Nahitaji mtaalam wa kuku wa mayai

mama mhaya

Member
Joined
Mar 18, 2015
Posts
7
Reaction score
1
Habarini wapendwa,

Mimi ni mjasiliamali mpya kabisa na nataka kuanza na kuku wa kisasa wa mayai hivyo naomba mnisaidie yafuatayo,

Nataka kuanza na kuku 500(vifaranga) nahitaji mtaji kiasi gani mpaka watakapoanza kutaga? (Banda lipo)

Je kuna uwezekano wa mimi mwenyewe kutengeneza chakula chao?

Kwa hapa dar naweza kununua wapi vifaranga na wanapatikana kwa bei gani?

Nimepitia thread nyingi kwenye hili jukwaa kuhusu kuku na nikaoana tarifa mbalimbali ila naomba mnijibu nayo maswali yangu maana sijaona maelezo take popote



Cc muhinda
 
Last edited by a moderator:
Kuku wazuri waliochanjwa chanjo ya MAREKSI siku ya kuzaliwa si chini ya 2,500=kifaranga kimoja
kuku mmoja huwa anakula kg 0.125 kwa siku
kwa hiyo kuku 400 wanakula mfuko wa kg 50 kwa siku.
Kuku mmoja mpaka atage anakula kg 8
kwa hiyo hao kuku wako 500 watakula kg 4,000 sawa na mifuko 80 ya kg ya chakula mpaka watage
mambo mengune ni PM.
 
Asante dada NEEMA ngoja niku pm
 
Last edited by a moderator:
nikihitaji kuku wakubwa walioanza kutaga nawapata wapi kwa hapa dsm na bei ni kiasi gani?
 


neema...roho mbaya umejifunzia wapi?...mbona mie nakujua vizuri huna na wala hukuwahi kuwa na roho mbaya kiasi cha kutunyima elimu ya bureeeee watanzania wenzako...behu njoo uweke yote hayo uliyonayo huko pm...weka hapa tusome wote...unaficha desa utadhani mwisho wa siku utakuwa mshindi wa kwanza na kupigiwa makofi.

Mwaga nchele tule wote somoooo....
 

kuna .......link inaongelea zaidi kuku wa mayai itafute kwenye ujasirilimali
 
Mkuu unaonekana uko vyema sana kwenye ujasiriamali.
Hongera sana.
 

umemshauri vizuri ila umempa formula ya kuku wa nyama.
kuku wa mayai akifikia mda wa kutaga anatakiwa kula gram135=kg0.135.hapa atafikia akiwa na wiki angalau 21.
hivyo kifara kwa wiki ya kwanza
135grm-15grm=120grms. pia 21weeks-1week=20weeks, gawa (120grm/20week=6grm/week). .hivyo ongeza gram 6kila wiki

1) 1st week-15grm
2)2nd week-15+6=21grm
3)3rd week-21+6=27grm
4)27grm+6=grm33
5)33+6=39
6)45
7)51
8)57
9)63
10)69
11)75
12)81
13)87
14)93
15)99
16)105
17)111
18)117
19)123
20)129
21)21st week-gram129+6=135
(formula hii tumia hata kwa kuku wa nyama ambapo wao ili aliwe anatakiwa ale gram125, ongeza grm15.7 kila wiki)
 
mama mhaya;

Maelezo yangu yanamsaada kwako? pia walio dar wataongezea
 
Unaweza kunipigia kwenye namba 0767989713 kwa ushauri wa bure kabisa kwa sasa niko katika maandalizi ya bure kabisa kwa sasa niko kwenye maandalizi ya nane nane
 
Ahsanteni mlotoa ushauri kwenye thread hii, Je na wa kienyeji wanatakiwa kuongezewa lishe kiasi kile kile kama kuku wa mayai / nyama??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…