NyegereBOY
JF-Expert Member
- Mar 24, 2021
- 302
- 520
- Thread starter
- #81
Hahahahahah Nusu yake ndugu muwekezaji ingependeza mana hatuendi kupata mateso tunaenda kupata hela mkuuuIdea nzuri sana. Sema 50 parefu. Ungeanza na robo yake.
Hahahahahah Nusu yake ndugu muwekezaji ingependeza mana hatuendi kupata mateso tunaenda kupata hela mkuuuIdea nzuri sana. Sema 50 parefu. Ungeanza na robo yake.
😁😅😅😅😅Hauna pesa bwashee acha kusumbua uma
Jitahidi tu u some mkuu Kuna kitu utapata na kuelewa zaidiHebu ni convince mimi hapa
Nisamehe sijaweza kusoma mpaka mwisho na pia maswali ya wadau nimejaribu kuyasoma machache.
Je umefungua sehemu ngapi mpaka sasa hata kwa mtaji mdogo?
Ila kama bado hujafungua hata moja? Mimi ntaaminije kuwekaeza 50m kwenye biashara mpya? Ambayo ndio itaanza kwa mtaji wangu?
Kama ishu ni mtaji unaweza kupata hata bank, tafauta mwekezaji anayekupa kitu zaidi ya fedha with exachange ya yeye kuw na share kwenye hiyo biashara.lengo namba moja ni muwekezaje kurudisha mtaji ya pili ni makubaliano kati yake katika kutengeneza faida kati ya 50/50 au 60/40
Shukran sana bossJitahidi tu u some mkuu Kuna kitu utapata na kuelewa zaidi
Ila kiufupi biashara tayari imeshafanyika na Ina muda karibia wa miaka 2 lakini kwa udogo lengo la kutafuta muwekezaji ni kujitanua zaidi na kufika masoko mengi
That's all I want a business partner ambae yeye atakuja na fedha ila ujuzi mahalifa biashara ataikuta ila bank sio rahisi hivo mkuuKama ishu ni mtaji unaweza kupata hata bank, tafauta mwekezaji anayekupa kitu zaidi ya fedha with exachange ya yeye kuw na share kwenye hiyo biashara.
Hivi hawawezi kukuzunguka kichukua wazo lako na wewe waka kukacha?Nenda bank Kama wazo lako ni zuri am sure watakupatia hela. Ila ukiona wamekataa ujue wazo lako ni mfu kabisa. Yaani cheki hao jamaa Wana hela zimejaa Ila hawazitoi ovyo ovyo Sasa masikini na kamilioni kake 200 anawaza namna ya kukatoa bila uhakika wa kurudishwa.
Yaani Kama unayo business idea.nzuri nenda bank huko ndiko watu wanaweka hela wasiojua kuzitumia
Mkuu Kwema huko!Mimi sifi kizembe bwashee😁😁
1. kuna kitu watu wengi huwa wanachanganya naomba nikueleweshe mkuu Starlink haji kufanya Hotspot business hata kidogo tena akija starlink kwa sisi tunaofanya Hotspot itakuwa neema zaidi kwakuwa tutaweza kuuza hadi vijijini naomba nikueleze hotspot kwa lugha rahisi kabisa najua unafahamu hili neno WINGA huyu ni mfanyabiashara mdogo amabae ananunua au kuchukua biashara kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa au wa kati na kuiwasilisha watumiaji sasa nakurudisha huku kwenye mada sasa unamuona AIRTEL,TIGO,VODACOM,STARLINK hawa tunawaita ISP ( Internet Service Providers ) hawa wanatoa huduma ya internet katika Wholesale na retail sale sasa Hotspot nayo ni huduma ya kutoa internet katika levo ya MACHINGA hivo uwepo wa ISPs wengi kwetu ni neema ya kupata internet kwa bei rahisi na sisi kuiuza kwa bei nzuri zaidi kwaio starlink na ISPs wengine sio tishio la hotspot fuatilia hata bei za receiver za STARLINK still bado sio internet nafuu kama wengi mnavyodhani ila kwasisi HOTSPOT enterprenuers tunafurahia uwepo waoBInafsi nimekuelewa vzr sana mkuu,ila nilikuwa naomba kuuliza pia...
