Nahitaji mume mwema jamani

PesaNdogo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
1,994
Reaction score
1,291
Habari zenu, mimi nahitaji mwanaume mwema, mwenye heshima,asiyepiga ovyo na anayejua kupenda wa kunioa. Asilimia kubwa ya wanaume ninaowaona huku mtaani wameoa au wana msululu wa wanawake,sasa mwana jf kama unajijua una sifa hasa ya kuja kuwa mume mwema nijibu. Mimi Nina uhakika ntakuwa mke mwema🙂
 
Kwanza namna ulivyiweka hii inaonyesha iko tabu mbele ya safari. Wewe kama ni msomaji wa Biblia kasome Mwanzo sura ya 24:1-67. Ukisha ipitia naamini utaona wewe umesimamia wapi!
 
Nani kakwambia Mwanaume mwema anapatikana huku? Nenda kwa Viongozi wako wa Dini wakuongoze. Imani/Dini yangu inaniambia 'Mke/mme mwema atoka kwa Bwana' Mithali 19:14-15. Mtangulize Mungu kila jambo, usipende kutumia akili zako au watu ambao hawana hofu ya Mungu.
 
jaman mbona mnamsakama pesandogo, hawa dada wakitudanganya tunalalamika, wakituambia ukweli kama ivi oooo huyu anawalikini ........dada ningekua single ningekutafuta bahat mbaya au nzuri nipo na fiancée aisee, ngoja wadau wapite pande hizi mume tuu utapata dada!!! tena mwemaaaa!!!
 
Asante kwa mchango wenu, hata mimi nasali. Nimejjijua kwamba ni mke mwema kwa kutumia standard ya biblia
 
first umri usije ukawa bi.kizee teh teh .... na jina lako halisi
 
Duh,hizi post zingine sasa,hivi kweli mume mwema anapatikana JF?wacha habari zako bana, piga magoti chumbani kwako lia na mungu wako atakusikia.
 
Ka uko serious. Naomba uni-pm. Lakini uwe tayari kupima ngoma kabla ya yote.
 
Kwanza jina tu unajiita pesa ndogo afu eti utakuwa mke mwema.. Huna jipya kama mtaani kwenu hakuna wanaume imekula kwako na aliyekwambia mme anapatikana jf kakudanganya..
 
Heee! Jamen! Punguzeni ukali basi hata kidogo tu! Mmesahau kama hili ni jukwaa kwa maombi kama hayo!
Mi nahisi hii ni Golden chance kwa wale watafutao wachumba!
Kila la heri bi mdogo! Zingatia hakuna mji wa JF, w/me wa hapa ndio sisi sisi wa mitaani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…