Nahitaji msaada wenu kimawazo.......

Nahitaji msaada wenu kimawazo.......

marida kwakweli huyo kaka yako muache iyo ndo hadhabu yake, hasiyejua thaman ya kupendwa ndo mwisho wao huo.
 
naona bora hilo swala uachane nalo tu-kama kakayako ana tabia ya mtindo huo,inamaana kila siku utakuwa unamwombea misamaha?
cha kufanya wewe mshauri kaka yako,atulie,mpe mifano hai,maana afanyayo anayajua,kuliko kumfata huyo binti tena,unaweza kumfata then mwisho wa siku kka yako akaharibu tena

ok.asante
 
Unahangaisha kichwa kwa ajili ya bro, acha ajihangaikie mwenyewe na wewe hangaika na yakwako, haya ukimpata huyo dada then ukawaunganisha siku akija kumtenda nani atabeba lawama? Dada mapenzi ni ya wawili tu ukiingia wewe wa tatu utakuwa ni uongo huo, kwanza nimeona una miaka 17, it means bado uko mwanafunzi yanini kufuatilia mapenzi ya kaka badala ya kufuatilia shule?lol

ushauri wangu nijaribu kutokuwa mtu wa kati katika mahusiano ya mtu yoyote utaishia kuumia wewe...mapenzi ni ya 2
 
mwanangu Marida,huyo kaka yako ana umri gani? Nyumbani vipi utoto wenu mlikuwa mnafungiwa ndani sana? nauliza hivi isije ikawa kaka yako ndo kwanza anaibukia mambo ya mjini kwa pupa.
La mwisho nakushauri kwa umri wako si rahisi kujua mwanamke gani anafaa kuolewa katika boma lenu,jaribu kujiweka pembeni,na hilo jibu la wifi yako umesema hutalisahau mi nasema lisahau tu,maana kwa mtindo huu wa kakako si ajabu kabla hujafikisha miaka 25 atakuwa amekutambulisha mawifi mia.
Bila shaka bado unasoma,kazania kitabu mwanangu,kakako asikupasue kichwa na uhuni wake.
ONYO KWA WANA MMU WOTE:
JIHADHARI NA UKIMWI,UNAUA!
 
Asanteni sana.jibu nimelipata.sitoenda kwa huyo dada.ataenda mwenyewe bro.wengi wapo against it.nawashukuruni nyote.
 
kwa jinsi nilivyokuelewa nahisi kuwa huyo kaka yako bado hajawa tayari kuoa, ila anamkumbuka yule binti kwa sababu kaka yako amechunwa sana na videmu ambavyo ni your age mates. ni kweli kuwa ni kaka yako lakini nakushauri kabla ya kuongea na huyo binti kwanza ni lazima umwambie kaka yako abadilike kwa tabia yake aliyonayo vinginevyo utakuja kubeba lawama kutoka kwa wifi yako
Jambo la pili mwambie kaka yako aende aongee na huyo binti wao wawili kwani wao ndio wanandoa wakae na wakubaliane wakishakubaliana wewe uwepo ili kuwasupport lakini nakushauri usiende kumwombea ndugu yako msamaha
 
nafkiri hacha kaka yako amtafute mwenyewe maana kabla ya hapo,wewe hujui walikutana wapi.kaa pembeni kabisa
 
sijui tukushauri nini kwa kweli.....

labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol
jamani The Boss,hapa unaongea na mtoto wa miaka 17,majibu makali we watunzie vingunge wa mmu.
 
mwanangu Marida,huyo kaka yako ana umri gani? Nyumbani vipi utoto wenu mlikuwa mnafungiwa ndani sana? nauliza hivi isije ikawa kaka yako ndo kwanza anaibukia mambo ya mjini kwa pupa.
La mwisho nakushauri kwa umri wako si rahisi kujua mwanamke gani anafaa kuolewa katika boma lenu,jaribu kujiweka pembeni,na hilo jibu la wifi yako umesema hutalisahau mi nasema lisahau tu,maana kwa mtindo huu wa kakako si ajabu kabla hujafikisha miaka 25 atakuwa amekutambulisha mawifi mia.
Bila shaka bado unasoma,kazania kitabu mwanangu,kakako asikupasue kichwa na uhuni wake.
ONYO KWA WANA MMU WOTE:
JIHADHARI NA UKIMWI,UNAUA!

Asante bishagazi,nasema ukweli ili hata mimi nijifunze pia.kweli namawifi wengi sana,but aliekuwa anapendwa zaidi ni huyo mdada.akawa anakwepwa ili asijue maovu yake.Ana miaka 29.lakini ana mambo ya kitoto mno.siyo watoto wa getini.niwa kawaida tu.na mahusiano kaanza zamani.hajaanza sasa hivi.
 
kwa jinsi nilivyokuelewa nahisi kuwa huyo kaka yako bado hajawa tayari kuoa, ila anamkumbuka yule binti kwa sababu kaka yako amechunwa sana na videmu ambavyo ni your age mates. ni kweli kuwa ni kaka yako lakini nakushauri kabla ya kuongea na huyo binti kwanza ni lazima umwambie kaka yako abadilike kwa tabia yake aliyonayo vinginevyo utakuja kubeba lawama kutoka kwa wifi yako
Jambo la pili mwambie kaka yako aende aongee na huyo binti wao wawili kwani wao ndio wanandoa wakae na wakubaliane wakishakubaliana wewe uwepo ili kuwasupport lakini nakushauri usiende kumwombea ndugu yako msamaha

asante sana.
 
