Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Natumaini ni wazima wa Afya na heri ya mapumziko ya mwisho wa mwaka

Najua mwaka huu ulikuwa na changamoto nyingi na baadhi yetu tulikuwa na malengo mengi naimani kwa uwezo wake M/Mungu mwaka ujao tutakamilisha au kuanzisha ndoto tulizoacha

Nisiwachoshe sana kwa salamu ni kama kichwa kinavyojieleza hapo ya kuwa nahitaji muwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika hotspot business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6 na ataendelea kupata gawio la milioni 5 kila mwezi

Kwanini naandika hili ni kwakuwa naimani sisi katika kujaaliwa ridhki tumetofautiana naimani kuna mtu ana kiasi fulani cha fedha na hajua wapi pa kuwekeza au hana mtu sahihi wa kumshauri kuwekeza, lakini pia kuna akina sisi tuna mawazo mbali mbali ya kibiashara lakini hatuna mitaji ya kuwekeza

Hivo basi lengo la uzi huu ni kumfikia yule mwenye mtaji ila hajui wapi pa kuwekeza ili tuweze kushirikiana na kulisongesha gurudumu la mafanikio kwa pamoja.

Turudi kwenye mada Husika ni kuwa nahitaji muwekezaji wa kiasi kisichopungua 50 millioni kwaajili ya biashara ya HOTSPOT BUSINESS

Nini maana ya HOTSPOT ?
Hotspot
Ni sehemu ambayo inakupa muunganisho wa internet kwa kutumia WI-FI bila kutumia nyaya

Nini maana ya WI-FI ?
Kwanza kabisa tufahamu kirefu cha neno WI-FI (Wireless Fidelity)

Wireless Fidelity ni teknolojia inayotumika kuunganisha vifaa kwenye mtandao wa internet bila nyaya

sasa kwakuwa tumeshafahamu maana ya hotspot na maana ya wi-fi sasa turudi kwenye mada ili twende sawa

Nini maana ya HOTSPOT BUSINESS ?
Hotspot Business ni biashara ya kuuza Huduma ya internet kwa njia ya WI-FI katika eneo fulani kwa malipo au makubaliano maalumu, sehemu hizo ni kama mtaani,sokoni,vyuoni na eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu

kwa maelezo ya ziada biashara ya hotspot hufanyika katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu eidha ni wakaazi wa eneo husika au mahala pa biashara ambao watu hukutana na kushinda muda mrefu eneo hilo kwa siku zote mfano stand,sokoni,mtaani

unaweza pitia uzi wenye kichwa cha habari hichi kuongeza ujuzi zaidi Tengeneza hadi 50,000/= kwa siku kwa kufanya biashara ya kuuza internet kupitia WiFi kwenye maeneo yenye mkusanyiko

sasa basi kwakuwa tumeshafahamu nini kusudio la huu uzi sasa tuangalie huo mchananuo wa uwekezaji unao hitajika kiujumla mpaka ukafikia thamani hiyo tajwa hapo juu

ili kufanikisha biashara ya hotspot kuna vitendea kazi uhitajika kwaajili ya kukamilisha biashara hii ya Hotspot
1. Internet ( Hutolewa na kampuni za mawasiliano kama TTCL,HALOTEL,TIGO n.k )
2. Router ( Huuzwa madukani au hutolewa na kampuni za mawasilaino ukinunua huduma zao )
3. Gateway ( Huuzwa madukani )
4. Access Point ( Huuzwa madukani )

sasa basi ukiwa na vifaa tajwa hapo juu tayari unakuwa na vitendea kazi maalumu kwaajili ya biashara ya Hotspot sasa naomba nikupe hesabu kwanini inahitajika 50 milioni

Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache tuliopata fursa ya kuutambua uwekezaji huu adimu hapa nchini na wenye faida ya uhakika na kwabahati nzuri tunafanya na kunufaika hadi sasa na lengo la kutafuta uwekezaji ni kuona namna gani tunaweza kufikia masoko zaidi ili kutengeneza faida zaidi

ili upate faida kubwa katika biashara ya hotspot yakupasa kufanya uwekezaji mkubwa

