Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Nahitaji mwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika Hotspot Business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6

Lianzishe tyuuu mkuu wadau wapo
Kuna watu wengi sana wana maarifa ila wanachohofia ni tatizo la humu ukileta madini ujiandae challenges za kutosha,shida yetu kubwa ki kwamba kila mtu huku ni mjuaji na kwamb huna cha kumwambia
 
Hao wadau mpka uwa shawishi
Alafu wasiwe na tamaa wakabeba wazo lako na kulifanya wao kwakua wanapesa
Hiyo ni changamoto kubwa hasa kwa wadau waswahili njia pekee Bora ambayo Mimi nimejifunza ni kuwa na mikataba ya kisheria itakayo ruhusu kupata stahiki zako lakini kingine wewe kama mwenye wazo unawazo tyuu na utaweza kulifanya Bora kuliko mwingine
 
Hiyo ni changamoto kubwa hasa kwa wadau waswahili njia pekee Bora ambayo Mimi nimejifunza ni kuwa na mikataba ya kisheria itakayo ruhusu kupata stahiki zako lakini kingine wewe kama mwenye wazo unawazo tyuu na utaweza kulifanya Bora kuliko mwingine
Mikataba ni hii ya non disclosure agreement NDA?
maan kuna mtu aliomba nimtumie mkataba online ili a sign kwamba asiweze kutumia wazo langu
Ila bdo sikuwa na iman nae kwakuw tuko mazingira ya mbali
 
N
Mikataba ni hii ya non disclosure agreement NDA?
maan kuna mtu aliomba nimtumie mkataba online ili a sign kwamba asiweze kutumia wazo langu
Ila bdo sikuwa na iman nae kwakuw tuko mazingira ya mbali
Ni ku take risk tu kwani wazo lako umeshaanza kuzifanyia kazi ? Kama Bado Anza kulifanyia kidogo wadau watajitokezaga baadae
 
Natumaini ni wazima wa Afya na heri ya mapumziko ya mwisho wa mwaka

Najua mwaka huu ulikuwa na changamoto nyingi na baadhi yetu tulikuwa na malengo mengi naimani kwa uwezo wake M/Mungu mwaka ujao tutakamilisha au kuanzisha ndoto tulizoacha

Nisiwachoshe sana kwa salamu ni kama kichwa kinavyojieleza hapo ya kuwa nahitaji muwekezaji wa kuwekeza milioni 50 katika hotspot business, mtaji utarudi ndani ya miezi 6 na ataendelea kupata gawio la milioni 5 kila mwezi

Kwanini naandika hili ni kwakuwa naimani sisi katika kujaaliwa ridhki tumetofautiana naimani kuna mtu ana kiasi fulani cha fedha na hajua wapi pa kuwekeza au hana mtu sahihi wa kumshauri kuwekeza, lakini pia kuna akina sisi tuna mawazo mbali mbali ya kibiashara lakini hatuna mitaji ya kuwekeza

Hivo basi lengo la uzi huu ni kumfikia yule mwenye mtaji ila hajui wapi pa kuwekeza ili tuweze kushirikiana na kulisongesha gurudumu la mafanikio kwa pamoja.

Turudi kwenye mada Husika ni kuwa nahitaji muwekezaji wa kiasi kisichopungua 50 millioni kwaajili ya biashara ya HOTSPOT BUSINESS

Nini maana ya HOTSPOT ?
Hotspot
Ni sehemu ambayo inakupa muunganisho wa internet kwa kutumia WI-FI bila kutumia nyaya

Nini maana ya WI-FI ?
Kwanza kabisa tufahamu kirefu cha neno WI-FI (Wireless Fidelity)

Wireless Fidelity ni teknolojia inayotumika kuunganisha vifaa kwenye mtandao wa internet bila nyaya

sasa kwakuwa tumeshafahamu maana ya hotspot na maana ya wi-fi sasa turudi kwenye mada ili twende sawa

Nini maana ya HOTSPOT BUSINESS ?
Hotspot Business ni biashara ya kuuza Huduma ya internet kwa njia ya WI-FI katika eneo fulani kwa malipo au makubaliano maalumu, sehemu hizo ni kama mtaani,sokoni,vyuoni na eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu

kwa maelezo ya ziada biashara ya hotspot hufanyika katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu eidha ni wakaazi wa eneo husika au mahala pa biashara ambao watu hukutana na kushinda muda mrefu eneo hilo kwa siku zote mfano stand,sokoni,mtaani

unaweza pitia uzi wenye kichwa cha habari hichi kuongeza ujuzi zaidi Tengeneza hadi 50,000/= kwa siku kwa kufanya biashara ya kuuza internet kupitia WiFi kwenye maeneo yenye mkusanyiko

sasa basi kwakuwa tumeshafahamu nini kusudio la huu uzi sasa tuangalie huo mchananuo wa uwekezaji unao hitajika kiujumla mpaka ukafikia thamani hiyo tajwa hapo juu

ili kufanikisha biashara ya hotspot kuna vitendea kazi uhitajika kwaajili ya kukamilisha biashara hii ya Hotspot
1. Internet ( Hutolewa na kampuni za mawasiliano kama TTCL,HALOTEL,TIGO n.k )
2. Router ( Huuzwa madukani au hutolewa na kampuni za mawasilaino ukinunua huduma zao )
3. Gateway ( Huuzwa madukani )
4. Access Point ( Huuzwa madukani )

sasa basi ukiwa na vifaa tajwa hapo juu tayari unakuwa na vitendea kazi maalumu kwaajili ya biashara ya Hotspot sasa naomba nikupe hesabu kwanini inahitajika 50 milioni

