio kwenye mitego na kesi maana hutatoka..