MFANO makadirio ya faida inayoweza kupatikana katika biashara ya hotspot kwa uwekezaji wa kiasi cha milioni 50 na hii sio makadirio ya kichwani ni kutokana na uzoefu na muundo wa biashara hii ambayo tayari nimeifanya kwa makadirio ya miaka miwili sasa


tumeona hapo juu mahitaji halisi ili kufanikisha biasharA hii ya hotspot ambayo ni
internet ,Router ,Gateway ,Access point sasa hii hotspot huwa tunafunga kwa site sasa ngoja tuone site moja inahitaji mtaji wa kiasi gani

MTAJI KWA SITE MOJA YA HOTSPOT
Vitendea kazi vinavyohitajika
internet
nanunua kwa 200,000/= malipo ya kila mwezi
Router nanunua kwa 250,000/= malipo ya mara moja
Gateway nanunua kwa 150,000/= malipo ya maramoja
Access point nanunua 1 kwa 350,000/= hivo kwa site moja uhitajika 5 ambazo ni sawa na 1,750,000/=
Extra accessories
(erthenet,RJs,climper,cable tie ) nanunua 150,000/=
kwa mchanganuo huu tunapata jumla ya Tsh 2,500,000/= za uwekezaji katika site moja
hivo basi tukirejea kwa dhumuni letu la kupata muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50 milioni tunakusudia kupata mtaji wa kuweza kuanzisha sites 20
sasa hela inapatikana vipi kwa site moja ?

kwa namna mimi ninavofanya kwa site moja naweza kukusanya 40,000 kimo cha chini kwa siku 30,000

sasa kwakuwa tunahitaji muwekezaji wa kutupa mtaji wa 50,000,000 ambao ni sawa na site 20 tunaweka makadirio kila siku kwa site moja ikusanye kiasi cha 25,000 tu hii inamaanisha kwa site zote 20 tutakusanya 500,000 kwa siku

yaani kimahesabu 20 x 25,000 = 500,000 kwa siku
tukichukua makusanyo ya siku kwa mwezi ni sawa na
500,000 x 30 = 15,000,000/= Makusanyo kwa mwezi
tukitoa matumizi ya lazima ya kila mwezi kama nilivoainisha hapo juu ni malipo ya internet kwa mwezi
ambapo kwa site moja tumeona ni 200,000 kwa mwezi hivo kwa site 20 itakuwa
200,000 x 20 = 4,000,000 hii ndio gharama ya mwezi

kwakuwa tumeona kuwa kila mwezi tunahitajika matumizi ya internet basi tutachukua makusanyo ya jumla na kutoa matumizi ya lazima
15,000,000 makusanyo ya jumla mwezi mzima
4,000,000 malipo ya internet kwa mwezi mzima

15,000,000 - 4,000,000 = 11,000,000 kiasi kinachobaki

sasa kwanini tulisema kuwa muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50,000,000 ataweza kurudisha mtaji wake kwa muda wa miezi sita na kuendelea kula faida kila mwezi isiopungua ya 5,000,000 ni kwa hesabu hii

kwakuwa tumeona kiasi ambacho kitaweza kubakia kwa mwezi ni 11,000,000 au 10,000,000 basi tutachukua hichi kiasi na kuzidisha mara 6 muda ambao tumeweka maximum muwekezaji kurudisha mtaji wake

kwaio
10,000,000 x 6 = 60,000,000/= au tunaweza weka makadirio ya 50,000,000/=

Hapo tutakuwa tumefanikisha kurudisha kiasi cha mtaji wa muwekezaji kilichobaki ni muendelezo wa safari ya kufurahia matunda ya uwekezaji wake ambao sisi tumeona iwe nusu ya faida itakayopatikana kwa kuthamini mchango wa muwekezaji kwa kuweka mtaji na sisi kuweka ujuzi wetu katika fursa hii

ambapo kama kwa mwezi makusanyo baada ya kutoa kila kitu kubakia 10,000,000 basi nusu itakuwa ya muwekezaji na nusu itskuewa ya kwetu sisi