1:Umesema soko kwa sasa ni pana sana,ni kweli,sasa je hivi karibuni ikitokea yamekuja ma big fish kma Starlink Tanzania,jamaa naskia wanagawa utamu kwa bei rahisi sana,sasa huku kuna mtu kawekeza mil50 mtaani kwa site 20...je unadhani huyu muwekezaji atakuwa salama kuendelea na hii biashara?
2:Huu usamabazaji wa kasi wa routers kutoka kwa makampuni ya simu haiwezi kukuumiza hapo mbele?
3:Mimi binafsi nina damu ya risk taker ila kwa siku hizi nimekua muoga muoga sana maana naona mambo yanaenda kasi mnoo,yan mambo yana change kila baada ya wiki so Nikiwa na kma mil5 siwezi kuanza hii biashara huku naskilizia?
5::Hii biashara ni lazima mtu aisomee japo kidogo au mtu anaweza akapata maarifa ndaji ya kazi?
6:Kwa sisi ambao vimitaji unga unga mwana,mtu akikutafuta kisha akakupatia laki 5 ili umpige training kama ya wiki khs hii biashara kisha huyu mtu akaenda zake kuanzisha kivyake huku akiendelea kuomba msaada wa hapa na pale inawezekana?
Nina maswali mengi ila naomba msaada kunijibu haya kwanza mkuu...nakushkuru tena kwa mwanga huu kiasi uliotupatia
Kaka me nimekulewa vzr na shukran kwa uchambuzi mzuri.1. kuna kitu watu wengi huwa wanachanganya naomba nikueleweshe mkuu Starlink haji kufanya Hotspot business hata kidogo tena akija starlink kwa sisi tunaofanya Hotspot itakuwa neema zaidi kwakuwa tutaweza kuuza hadi vijijini naomba nikueleze hotspot kwa lugha rahisi kabisa najua unafahamu hili neno WINGA huyu ni mfanyabiashara mdogo amabae ananunua au kuchukua biashara kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa au wa kati na kuiwasilisha watumiaji sasa nakurudisha huku kwenye mada sasa unamuona AIRTEL,TIGO,VODACOM,STARLINK hawa tunawaita ISP ( Internet Service Providers ) hawa wanatoa huduma ya internet katika Wholesale na retail sale sasa Hotspot nayo ni huduma ya kutoa internet katika levo ya MACHINGA hivo uwepo wa ISPs wengi kwetu ni neema ya kupata internet kwa bei rahisi na sisi kuiuza kwa bei nzuri zaidi kwaio starlink na ISPs wengine sio tishio la hotspot fuatilia hata bei za receiver za STARLINK still bado sio internet nafuu kama wengi mnavyodhani ila kwasisi HOTSPOT enterprenuers tunafurahia uwepo wao
2. haiwezekani hata kidogo kwanza kwetu ni faida zaidi unajua kwanini ni kwasababu router ina limitation na hao wote wanasambaza CPEs router ( CUSTOMER PREMISES EQUIPMENT ) ni kifaa maalumu cha kupokea internet kutoka kwa mtoa huduma wa internet ambao kusudio kubwa ni kuwezesha internet nyumbani au ofisini ila hotspot inaweza kusambaza internet mtaa mzima mfano ni wangapi katika jamii yetu wanaweza kununua router na kuendeleza malipo ya bando la laki kila mwezi ? sio wengi kwaio bado kuna jamii kubwa inayohitaji ila haina uwezo wa kuigharamia ila kupitia Hotspot inakuwa mkombozi wao mfano mimi katika internet ya mtaa nampa mteja mmoja unlimited internet kwa mwezi mzima kwa 20,000 tu
