Nahitaji mwanasaikolojia

Nahitaji mwanasaikolojia

Heshima kwenu!!!
kiukweli nipo siriaz si hitaji mzaha wa kupotezeana mda.
kwa wanasaikolojia wote mliopo humu jamii forum nawaombeni pindi mtapo kuwa free mnisaidie tatizo langu.
shida yangu kuu nisaidieni namna ya kumliwaza mtu aliejichukia na kuamua kujitenga hataki kukaa na watu. yaani ni mkali hata namna ya kumsogelea unashindwa.
ombi kuu mnipe mbinu za kumtoa katika hali yake taratibu maneno ya kumfariji vitu vya kumfanyia n.k ili atoke katika hali hiyo inaniuma sana ndugu yangu huyu kuamua kujichukia / kujitenga hata simu hapokei katu blacklist.

msaada wenu wanasaikolojia.[/Q

Wewe ndo mwenye shida kubwa sana fanya haraka uende kutibiwa
 
Zamani watu wa namna hiyo tulikuwa tunampa kipigo cha kutosha kumtoa ujinga huo. Kisha akitulia ndio mnamuhoji nn tatizo. Maana akati mwingine hasira hutoka kwa mtu KULIA machozi mengi.

Anyway, endelea kumtafuta mtaalamu,maana yupo ninayemjua,lakini ninahofu anaweza kukuongezea matatizo badala ya kuyatatua yaliyopo.
 
Huyo ndugu yako ana msongo wa mawazo au stress mnaita, kwahiyo ili kuweza kumsaidia mtu wa namna hiyo inatakiwa kwanza yeye mwenyewe awe tayari kusaidiwa. Mimi sina utaalam wa aina yyt ule katika taaluma ya mambo kama haya, ila si vibaya nikashare ninachokijua pengine kinaweza msaidia ,Kuna njia kadhaa unaweza fanya ili kumsaidia....ila kabla sijazitaja kwanza ningependa nijue wewe ni nani kwake? Nature ya kazi anayofanya ni ipi? Wazazi wake huyo mtu wapo hai? Je umefanya jitihada za kumshirikisha muajiri wake? Baada ya kusema hayo naomba pia niseme huyo nduguyo ana shida ya msongo wa mawazo kubwa, na usipochukua hatua inaweza muathiri sana kiafya hata kijamii. Akishakubali kuongea na kuaddress kinachomkabili (ingawa mara nyingi huwa ni ngumu kukubali) basi anaweza akakutana na mtaalamu wa saikologia (ikibidi mtafute na aje hapo nyumbani incase ataendelea kuwa mkali) aongee nae , ajaribu kufanya meditation au yoga atlease lisaa kila siku. Ikishindikana basi atumie anti-depressant medications ili zimfanye arelax. Wacha niishie hapo....mengine watakuja ongezea wengine
 
Du! poleni sana. Ni hatari sana. Pia ni tatizo maana anaweza hata kupoteza maisha.
Au labda ameenda "kupima" majibu sio mazuri.
Mshana Jr hebu saidia hapa aisee kwa ushauri sio uganga wako ule
 
Kwanza poleni, pia kwa ushauri ni kwamba kwa msaada haraka na uhakika inahitajika huyo psychologist kuyafahamu vilivyo mazingira ya huyo mtu, chanzo cha tatizo, ukaribu wenu na wapi pa kuanzia yaani panahitajika information nyingi, na kufuatilia maendeleo kila siku kitu ambacho kwa mtu aliyembali au busy ni ngumu kufanya ipasavyo.
Hivyo basi ukikosa mwanasaikolojia (maana ni adimu), tafuta hata daktari hospital ambaye atakuwa tayari ku'deal na huyo mtu nje ya ratiba za kazi, ukimpata mtaalamu wa afya ya akili itapendeza zaidi hata kama ni nesi atafaa.
Ukikosa kabisa mtu wa kuwasaidia na hali ikiwa haina unafuu basi tuwasiline japo si psychologist by profession, ila taaluma inaruhusu, ile kumfuatilia kwa ukaribu napo naweza nisiwe na hiyo nafasi.
 
upendo utauoneshaje wakati ni mkali hasogeleki? ndo maana nalia na wanasaikolojia wanisaidie teknic za kufanikiwa kumuingia nijue tatizo.
Huyo jamaa yako Hana rafiki?ongea na rafiki yake wa karibu amliwaze atamueleza shida yake Kisha asaidiwe.lakini kwa kawaida ya wanna wake wlio wengi akijua tatizo la mume au jamaaa yake badala ya kumsaidia atamsimanga Hadi ajute kumweleza
 
Kwanza poleni, pia kwa ushauri ni kwamba kwa msaada haraka na uhakika inahitajika huyo psychologist kuyafahamu vilivyo mazingira ya huyo mtu, chanzo cha tatizo, ukaribu wenu na wapi pa kuanzia yaani panahitajika information nyingi, na kufuatilia maendeleo kila siku kitu ambacho kwa mtu aliyembali au busy ni ngumu kufanya ipasavyo.
Hivyo basi ukikosa mwanasaikolojia (maana ni adimu), tafuta hata daktari hospital ambaye atakuwa tayari ku'deal na huyo mtu nje ya ratiba za kazi, ukimpata mtaalamu wa afya ya akili itapendeza zaidi hata kama ni nesi atafaa.
Ukikosa kabisa mtu wa kuwasaidia na hali ikiwa haina unafuu basi tuwasiline japo si psychologist by profession, ila taaluma inaruhusu, ile kumfuatilia kwa ukaribu napo naweza nisiwe na hiyo nafasi.
asante mkuu nimemta boss wake wa zaman ajaribu kuongea nae jumapil hii
 
Huyo jamaa yako Hana rafiki?ongea na rafiki yake wa karibu amliwaze atamueleza shida yake Kisha asaidiwe.lakini kwa kawaida ya wanna wake wlio wengi akijua tatizo la mume au jamaaa yake badala ya kumsaidia atamsimanga Hadi ajute kumweleza
naomba usome reply za juu utaeleewa
 
Kaachwa na demu wake na demu kapata mshefa wanakula Bata,inauma sana ktendo hicho ukizingatia waliweka malengo uchwara ya kuoana. Hizo ni stress na ukimchelewea utamkosa Kwan Mim mwenyew yalinikuta yaan unakua m Kali Kama simba alaf hutaki kua na watu unapenda uende sehem hata mjusi asipite na hautak kelele ya Aina yoyote, apo anasema Akifa adhabu atapewa uyo Demu,na Kwa mazingira hayo kifo anaona Kama kunywa maji tyuuu, Mara nying visa vya mapenz vinapekea matokeo ya hatarihatari. Anza kumuombea
 
Back
Top Bottom