Nahitaji mtoto, naomba msaada nifanikiwe!!!!

Nunio

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
747
Reaction score
1,856
Habari wakuuu!!!!

Mimi niko kwenye ndoa kwa miaka minne sasa. Kwa bahati mbaya bado hatujajaaliwa kupata mtoto. Hapo ndipo ninapoomba msaada wenu waungwana ili nami niingie kwenye ulimwengu wa kulea wana wangu mwenyewe.

Nilienda kufanya vipimo mimi na mwenzangu, wote tukaonekana tuko safi, vipimo hivi tulifanya hospitali mbili tofauti. Kama hiyo haitoshi, tulionana na Gyno mmoja pale Regency akapendekeza mwenzangu afanyiwe DnC, akasafishwa na kupewa dawa.

Tukapewa mbinu kadhaa ili tujaaliwe mtoto, ila hatukupata matokeo yoyote. Nikaamua kwenda kwa wasabato na tukafanyiwa vipimo wote. Mimi nikaambiwa mbegu zangu zimepungua spidi na mwenzangu njia yake haivuti mbegu ndani kutokana na yeye kuonekana kuwa na cist( wanasema viuvimbe vidogodogo kwenye mirija yake ya uzazi). Na dalili ya tatizo hilo tukaambiwa ni kupata maumivu kwenye chuchu wakati wa hedhi na upande wa kulia na kushoto chini ya kitovu. Maumivu hayo ni ya kweli kwakuwa mwenzangu amekuwa akilalamika mara kwa mara. Tukapewa dawa za kutumia, imepita miezi miwili sasa bila matokeo chanya.

Katika utafiti wangu, nimesoma soma kwenye mtandao na kuona kuwa mate yanaua mbegu za kiume. Mimi huwa natumia sana mate kama kilainishi tunapokutana faragha na mwenzangu. Je, hii pia inaweza kuwa ni sababu ya kutofanikiwa.

Naomba mnisadie waungwana.
 
usiogope hilo ni suala la kawaida tu muombeni mungu atawasaidia
 
Yupo Kristo Yesu bado hamjachelewa kwake. Yy n doctor wa madoctor. Kifup yy anafanya njia pasipo njia.hamna jambo linalomshinda.
 
Just try another woman. Maybe u can get a child with another woman.
 
Pole sana !

Usijisikie vubaya bado una nafasi kubwa
ya kupata mtoto tena zaidi ujue wazi
mtoto anatoka kwa Mungu mwenyewe.

Kubwa kuliko yote ina maana hao wataalam
wametumia kila njia na hakupata kile mtakacho
Naamini kwakuwe jambo lako umeliweka
jamvini utapata mtoto.

Hakika Mungu ni Mwema kila iitwapo Leo.
 
Just try another woman. Maybe u can get a child with another woman.

Mkuu, ndoa yangu ni ya kikristo. Ni ndoa ya mke na mume mmoja mpaka kifo kitakapoamua.
 
Usikubali hata kifo kiwaahamue ila Mungu peke yake. Endelea kuomba washirikishe na watumishi wa Mungu.

Mkuu, ndoa yangu ni ya kikristo. Ni ndoa ya mke na mume mmoja mpaka kifo kitakapoamua.
 
Habari wakuuu!!!!

Mimi niko kwenye ndoa kwa miaka minne sasa. Kwa bahati mbaya bado hatujajaaliwa kupata mtoto. Hapo ndipo ninapoomba msaada wenu waungwana ili nami niingie kwenye ulimwengu wa kulea wana wangu mwenyewe.

Nilienda kufanya vipimo mimi na mwenzangu, wote tukaonekana tuko safi, vipimo hivi tulifanya hospitali mbili tofauti. Kama hiyo haitoshi, tulionana na Gyno mmoja pale Regency akapendekeza mwenzangu afanyiwe DnC, akasafishwa na kupewa dawa.

Tukapewa mbinu kadhaa ili tujaaliwe mtoto, ila hatukupata matokeo yoyote. Nikaamua kwenda kwa wasabato na tukafanyiwa vipimo wote. Mimi nikaambiwa mbegu zangu zimepungua spidi na mwenzangu njia yake haivuti mbegu ndani kutokana na yeye kuonekana kuwa na cist( wanasema viuvimbe vidogodogo kwenye mirija yake ya uzazi). Na dalili ya tatizo hilo tukaambiwa ni kupata maumivu kwenye chuchu wakati wa hedhi na upande wa kulia na kushoto chini ya kitovu. Maumivu hayo ni ya kweli kwakuwa mwenzangu amekuwa akilalamika mara kwa mara. Tukapewa dawa za kutumia, imepita miezi miwili sasa bila matokeo chanya.

Katika utafiti wangu, nimesoma soma kwenye mtandao na kuona kuwa mate yanaua mbegu za kiume. Mimi huwa natumia sana mate kama kilainishi tunapokutana faragha na mwenzangu. Je, hii pia inaweza kuwa ni sababu ya kutofanikiwa.

Naomba mnisadie waungwana.

Mkuu usikate tamaa....still unaweza kupata mtoto....Yesu kristo yupo kwa ajili yetu it is possible na inawezekana kabisa naamini.Pata pia anointing water au sticker pray with it and with faith it shall be done.
 
Mkuu Kennedy,

Nipo Lindi kwa sasa ila napatikana pia Dar mara kwa mara. Mi mgeni kwenye hii jamii forum ndo maana nimeshindwa kukujibu kupitia PM mpaka nifikishe angalau Post tano.
 
Mkuu usikate tamaa....still unaweza kupata mtoto....Yesu kristo yupo kwa ajili yetu it is possible na inawezekana kabisa naamini.Pata pia anointing water au sticker pray with it and with faith it shall be done.

Nashukuru mkuu, hizo sticker na hayo maji yanapatikana wapi?
 
walicheck pouch of Douglas if there is any fluid.......?......

cc: Dr watu8.........

Dr Preta......
 
Last edited by a moderator:
Asante Preta, nawezaje kupata huduma hiyo na hospitali gani ni nzuri zaidi kwa hilo.
 
Mkuu, ndoa yangu ni ya kikristo. Ni ndoa ya mke na mume mmoja mpaka kifo kitakapoamua.

Imani ngumu sana...na David alikuwa na wake wangapi...vipi kuhusu Solomon?!

nafahamu kuzaa nje kuna complications zake but acheni kuingiza dini hapo hilo ni suala la mila,desturi na taratibu za jamii fulani...siyo suala la kiimani...mila na taratibu za walioleta dini kwetu ni mke mmoja...

UKIACHA MWANA WA MTU(YESU) NANI MKUU KULIKO DAVID?? ...WAKE NA NYUMBA NDOGO(CONCUBINES) KIBAO..
 
jaribuni ivf,ingawa siyo 100%guarantee.nasikia hospitali dar ipo.na nairobi pia ipo.kuna shost wangu alijaribu na alipata twins.yeye alienda nairobi na mume wake
 
Usiwasikilize wanaokushauri usaliti ndoa yako. Ni PM nitakupa msaada mimi mwenyewe nilitafuts for good 6 yrs. But God is great now i have my own children not a child.
 
Kila siku tunaomba kwa Mungu lakini Mungu anatowa kwa amtakae yeye na humnyima amtakae yeye
Usiwache kumuomba huenda muda wa kukupa uko njiani lakini imani yako iko vipi?
Wakati mwengine Mungu anakupa mali au mtoto kukuangalia imani yako, yeye ndie anayejuwa mwanzo na mwisho wa maisha yetu sote
 
Back
Top Bottom