3. HOTSPOT ni kitu ya tofauti na inanafasi kubwa sanaaa Tanzania na advantage kubwa sana ya soko kwakuwa tuna idadi kubwa ya watu na pia ambao wanatumia sana smartphone iwe mjini au vijijini mimi nili take risk kwa kujifunza kupitia watu wa philipino na malesia kwa kulipa tusion fee na bahati nzuri baadhi ya wadau wa kenya mana biashara hii kwa kenya na uganda ni kubwa sanaa na sio ngeni kabisa ila kwa Tanzania haijasambaa kabisa na sehemu kubwa inapatikana Dar pekee nimetembelea mikoa mingi kiukweli hii ni biashara pekee ambayo haina ukanda kwa sasa inaweza kufanyika popote
4. sio lazima usiome itakuchukua muda ku master na kuianza kuifanya mfano mimi nilichua muda ku master sasa nahangaika mitaji ya kuikuza ila wewe unaweza kuwa na mtaji ila ikakuchukua muda kui master hivo ukajikuta uko nje ya matarajio kwakuwa bado huna experiance na ndio mana tunatafuta joint ya mwenye ujuzi na mtaji kwakuwa kwa pamoja tutaokoa muda na rasilimali kwa pamoja
5 Ndio nafanya hivo kuna training fee na monthly fee ambayo kwa kila mwezi baada ya kuanza biashara ni 30,000 tu
Nafikiri nimejibu maswali yako yotee
Makalio yako me sina demu kama mkeo mvaa malapa marefu.Toto tundu unaturingishia furaha yako ya krismas na demu wako mwajuma ndala ndefu?
Nyau ww
Hahahahahaaaaa toto tundu.Makalio yako me sina demu kama mkeo mvaa malapa marefu.
Naunga hoja hii mkonoKijana acha kwanza tufurahie X-Mas kwa amani wakati huu, mwaka umekwisha tukutane mwakani.
Pumbafu kabisa.Hahahahahaaaaa toto tundu.
Nyau wewe
Wewe ni nyau tu huna uhalali wa kusheherejea krismasi na mwajuma ndal ndefu. Toto tunduuuuPumbafu kabisa.
Lianzishe tyuuu mkuu wadau wapoDah mimi mwenyewe na wazo sijui nalianzisha vipi na hamu inaisha
Mwekezaji utampata, sema huwa hawakoment hapa...hawana blah blahNatumaini ni wazima wa Afya na heri ya mapumziko ya mwisho wa mwaka
Najua mwaka huu ulikuwa na changamoto nyingi na baadhi yetu tulikuwa na malengo mengi naimani kwa uwezo wake M/Mungu mwaka ujao tutakamilisha au kuanzisha ndoto tulizoacha
Nisiwachoshe sana kwa salamu ni kama kichwa kinavyojieleza hapo ya kuwa nahitaji muwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika hotspot business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6 na ataendelea kupata gawio la milioni 5 kila mwezi
Kwanini naandika hili ni kwakuwa naimani sisi katika kujaaliwa ridhki tumetofautiana naimani kuna mtu ana kiasi fulani cha fedha na hajua wapi pa kuwekeza au hana mtu sahihi wa kumshauri kuwekeza, lakini pia kuna akina sisi tuna mawazo mbali mbali ya kibiashara lakini hatuna mitaji ya kuwekeza
Hivo basi lengo la uzi huu ni kumfikia yule mwenye mtaji ila hajui wapi pa kuwekeza ili tuweze kushirikiana na kulisongesha gurudumu la mafanikio kwa pamoja.
Turudi kwenye mada Husika ni kuwa nahitaji muwekezaji wa kiasi kisichopungua 50 millioni kwaajili ya biashara ya HOTSPOT BUSINESS
Nini maana ya HOTSPOT ?
Hotspot Ni sehemu ambayo inakupa muunganisho wa internet kwa kutumia WI-FI bila kutumia nyaya
Nini maana ya WI-FI ?