JE NIKIWA KAMA MUWEKEZAJI NA UHAKIKA GANI WA KUREJESHA MTAJI WA PESA YANGU ?
Ukiwa na swali kama hili mimi nitakujibu hivi
inawezekana kurejesha hicho kiasi kwa muda kusidio kwakuwa hii ni biashara ya kisasa japo ngeni kwa macho ya wengi ila mimi nina uzoefu nayo kwa muda wamiaka miwili sasa na bado ninaifanya mpaka sasa hivo kumbukumbu za makusanyo yote katika site zangu yapo na tunamfumo wa kisasa kusimamia biashara hii mahali popote Tanzania hivo muwekezaji anauwezo wa kuona na kutambua kila kinachoendelea katika mfumo mahali popote alipo

lakini pia tunatoa fursa ya kutembelea mradi ulipo ambapo tunapatikana Dar es salaam na baadhi ya mikoa tumefunga hivo unaweza kujionea jinsi tunavyoendesha biashara hii na namna faida inavyoweza kuaptikana

Kwa wale wenye ndugu jamaa na marafiki ambao unaimani wanamitaji ila hawaoni pa kuwekeza tunawakaribisha muweze kuuliza maswali na tutajibu kila moja na kwa yule anaehitaji kuwekeza basi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0710020066
Mr. Motivation speaker, sir, Kwa kuwa una biashara inayofanya vizuri, nenda benki ukachote mihela hiyo.

Wanaweza kukupa hata 2bn, mara paaap unaingia kwenye Forbes list ya mabilionea kama Mo.
 
mkuu naomba nikukanushe kidogo hii biashara mimi naifanya kwa muda wa miaka 2 sasa kila nilichoandika sio fikra ni uhalisia na nakuruhusu kuja kuuushuhudia ngoja nikujibu swali moja baada ya lingine

ukiifahamu vizuri hotspot business haisumbui hata kidogo tofauti na wengi wanavyodhani

1. kwanza kabisa aina ya hotspot business nayo ifanya tofauti unayoijua wewe ya kuunga mtu kwa kutumia password hiyo kitu ni ya zamani sanaaa kwa sasa kuna mifumo inafahamika kama hotspot billing system ukipata nafasi google mkuu upate elimu zaidi

2 ushindani biashara hii kwa Tanzania badooo sanaaaa wanaofanya ni wachache mno na wengi wao wanaofanya niwale wenye CPE yake mfano kanunua ya airtel ndio anafanya ila mimi nafanya ina a large scale naweza ku deploy system hadi ya urefu wa kilometer moja moja na hii inanifanya niwe tofauti na zingine

3.TTCL kukata line kwanza kabisa bahati nzuri mimi main hustle yangu nauza unlimited internet kama partner wa mtandao moja wapo wa simu hapa nchini hivo internet providers ni wengi sanaaa na kuna kitu nimeandika hapo juu kinaitwa GATEWAY ukipata nafasi kaisome ujue inafanya nini

4. KODI ya eneo nafikiri picha ulionayo ya hotspot inavofanyika na uhalisia hauko hivo kabisa mfano mimi nimefunga hotspot maeneo mengi na hiyo code haipo mana kinachofungwa ni acccess point sasa nenda kaangalie access point ilivyo kisha niambie kodi stahiki ya kulipia it is imposible mkuu na sitoi kichwani ninafanya tayari hii biashara

5. kulipa wa simamizi hii sasa ukitaka kuielewa zaidi nakukaribisha site kwakuwa hapa ningumu kuweka kila kitu ila kifupi kuna agent ambao mimi nawauzia kila mmoja 10 vouchers kwa 5,000 then wao wanauza kwa 1,000 kisha wanapata 10,000 yao hivo faida 5000 ambayo wanajilipia umeme wenyewe easy sana mkuuu tofauti unavyofikilia

6. Uharibufu upotevu maintainance hii nimejibu na nakujibu tena kuwa hii biashara tofuti na unachofikiria nimefanya biashara hii na sitezote maintainace nafanya mwenyewe why ? kwakuwa na mudu hivo vyote mwenyewe bila ya kuongeza mtu nimekuweka na database inayoniwezesha kufuatilia wateja wangu

