Habari wakuuu!!!!
Mimi niko kwenye ndoa kwa miaka minne sasa. Kwa bahati mbaya bado hatujajaaliwa kupata mtoto. Hapo ndipo ninapoomba msaada wenu waungwana ili nami niingie kwenye ulimwengu wa kulea wana wangu mwenyewe.
Nilienda kufanya vipimo mimi na mwenzangu, wote tukaonekana tuko safi, vipimo hivi tulifanya hospitali mbili tofauti. Kama hiyo haitoshi, tulionana na Gyno mmoja pale Regency akapendekeza mwenzangu afanyiwe DnC, akasafishwa na kupewa dawa.
Tukapewa mbinu kadhaa ili tujaaliwe mtoto, ila hatukupata matokeo yoyote. Nikaamua kwenda kwa wasabato na tukafanyiwa vipimo wote. Mimi nikaambiwa mbegu zangu zimepungua spidi na mwenzangu njia yake haivuti mbegu ndani kutokana na yeye kuonekana kuwa na cist( wanasema viuvimbe vidogodogo kwenye mirija yake ya uzazi). Na dalili ya tatizo hilo tukaambiwa ni kupata maumivu kwenye chuchu wakati wa hedhi na upande wa kulia na kushoto chini ya kitovu. Maumivu hayo ni ya kweli kwakuwa mwenzangu amekuwa akilalamika mara kwa mara. Tukapewa dawa za kutumia, imepita miezi miwili sasa bila matokeo chanya.
Katika utafiti wangu, nimesoma soma kwenye mtandao na kuona kuwa mate yanaua mbegu za kiume. Mimi huwa natumia sana mate kama kilainishi tunapokutana faragha na mwenzangu. Je, hii pia inaweza kuwa ni sababu ya kutofanikiwa.
Naomba mnisadie waungwana.