mimi ushanishinda wewe mtuok.usijibu pm ya mtu
mpaka ufike 21.....lol
naona bora hilo swala uachane nalo tu-kama kakayako ana tabia ya mtindo huo,inamaana kila siku utakuwa unamwombea misamaha?
cha kufanya wewe mshauri kaka yako,atulie,mpe mifano hai,maana afanyayo anayajua,kuliko kumfata huyo binti tena,unaweza kumfata then mwisho wa siku kka yako akaharibu tena
ushauri wangu nijaribu kutokuwa mtu wa kati katika mahusiano ya mtu yoyote utaishia kuumia wewe...mapenzi ni ya 2
oooh afadhali umemtolea uvivu maana alitaka kukupanda uyontajibu tu.samahani lakini
jamani The Boss,hapa unaongea na mtoto wa miaka 17,majibu makali we watunzie vingunge wa mmu.sijui tukushauri nini kwa kweli.....
labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol
mwanangu Marida,huyo kaka yako ana umri gani? Nyumbani vipi utoto wenu mlikuwa mnafungiwa ndani sana? nauliza hivi isije ikawa kaka yako ndo kwanza anaibukia mambo ya mjini kwa pupa.
La mwisho nakushauri kwa umri wako si rahisi kujua mwanamke gani anafaa kuolewa katika boma lenu,jaribu kujiweka pembeni,na hilo jibu la wifi yako umesema hutalisahau mi nasema lisahau tu,maana kwa mtindo huu wa kakako si ajabu kabla hujafikisha miaka 25 atakuwa amekutambulisha mawifi mia.
Bila shaka bado unasoma,kazania kitabu mwanangu,kakako asikupasue kichwa na uhuni wake.
ONYO KWA WANA MMU WOTE:
JIHADHARI NA UKIMWI,UNAUA!
jamani The Boss,hapa unaongea na mtoto wa miaka 17,majibu makali we watunzie vingunge wa mmu.
kwa jinsi nilivyokuelewa nahisi kuwa huyo kaka yako bado hajawa tayari kuoa, ila anamkumbuka yule binti kwa sababu kaka yako amechunwa sana na videmu ambavyo ni your age mates. ni kweli kuwa ni kaka yako lakini nakushauri kabla ya kuongea na huyo binti kwanza ni lazima umwambie kaka yako abadilike kwa tabia yake aliyonayo vinginevyo utakuja kubeba lawama kutoka kwa wifi yako
Jambo la pili mwambie kaka yako aende aongee na huyo binti wao wawili kwani wao ndio wanandoa wakae na wakubaliane wakishakubaliana wewe uwepo ili kuwasupport lakini nakushauri usiende kumwombea ndugu yako msamaha
Unahangaisha kichwa kwa ajili ya bro, acha ajihangaikie mwenyewe na wewe hangaika na yakwako, haya ukimpata huyo dada then ukawaunganisha siku akija kumtenda nani atabeba lawama? Dada mapenzi ni ya wawili tu ukiingia wewe wa tatu utakuwa ni uongo huo, kwanza nimeona una miaka 17, it means bado uko mwanafunzi yanini kufuatilia mapenzi ya kaka badala ya kufuatilia shule?lol
ya ngoswe mwachie ngoswe.
Halafu ulijuaje kama huyo dada anamfaa kaka yako? Je ulijiuliza kama kaka yako anamfaa huyo dada?
La mwisho hiyo tabia acha ndo nyie mawifi mnaoingilia ndoa /mambo ya kaka zenu.(huu ni mtazamo tu, pole kama nimekukwaza)
kweli Mkuu!embu turudi kule kwa wavulana/wanaume,kuna mtu hajatokea namsubirimkuu
ndo maana nilipomuuliza age,nimenyamaza lol
sijui tukushauri nini kwa kweli.....
labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol
Habari zenu wana jf,mi mgen humu ndani,nilikuwa naomba msaada wenu wa kimawazo kuhusu hili.
Kaka yangu alimpenda msichana mmoja.mara za mwanzo mwanzo msichana alikuwa hampendi,ikafika sehemu mpaka akaanza kumpenda taratibu kadri walivyozidi kuwa karibu zaidi.Baada ya muda kadhaa kaka yangu alivyojua anapenda akaanza kujisikia.Siku nyingine alikuwa anazima simu siku hata ishirini,hapatikani.yule msichana akimuuliza,anasema.nipo kikazi huku porini,hakuna network.Msichana wa watu alivumilia,ila mimi kwa sababu nilimpenda sana wifi yangu yule kutokana na ustaarabu wake,niliona anamfaa kaka yangu,hivyo nikawa nawasiliana nae,ili asimpoteze.Kaka yangu aliendelea na tabia hiyo.huku mimi nikimlinda yule msichana asichoke na kukimbia.
Cha kushangaza,siku moja,alikuwa anampigia simu,akamwambia nipo kigoma baby,natafuta maisha ntarudi tu.Baada ya siku kadhaa walikutana macho kwa macho katika restaurant flan,ambayo msichana huyo alikuwa na rafiki zake,na kaka yangu akiwa na videmu vitatu wakila na kunywa.Wifi yangu aliumia,alinitumia msg ambayo sitasahau,wifi nashukuru kwa kunificha.Tangu siku hiyo hakupatikana tena.Tunasikia tu yupo sehemu fulani anafanya kazi.Kaka yangu ameishia kuliwa hela tu na wanawake wale na kutuma vocha tu,mpaka sasa hivi navyoongea hana msichana wa kusema wakuoa,kila mmoja ashamuona mbaya,anatamani kwenda kumrudia yule binti ila anaona aibu,jinsi alivyomfanyia.Wakaka pia wadada mkipendwa pendeni pia.anachoniomba hapa,nimfuate yule binti nikaongee nae,najiuliza,ni vyema kweli kwenda,au nimuache tu,na tangu muda walipoachana nahisi kashapata mume mwingine,naombeni maoni yenu..
17yrz.