Nahitaji msaada wenu kimawazo.......

Nahitaji msaada wenu kimawazo.......

marida

Senior Member
Joined
Oct 27, 2011
Posts
168
Reaction score
20
Habari zenu wana jf,mi mgen humu ndani,nilikuwa naomba msaada wenu wa kimawazo kuhusu hili.
Kaka yangu alimpenda msichana mmoja.mara za mwanzo mwanzo msichana alikuwa hampendi,ikafika sehemu mpaka akaanza kumpenda taratibu kadri walivyozidi kuwa karibu zaidi.Baada ya muda kadhaa kaka yangu alivyojua anapenda akaanza kujisikia.Siku nyingine alikuwa anazima simu siku hata ishirini,hapatikani.yule msichana akimuuliza,anasema.nipo kikazi huku porini,hakuna network.Msichana wa watu alivumilia,ila mimi kwa sababu nilimpenda sana wifi yangu yule kutokana na ustaarabu wake,niliona anamfaa kaka yangu,hivyo nikawa nawasiliana nae,ili asimpoteze.Kaka yangu aliendelea na tabia hiyo.huku mimi nikimlinda yule msichana asichoke na kukimbia.
Cha kushangaza,siku moja,alikuwa anampigia simu,akamwambia nipo kigoma baby,natafuta maisha ntarudi tu.Baada ya siku kadhaa walikutana macho kwa macho katika restaurant flan,ambayo msichana huyo alikuwa na rafiki zake,na kaka yangu akiwa na videmu vitatu wakila na kunywa.Wifi yangu aliumia,alinitumia msg ambayo sitasahau,wifi nashukuru kwa kunificha.Tangu siku hiyo hakupatikana tena.Tunasikia tu yupo sehemu fulani anafanya kazi.Kaka yangu ameishia kuliwa hela tu na wanawake wale na kutuma vocha tu,mpaka sasa hivi navyoongea hana msichana wa kusema wakuoa,kila mmoja ashamuona mbaya,anatamani kwenda kumrudia yule binti ila anaona aibu,jinsi alivyomfanyia.Wakaka pia wadada mkipendwa pendeni pia.anachoniomba hapa,nimfuate yule binti nikaongee nae,najiuliza,ni vyema kweli kwenda,au nimuache tu,na tangu muda walipoachana nahisi kashapata mume mwingine,naombeni maoni yenu..
 
sijui tukushauri nini kwa kweli.....

labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol
 
sijui tukushauri nini kwa kweli.....

labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol

Damu nzito kuliko maji...boss.na sijafikia muda wa kuolewa bado.nahitaji maoni tu.siwezi kumwacha,ntamsaidia tu.asante pia kwa mchango wako.
 
huyo binti alishaona wewe na kaka yako lenu moja unafikiri atakuamini tena.......ikitokea akakubali kurudiana nae akajafanya madudu ya kumwache huyo binti unafikiri utakuwa katika hali gani.........mwache kaka yako ashugulike kumtafuta huyo binti mwenyewe wakielewana/kutoelewana wewe hayakuhusu
 
Damu nzito kuliko maji...boss.na sijafikia muda wa kuolewa bado.nahitaji maoni tu.siwezi kumwacha,ntamsaidia tu.asante pia kwa mchango wako.

kwanza kamuombe samahani huyo dada....
 
huyo binti alishaona wewe na kaka yako lenu moja unafikiri atakuamini tena.......ikitokea akakubali kurudiana nae akajafanya madudu ya kumwache huyo binti unafikiri utakuwa katika hali gani.........mwache kaka yako ashugulike kumtafuta huyo binti mwenyewe wakielewana/kutoelewana wewe hayakuhusu

Asante black woman.
 
sijui tukushauri nini kwa kweli.....

labda tu na wewe tafuta mume uolewe....
kaka yako muache mwenyewe atajiju.......lol
mmmh,majibu yako wewe.yeye hajajizungumzia kama yeye,na wewe unamwambia atafute mume aolewe
 
mmmh,majibu yako wewe.yeye hajajizungumzia kama yeye,na wewe unamwambia atafute mume aolewe

akipata mume
hatakuwa bize na yasiyo muhusu....
atakuwa na yake yanamfanya awe bize
 
Acheni Kumpotezea Mtoto wa watu muda wake, yaani mnataka kumtumia wakati wa dhiki tu? kama anataka aandae mpango wa ndoa kisha aende kuomba msamaha kama akikubari aoe kabisa.
 
nia yk ni KUMUUA BINT WA WA2 KWA UKIMWI AU? mwache mtoto wa watu!
 
Acheni Kumpotezea Mtoto wa watu muda wake, yaani mnataka kumtumia wakati wa dhiki tu? kama anataka aandae mpango wa ndoa kisha aende kuomba msamaha kama akikubari aoe kabisa.

Ndo nia yake hiyo likwanda.
 
naona bora hilo swala uachane nalo tu-kama kakayako ana tabia ya mtindo huo,inamaana kila siku utakuwa unamwombea misamaha?
cha kufanya wewe mshauri kaka yako,atulie,mpe mifano hai,maana afanyayo anayajua,kuliko kumfata huyo binti tena,unaweza kumfata then mwisho wa siku kka yako akaharibu tena
 
ushauri wangu nijaribu kutokuwa mtu wa kati katika mahusiano ya mtu yoyote utaishia kuumia wewe...mapenzi ni ya 2
 
Back
Top Bottom