Nahitaji mume 33-40 age

mushijack

Member
Joined
Feb 19, 2011
Posts
8
Reaction score
4
Mimi ni msichana tayari 32yrs sijawahi kuolewa na sina mtoto. Ninahitaji mume Mkristo tayari kupima VVU pia awe amesoma angalau kidato cha sita, awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe. Mimi nina elimu ya Advance diploma na nimeajiriwa na kampuni fulani hapa Dar es salaam. Samahani najua wengi mtaniponda nakadhalika lakini mimi niko serious kabisa nimeshachoka maisha ya upweke na ubusy wa kazi kiasi kwamba hata muda wa kukutana na watu nakosa. Sitakasirika kwa wale watakaoniponda ila kwa wale walioko serious ni tumie message kwenye profile yangu then tutaendelea kuwasiliana. Naomba tafadhali uelewe niko serious sana kuhusu hili swala na siyo kwamba nina tabia mbaya au labda muhuni au mi mwenyewe sina mvuto hapana, nadhani kwa kadri tutakavyozidi kufahamiana utanifahamu na kunielewa vizuri. Niko nasubiri Private message (PM) kwa wale tu walioko serious karibuni.
 
Vp hapo kwenye umri hauwezi kushuka kidogo? Nahisi kama vile hii bahati inanihusu kabisa.
 
Karibu Jamvini Mushijack.. (Naona hii ndio post ya kwanza)
All the Best and am sure utapata Singles humu Jamvini ni wa Kumwaga...
 
Dada,
Nakutakia mafanikio.
Mimi si kati ya wale watakaokusema vibaya, maana unachagua njia njema ya kuishi kiuwenza na kufarijiana na mwenzi wako!
Bahati mbaya mimi nishabukiwa, lakini vinginevyo ningekutumia ujumbe ili tuingie kwenye biashara serious!

Seriously ninaamini utapata mtu mwaminifu hapa ndani!
Lakini ukipata utoe feedback, na kwa kuwa umejiunga kwa kuanzisha mada hiyo, huu usiwe mwisho wako wa kuja hapa, hata kama matarajio yako yatakuwa ndivyo sivyo!
Tunakupenda sana!
 
Samahani kwa kwenda ofu topik, hivi ulikumbuka kupitia kule sebuleni kwanza kabla ya kuingia humu chumbani?
Mkuu hii ndio inaonesha kweli yupo serious..., kuliko wale wote ambao wameshatoa mabandiko yao...
Sasa wewe endelea hapa kuuliza maswali wakati wenzako wameshatuma application
Ushauri wangu Konga hicho kibutton cha PM Opportunity Never Knocks Twice...
 
Mi npo, ntafte fasta..
Mana vigezo nnavyo
 

I can see...This is a serious business!
Naomba wadau tusiingize mizaha kwa suala kama hili!...hope u know worram say!
 

Yeye anataka mum-PM tu, hapa sijui kama atachangia tena
 
VoR we unahamasisha wenzako tu... mbona we hutumi?
 
Hii mambo ya kutafuta mpenzi humu ndani sasa kama ugonjwa wa kuambukiza. Au ni ishara kwamba kuna tatizo la watu kutongozana live inabidi kupitia humu? Lakini nakutakia heri mama
 
Nahisi kama nime-qualify. Ebu jidescribe angalau kidogo. Mimi napenda upande wa nyuma uwe umekamilika. Sijui kama ndivyo ulivyo?
 
kama tu huhitaji PM za kukuchangamsha na uko serious kweli, then kila la kheri mwanadada:rain:
 
Pauuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
VoR we unahamasisha wenzako tu... mbona we hutumi?

Unajuaje Lizzy...inawezekana tayari ameshaanza mawasiliano....🙂

Kila la heri mushijack, ukipata usiache kutupa feedback! Karibu sana Jamvini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…