Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Hongera, kwahiyo mwekezaji akitoa Milioni 50 anapata share kiasi gani ya biashara yako, au kama ni hiyo milioni 5 kila mwezi ni mpaka lini?
 
Nenda bank Kama wazo lako ni zuri am sure watakupatia hela. Ila ukiona wamekataa ujue wazo lako ni mfu kabisa. Yaani cheki hao jamaa Wana hela zimejaa Ila hawazitoi ovyo ovyo Sasa masikini na kamilioni kake 200 anawaza namna ya kukatoa bila uhakika wa kurudishwa.
Yaani Kama unayo business idea.nzuri nenda bank huko ndiko watu wanaweka hela wasiojua kuzitumia
 
sawa sasa naanza na swali la kwanza

1. mashindano na mitandao ya simu
( kama nilivoeleza hapo juu hii ni hotspot business inamaana ni huduma inayotolewa ktk eneo maalumu mfano mimi hii huduma huwa naitoa mitaani na masokoni ambapo kuna watu shuguli zao za kila siku huwa hapo na internet katika hilo eneo mimi hutoa kwa masaa 24 per voucher ya 1,000 hivo mteja akijiunga mfano saa 11 jioni hadi kesho saa 11 jioni ndio inaisha na kwakuwa mteja voucher yake inampa access ya kupata unlimited internet kwa muda wa masaa 24 hivo kwake ni affordable ukilinganisha na kununua voucher ya 1000 ya mtandao wa simu ambao watakupa mb500
 
wazo lako zuri na nimelipokea ila system ya banks hapa bongo sio rafiki sanaa hiyo inawezekana tu kwa wafanyabiashara ambao ni wakubwa na wenye jina kwa sisi tutalazimika kuwa na colateral kitu ambacho kwa mtu anaeanza au mfanyabiashara mdogo ni ngumu kuna leval tukifikia tutaenda huko
 
Swadakta!

Maelezo yake yameegemea upande wa Faida tu, sijaona ameelezea Changamoto mahala popote. Site Ishirini sijaona mahali ameainisha gharama za nguvu kazi ya kuzisimamia, hajaeleza kupanda ama kushuka Kwa idadi ya Wateja, usalama wa hivyo vifaa, Changamoto ya Umeme ikijitokeza, way forward..

The deal is too Good to be true..
 
NITAKUPATA WAPI SASA ILI NIKUPE HIYO MILIONI 50 ILI KILA MWEZI NIPATE MILIONI TANO?MAANA HAPA MFUKO WANGU UNASOMA BILIONI KUMI NA MBILI NA SIONI PA KUZIPELEKA.
 
Swadakta!

Maelezo yake yameegemea upande wa Faida tu, sijaona ameelezea Changamoto mahala popote.

The deal is too Good to be true..
ndio mkuu kwa uzoefu wangu changamoto kubwa ya biashara hii kama hutoi internet nzuri wateja watakukimbia changamoto nyingine kubwa niliowahi ku experience ni ile lockdown na serikali kuzima mitandao ilipelekea Kushindwa kutoa huduma nje ya hapo hakuna changamoto kubwa labda za maintanance ambazo huzi solve haraka zikijitokeza
 
NITAKUPATA WAPI SASA ILI NIKUPE HIYO MILIONI 50 ILI KILA MWEZI NIPATE MILIONI TANO?MAANA HAPA MFUKO WANGU UNASOMA BILIONI KUMI NA MBILI NA SIONI PA KUZIPELEKA.
sawa tajiri napatikana Dar es salaam mawasiliano yangu 0710020066 ukiweza tunaweza kuwasiliana na kila kitu kikaanzia hapo
 
Hongera, kwahiyo mwekezaji akitoa Milioni 50 anapata share kiasi gani ya biashara yako, au kama ni hiyo milioni 5 kila mwezi ni mpaka lini?
lengo namba moja ni muwekezaje kurudisha mtaji ya pili ni makubaliano kati yake katika kutengeneza faida kati ya 50/50 au 60/40
 
umepanga mengi ni bora ufanye wewe
 
umepanga mengi ni bora ufanye wewe
mimi tayari nafanya na kuna sehemu nimefikia ila kila biashara ina ndoto kubwa ya kukuwa kubwa zaidi changamoto ni mitaji ila kuna watu wana mitaji changamoto ni sehemu ya uwekezaji kwaio tunajaribu kubadilishana tulichojaaliwa ili kufanikisha zaidi ni ngumu dunia ya sasa kufanya kila kitu mwenyewe hata kama ni kizuri zaidi
 
ROI ya miezi 6 kwa hotspot ni ndoto sana mkuu tofauti na unavyofikiria.

Unapotaka milioni 50 zirudi ndani ya miezi 6 bila collateral, hiyo siyo biashara, ni props au seeking validations tu.

Hayo makadirio yako ni ya darasani siyo ya mtaani.

Hiyo faida unayokadiria kwa siku kwa kila site bila kuhesabu:

Downtime,
Ushindani,
Wizi wa password,
TTCL kukata line,
Vijana kugawana pasword for free,
Kodi ya eneo,
Umeme,
Maintenance fee,
Uharibifu au upotevu wa vifaa,
Mlipo ya Wasimamizi,
Marketing,
Serikali (Leseni/Kodi),

Wewe umehesabu gharama za bando la internet tu.
Hilo ni kosa linalofanywa na wasomi wengi kabla hawajafeli vibaya.

Hauja include hata:
Bussiness Statement,
Cashflow halisi,
Site zilizopo ziko wapi ili twende,
Hujaweka revenue proof,
Sijaona Contract za hao wawekezaji wengine.
Hivi unfahamu maana ya uwekezaji kweli wewe?