Unahangaisha kichwa kwa ajili ya bro, acha ajihangaikie mwenyewe na wewe hangaika na yakwako, haya ukimpata huyo dada then ukawaunganisha siku akija kumtenda nani atabeba lawama? Dada mapenzi ni ya wawili tu ukiingia wewe wa tatu utakuwa ni uongo huo, kwanza nimeona una miaka 17, it means bado uko mwanafunzi yanini kufuatilia mapenzi ya kaka badala ya kufuatilia shule?lol

Nilipoamua kujiunga,nilikuwa naakili timamu.na najua bado mambo hayo ya ndoa,hayanihusu.ila huwezi jua background yetu.inawezekana mimi ndo ni mtoa msaada mkubwa kwake ili abadilike.ningeamua kuwaambia wazazi,marafiki,ila wangeshangaa kama mnavyoshangaa now,najua hayanihusu.ni msaada tu wa mawazo nahitaji.

Na siyo kwamba mtu ukiwa na umri mdogo,basi,husijue vitu visivyo kuhusu.inawezekana nikawa mshauri hata kwa watu wengine,zaidi ya umri wangu.kusoma kupo.pia unatakiwa kukuza upeo wako kimawazo kwa maswala kama haya.kwa sababu,ndipo napoelekea.
Asante.
 
ya ngoswe mwachie ngoswe.

Halafu ulijuaje kama huyo dada anamfaa kaka yako? Je ulijiuliza kama kaka yako anamfaa huyo dada?

La mwisho hiyo tabia acha ndo nyie mawifi mnaoingilia ndoa /mambo ya kaka zenu.(huu ni mtazamo tu, pole kama nimekukwaza)
 
Wala hujanikwaza badili tabia.aliniambia mwenyewe..najua hata wewe kama either ni mwanaume au mwanamke,kabla ya kuoa,una chaguo lako,uliloweka moyon mwako binafsi.So,ndo kama hivyo.

Kukwazika kupo,but because nahitaji ushauri,na accept everythin.
Asante pia.
 
sijui tukushauri nini kwa kweli.....

labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol

jibu lako tosha kabisa umempa. Msaada ulompa kipindi chote ambacho alikuwa akimpotezeaga huyo binti, ndo msaada tosha.
Achana nae bro wako, tafuta mume nawe uolewe.
 
Habari zenu wana jf,mi mgen humu ndani,nilikuwa naomba msaada wenu wa kimawazo kuhusu hili.
Kaka yangu alimpenda msichana mmoja.mara za mwanzo mwanzo msichana alikuwa hampendi,ikafika sehemu mpaka akaanza kumpenda taratibu kadri walivyozidi kuwa karibu zaidi.Baada ya muda kadhaa kaka yangu alivyojua anapenda akaanza kujisikia.Siku nyingine alikuwa anazima simu siku hata ishirini,hapatikani.yule msichana akimuuliza,anasema.nipo kikazi huku porini,hakuna network.Msichana wa watu alivumilia,ila mimi kwa sababu nilimpenda sana wifi yangu yule kutokana na ustaarabu wake,niliona anamfaa kaka yangu,hivyo nikawa nawasiliana nae,ili asimpoteze.Kaka yangu aliendelea na tabia hiyo.huku mimi nikimlinda yule msichana asichoke na kukimbia.
Cha kushangaza,siku moja,alikuwa anampigia simu,akamwambia nipo kigoma baby,natafuta maisha ntarudi tu.Baada ya siku kadhaa walikutana macho kwa macho katika restaurant flan,ambayo msichana huyo alikuwa na rafiki zake,na kaka yangu akiwa na videmu vitatu wakila na kunywa.Wifi yangu aliumia,alinitumia msg ambayo sitasahau,wifi nashukuru kwa kunificha.Tangu siku hiyo hakupatikana tena.Tunasikia tu yupo sehemu fulani anafanya kazi.Kaka yangu ameishia kuliwa hela tu na wanawake wale na kutuma vocha tu,mpaka sasa hivi navyoongea hana msichana wa kusema wakuoa,kila mmoja ashamuona mbaya,anatamani kwenda kumrudia yule binti ila anaona aibu,jinsi alivyomfanyia.Wakaka pia wadada mkipendwa pendeni pia.anachoniomba hapa,nimfuate yule binti nikaongee nae,najiuliza,ni vyema kweli kwenda,au nimuache tu,na tangu muda walipoachana nahisi kashapata mume mwingine,naombeni maoni yenu..

dah, nina hamu ya kitimoto...
 
Back
Top Bottom