Kwanza kabisa tufahamu kirefu cha neno WI-FI (Wireless Fidelity)
Wireless Fidelity ni teknolojia inayotumika kuunganisha vifaa kwenye mtandao wa internet bila nyaya
sasa kwakuwa tumeshafahamu maana ya hotspot na maana ya wi-fi sasa turudi kwenye mada ili twende sawa
Nini maana ya HOTSPOT BUSINESS ?
Hotspot Business ni biashara ya kuuza Huduma ya internet kwa njia ya WI-FI katika eneo fulani kwa malipo au makubaliano maalumu, sehemu hizo ni kama mtaani,sokoni,vyuoni na eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu
kwa maelezo ya ziada biashara ya hotspot hufanyika katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu eidha ni wakaazi wa eneo husika au mahala pa biashara ambao watu hukutana na kushinda muda mrefu eneo hilo kwa siku zote mfano stand,sokoni,mtaani
unaweza pitia uzi wenye kichwa cha habari hichi kuongeza ujuzi zaidi Tengeneza hadi 50,000/= kwa siku kwa kufanya biashara ya kuuza internet kupitia WiFi kwenye maeneo yenye mkusanyiko
sasa basi kwakuwa tumeshafahamu nini kusudio la huu uzi sasa tuangalie huo mchananuo wa uwekezaji unao hitajika kiujumla mpaka ukafikia thamani hiyo tajwa hapo juu
ili kufanikisha biashara ya hotspot kuna vitendea kazi uhitajika kwaajili ya kukamilisha biashara hii ya Hotspot
1. Internet ( Hutolewa na kampuni za mawasiliano kama TTCL,HALOTEL,TIGO n.k )
2. Router ( Huuzwa madukani au hutolewa na kampuni za mawasilaino ukinunua huduma zao )
3. Gateway ( Huuzwa madukani )
4. Access Point ( Huuzwa madukani )
sasa basi ukiwa na vifaa tajwa hapo juu tayari unakuwa na vitendea kazi maalumu kwaajili ya biashara ya Hotspot sasa naomba nikupe hesabu kwanini inahitajika 50 milioni
Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache tuliopata fursa ya kuutambua uwekezaji huu adimu hapa nchini na wenye faida ya uhakika na kwabahati nzuri tunafanya na kunufaika hadi sasa na lengo la kutafuta uwekezaji ni kuona namna gani tunaweza kufikia masoko zaidi ili kutengeneza faida zaidi
ili upate faida kubwa katika biashara ya hotspot yakupasa kufanya uwekezaji mkubwa
MFANO makadirio ya faida inayoweza kupatikana katika biashara ya hotspot kwa uwekezaji wa kiasi cha milioni 50 na hii sio makadirio ya kichwani ni kutokana na uzoefu na muundo wa biashara hii ambayo tayari nimeifanya kwa makadirio ya miaka miwili sasa
tumeona hapo juu mahitaji halisi ili kufanikisha biasharA hii ya hotspot ambayo ni
internet ,Router ,Gateway ,Access point sasa hii hotspot huwa tunafunga kwa site sasa ngoja tuone site moja inahitaji mtaji wa kiasi gani
MTAJI KWA SITE MOJA YA HOTSPOT
Vitendea kazi vinavyohitajika
internet nanunua kwa 200,000/= malipo ya kila mwezi
Router nanunua kwa 250,000/= malipo ya mara moja
Gateway nanunua kwa 150,000/= malipo ya maramoja
Access point nanunua 1 kwa 350,000/= hivo kwa site moja uhitajika 5 ambazo ni sawa na 1,750,000/=
Extra accessories (erthenet,RJs,climper,cable tie ) nanunua 150,000/=
kwa mchanganuo huu tunapata jumla ya Tsh 2,500,000/= za uwekezaji katika site moja
hivo basi tukirejea kwa dhumuni letu la kupata muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50 milioni tunakusudia kupata mtaji wa kuweza kuanzisha sites 20
sasa hela inapatikana vipi kwa site moja ?