Kwanza hapo mimi kama muwekezaji sina kinga kwasababu sijaona asset inayohamishwa kwa muwekezaji, Hakuna Equity structure, Hakuna Exit plan yaani hata Legal framework tu hakuna.

Halafu unasema tutaziona tu kwenye system.
System gani?
Nani anaicontroll hiyo system?

Mtu mwenye biashara inayozalisha 10M net kwa mwezi hahitaji kuomba muwekezaji kwenye forums kama Jf.
Ni simple, Anaenda benki au kwa private investors bila kuhitaji post ndefu ya kuelimisha watu Wi-Fi ni nini.

Wasomi bhana 😂
Ibn Unuq.
 
Justification ya kuanzisha at least 20 sites ni nini?
 
Biashara yako haina RISKS?
Hujajadili potential risks kwenye biashara hii.

Ushauri: Wenda una wazo zuri lakini unashindwa kuliwasilisha vyema, au hujajua unahitaji nini. Mwekezaji/Investor sio Mhisani/Donor/Funder. Ukimweleza mwekezaji makini, aweke 50M, kwa ROI ya miezi sita, ataona wazi unataka kumwibia. Mwekezaji analenga kupata usalama hasa wa pesa yake kabla ya faida. Yaani unapochukua pesa ya mwekezaji cha kwanza ni usalama na uhakika wa pesa yake, afu faida. Kwa lugha nyepesi, akikosa hiyo faida, pesa yake itakuwepo. Au ndio mtaanza kudaiana na kupeana majina yasiofaa.
Hujaeleza risks ya biashara yako, hujaeleza ni vipi pesa ya mwekezaji takuwa salama katika mikono yako. Umevutia tuu faida.

Do your homework, wawekezaji makini hawataki kusikia kuhusu faida, wanataka kusikia kuhusu usalama wa fedha zao zikiwa mikononi mwako "How safe is the money.
 

Hakuna benki inatoa mtaji wa mwanzo "Initial capital" benki inatoa endelezo la mtaji "Working Capital".

Akienda benki, watamwambia biashara iwe na miaka mitatu, iwe na leseni, awe na akaunti ya biashara, awe na mizania ya hesabu za biashara "Financial statements".

Mwisho watamwambia awe na dhamana sizizo hamishika.
 
mkuu naomba nikukanushe kidogo hii biashara mimi naifanya kwa muda wa miaka 2 sasa kila nilichoandika sio fikra ni uhalisia na nakuruhusu kuja kuuushuhudia ngoja nikujibu swali moja baada ya lingine

ukiifahamu vizuri hotspot business haisumbui hata kidogo tofauti na wengi wanavyodhani

1. kwanza kabisa aina ya hotspot business nayo ifanya tofauti unayoijua wewe ya kuunga mtu kwa kutumia password hiyo kitu ni ya zamani sanaaa kwa sasa kuna mifumo inafahamika kama hotspot billing system ukipata nafasi google mkuu upate elimu zaidi

2 ushindani biashara hii kwa Tanzania badooo sanaaaa wanaofanya ni wachache mno na wengi wao wanaofanya niwale wenye CPE yake mfano kanunua ya airtel ndio anafanya ila mimi nafanya ina a large scale naweza ku deploy system hadi ya urefu wa kilometer moja moja na hii inanifanya niwe tofauti na zingine

3.TTCL kukata line kwanza kabisa bahati nzuri mimi main hustle yangu nauza unlimited internet kama partner wa mtandao moja wapo wa simu hapa nchini hivo internet providers ni wengi sanaaa na kuna kitu nimeandika hapo juu kinaitwa GATEWAY ukipata nafasi kaisome ujue inafanya nini

4. KODI ya eneo nafikiri picha ulionayo ya hotspot inavofanyika na uhalisia hauko hivo kabisa mfano mimi nimefunga hotspot maeneo mengi na hiyo code haipo mana kinachofungwa ni acccess point sasa nenda kaangalie access point ilivyo kisha niambie kodi stahiki ya kulipia it is imposible mkuu na sitoi kichwani ninafanya tayari hii biashara

5. kulipa wa simamizi hii sasa ukitaka kuielewa zaidi nakukaribisha site kwakuwa hapa ningumu kuweka kila kitu ila kifupi kuna agent ambao mimi nawauzia kila mmoja 10 vouchers kwa 5,000 then wao wanauza kwa 1,000 kisha wanapata 10,000 yao hivo faida 5000 ambayo wanajilipia umeme wenyewe easy sana mkuuu tofauti unavyofikilia

6. Uharibufu upotevu maintainance hii nimejibu na nakujibu tena kuwa hii biashara tofuti na unachofikiria nimefanya biashara hii na sitezote maintainace nafanya mwenyewe why ? kwakuwa na mudu hivo vyote mwenyewe bila ya kuongeza mtu nimekuweka na database inayoniwezesha kufuatilia wateja wangu

7. Revenue proof mkuu utaweka kila mahali kama nyanya si ndio mana muwekezaji anaruhusiwa kutembelea site na kujionea tatizo ni moja umekuja kwa negative energy tutulie tujifunze kwa pamoja

hili ni tatizo la confidance ikichanganyikana na ujinga Ungekuwa unafanya hii biashara ungeielewa zaidi ila kifupi kama ni muwekezaji nakukaribisha site
 

Attachments

  • Screenshot 2025-12-21 184413.png
    701.6 KB · Views: 47
  • Screenshot 2025-12-21 184506.png
    187.5 KB · Views: 46
  • Screenshot 2025-12-17 205252.png
    47.1 KB · Views: 51
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…