7. Revenue proof mkuu utaweka kila mahali kama nyanya si ndio mana muwekezaji anaruhusiwa kutembelea site na kujionea tatizo ni moja umekuja kwa negative energy tutulie tujifunze kwa pamoja

hili ni tatizo la confidance ikichanganyikana na ujinga Ungekuwa unafanya hii biashara ungeielewa zaidi ila kifupi kama ni muwekezaji nakukaribisha site
Good explanation,
 
nimekuelewa chief lakini kuna kitu kimoja tunatakiwa kuelewa wote kwa pamoja hata mimi sikuwahi kuelewa mpaka nilipopata maarifa ambayo yalitokana na kufanya research mbalimbali na ku take risk acha nielezee kwa kifupi hotspot ilivyo najua kwa wengi ni kitu kigumu kwakuwa ni kigeni hasa nchini ila kwa kenya na uganda au bara la asia ndiko zimeenea zaidi

kila biashara huwacina risk ila sio kila biashara ina risk pia kwanini nasema hii kwenye Hotspot risk zake nyingi ni za kufikirika ila uhalisia hauko hivo hata kidogo nakupa mfano

ili ufanye biashara hii inahitaji vitu hivi

internet
Hii utaipata kwa mitandao ya simu hivo ikitokea changamoto let say network nitarudi kwao na wata itatua kwakuwa mimi sio ISP

gateway
hichi ni kifaa kinachowezesha kuongoza internet kutoka kwa ISP kwenda kwa watumiaji namaanisha wateja wangu na ninaweza kutumia ISP zaidi ya mmoja ili kuepuka changamoto ya internet kufeli kwakuwa ikifeli ya huyu natumia ya huyu

access point
hichi ni kifaa kinachochukua internet kutoka kwa Gateway na kusambaza internet kwenda umbali zadi ambao mimi nimeukusudia hapa

sasa pata picha hii wastani wa gateway ina life span ya miaka 10 na access point ina miaka 7 huu ndio msingi wa biashara yangu na cha mwisho ni internet ambayo naipata kwa mtoa huduma wa internet kama tigo vodacom ttcl na wengine

niambie risk yake ya kwanza ni ipi ? wengi watasema kuibiwa vifaa hii ni ngumu kwakuwa hivi vifaa siku zote hufungwa juu ya paa na pia ni ngumu mwizi kuiba kifaa asichokifahamu nina miaka miwili sijawahi kupoteza wala kuibiwa

Risk ya pili tunaweza kusema ubora wa internet ? Hii sijawahi experiance kwakuwa ikitokea maybe provider huyu ni ghali au network yake haipo stable mimi huama na kutumia provider mwingine

hizi ndio kesi unazoweza kukutana nazo kwenye hotspot zaidi ya hapo huwezi kutana na risk ingine mana huo mtaji tunaoukusudia ni vifaa tu ambavyo hizi ndio mali na msingi wa biashara hii na hii biashara kwa Tanzania naitabiria kuwa na soko kubwa kwa miaka 10 hadi 15 Ijayo refeer kwa majirani zetu ambao walianza zamani na bado inaendelea sisi kwetu tumechelewa


kiufupi mkuu nimepokea ushauri kwenye makosa tutarekebisha ila amini hichi ni kitu cha tofauti na kipya kwa wengi hivo nikisema ni risk free wengi wanaweza wasiamini ila kwa muekezaji ambae anahitaji kuwekeza namkaribisha kwanza ajifunze aone aangalie operation zilivyo akijiridhisha tunatafuta misingi ya kanuni na taratibu ambazo yeye ataona kuwa pesa zake zipo mikono salama

ASANTEH SANA KWA MAARIFA
Imetosha ,itoshe kusame unaijua hii business na unajua unachokifanya wajinga wachache wasiota
ka kuelewa wasikuyumbishe kwanza hawana hela always thinking risks na ni pessimistic
 
Nenda benki mbona ni chapu unaipata hii hela. Ukiona benki hawakupi hela zao ujue bado wazo lako halina ukomavu ama sio viable yaani halifanyi kazi mkuu. Acha kuwazia hela za watu kufanya kazi namie nilikuwa ninawazaga Kama wewe yaani kama una mawazo mazuri utapata hela Ila Kama huna utaishia kulia kuwa mtaji sina. Nenda kwa matajiri uwaulize mtaji walitoa wapi wao
 
mkuu kuna jamaa kaweka pale ardhi university yeye malipo anafanya automatically kwa mitandaonya simu kama mpesa tigo pesa halafu inajiconnect hapo hapo… vp kwako wewe huo mfumo unaufahamu pia na je mfumo wako Una backup incase internet provider akafeli may be na vipi kuhusu vibari vya tcra maana wanaweza kunyooka na wewe wakiona unapiga hela
 
Back
Top Bottom