kwa namna mimi ninavofanya kwa site moja naweza kukusanya 40,000 kimo cha chini kwa siku 30,000
sasa kwakuwa tunahitaji muwekezaji wa kutupa mtaji wa 50,000,000 ambao ni sawa na site 20 tunaweka makadirio kila siku kwa site moja ikusanye kiasi cha 25,000 tu hii inamaanisha kwa site zote 20 tutakusanya 500,000 kwa siku
yaani kimahesabu 20 x 25,000 = 500,000 kwa siku
tukichukua makusanyo ya siku kwa mwezi ni sawa na
500,000 x 30 = 15,000,000/= Makusanyo kwa mwezi
tukitoa matumizi ya lazima ya kila mwezi kama nilivoainisha hapo juu ni malipo ya internet kwa mwezi
ambapo kwa site moja tumeona ni 200,000 kwa mwezi hivo kwa site 20 itakuwa
200,000 x 20 = 4,000,000 hii ndio gharama ya mwezi
kwakuwa tumeona kuwa kila mwezi tunahitajika matumizi ya internet basi tutachukua makusanyo ya jumla na kutoa matumizi ya lazima
15,000,000 makusanyo ya jumla mwezi mzima
4,000,000 malipo ya internet kwa mwezi mzima
15,000,000 - 4,000,000 = 11,000,000 kiasi kinachobaki
sasa kwanini tulisema kuwa muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50,000,000 ataweza kurudisha mtaji wake kwa muda wa miezi sita na kuendelea kula faida kila mwezi isiopungua ya 5,000,000 ni kwa hesabu hii
kwakuwa tumeona kiasi ambacho kitaweza kubakia kwa mwezi ni 11,000,000 au 10,000,000 basi tutachukua hichi kiasi na kuzidisha mara 6 muda ambao tumeweka maximum muwekezaji kurudisha mtaji wake
kwaio
10,000,000 x 6 = 60,000,000/= au tunaweza weka makadirio ya 50,000,000/=
Hapo tutakuwa tumefanikisha kurudisha kiasi cha mtaji wa muwekezaji kilichobaki ni muendelezo wa safari ya kufurahia matunda ya uwekezaji wake ambao sisi tumeona iwe nusu ya faida itakayopatikana kwa kuthamini mchango wa muwekezaji kwa kuweka mtaji na sisi kuweka ujuzi wetu katika fursa hii
ambapo kama kwa mwezi makusanyo baada ya kutoa kila kitu kubakia 10,000,000 basi nusu itakuwa ya muwekezaji na nusu itskuewa ya kwetu sisi
JE NIKIWA KAMA MUWEKEZAJI NA UHAKIKA GANI WA KUREJESHA MTAJI WA PESA YANGU ?
Ukiwa na swali kama hili mimi nitakujibu hivi
inawezekana kurejesha hicho kiasi kwa muda kusidio kwakuwa hii ni biashara ya kisasa japo ngeni kwa macho ya wengi ila mimi nina uzoefu nayo kwa muda wamiaka miwili sasa na bado ninaifanya mpaka sasa hivo kumbukumbu za makusanyo yote katika site zangu yapo na tunamfumo wa kisasa kusimamia biashara hii mahali popote Tanzania hivo muwekezaji anauwezo wa kuona na kutambua kila kinachoendelea katika mfumo mahali popote alipo
lakini pia tunatoa fursa ya kutembelea mradi ulipo ambapo tunapatikana Dar es salaam na baadhi ya mikoa tumefunga hivo unaweza kujionea jinsi tunavyoendesha biashara hii na namna faida inavyoweza kuaptikana
Kwa wale wenye ndugu jamaa na marafiki ambao unaimani wanamitaji ila hawaoni pa kuwekeza tunawakaribisha muweze kuuliza maswali na tutajibu kila moja na kwa yule anaehitaji kuwekeza basi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0710020066