Mimi ni miongoni mwa watanzania wachache tuliopata fursa ya kuutambua uwekezaji huu adimu hapa nchini na wenye faida ya uhakika na kwabahati nzuri tunafanya na kunufaika hadi sasa na lengo la kutafuta uwekezaji ni kuona namna gani tunaweza kufikia masoko zaidi ili kutengeneza faida zaidi

ili upate faida kubwa katika biashara ya hotspot yakupasa kufanya uwekezaji mkubwa

MFANO makadirio ya faida inayoweza kupatikana katika biashara ya hotspot kwa uwekezaji wa kiasi cha milioni 50 na hii sio makadirio ya kichwani ni kutokana na uzoefu na muundo wa biashara hii ambayo tayari nimeifanya kwa makadirio ya miaka miwili sasa


tumeona hapo juu mahitaji halisi ili kufanikisha biasharA hii ya hotspot ambayo ni
internet ,Router ,Gateway ,Access point sasa hii hotspot huwa tunafunga kwa site sasa ngoja tuone site moja inahitaji mtaji wa kiasi gani

MTAJI KWA SITE MOJA YA HOTSPOT
Vitendea kazi vinavyohitajika
internet
nanunua kwa 200,000/= malipo ya kila mwezi
Router nanunua kwa 250,000/= malipo ya mara moja
Gateway nanunua kwa 150,000/= malipo ya maramoja
Access point nanunua 1 kwa 350,000/= hivo kwa site moja uhitajika 5 ambazo ni sawa na 1,750,000/=
Extra accessories
(erthenet,RJs,climper,cable tie ) nanunua 150,000/=
kwa mchanganuo huu tunapata jumla ya Tsh 2,500,000/= za uwekezaji katika site moja
hivo basi tukirejea kwa dhumuni letu la kupata muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50 milioni tunakusudia kupata mtaji wa kuweza kuanzisha sites 20
sasa hela inapatikana vipi kwa site moja ?

kwa namna mimi ninavofanya kwa site moja naweza kukusanya 40,000 kimo cha chini kwa siku 30,000

sasa kwakuwa tunahitaji muwekezaji wa kutupa mtaji wa 50,000,000 ambao ni sawa na site 20 tunaweka makadirio kila siku kwa site moja ikusanye kiasi cha 25,000 tu hii inamaanisha kwa site zote 20 tutakusanya 500,000 kwa siku

yaani kimahesabu 20 x 25,000 = 500,000 kwa siku
tukichukua makusanyo ya siku kwa mwezi ni sawa na
500,000 x 30 = 15,000,000/= Makusanyo kwa mwezi
tukitoa matumizi ya lazima ya kila mwezi kama nilivoainisha hapo juu ni malipo ya internet kwa mwezi
ambapo kwa site moja tumeona ni 200,000 kwa mwezi hivo kwa site 20 itakuwa
200,000 x 20 = 4,000,000 hii ndio gharama ya mwezi

kwakuwa tumeona kuwa kila mwezi tunahitajika matumizi ya internet basi tutachukua makusanyo ya jumla na kutoa matumizi ya lazima
15,000,000 makusanyo ya jumla mwezi mzima
4,000,000 malipo ya internet kwa mwezi mzima

15,000,000 - 4,000,000 = 11,000,000 kiasi kinachobaki

sasa kwanini tulisema kuwa muwekezaji wa kiasi cha Tsh 50,000,000 ataweza kurudisha mtaji wake kwa muda wa miezi sita na kuendelea kula faida kila mwezi isiopungua ya 5,000,000 ni kwa hesabu hii

kwakuwa tumeona kiasi ambacho kitaweza kubakia kwa mwezi ni 11,000,000 au 10,000,000 basi tutachukua hichi kiasi na kuzidisha mara 6 muda ambao tumeweka maximum muwekezaji kurudisha mtaji wake

kwaio
10,000,000 x 6 = 60,000,000/= au tunaweza weka makadirio ya 50,000,000/=

Hapo tutakuwa tumefanikisha kurudisha kiasi cha mtaji wa muwekezaji kilichobaki ni muendelezo wa safari ya kufurahia matunda ya uwekezaji wake ambao sisi tumeona iwe nusu ya faida itakayopatikana kwa kuthamini mchango wa muwekezaji kwa kuweka mtaji na sisi kuweka ujuzi wetu katika fursa hii

ambapo kama kwa mwezi makusanyo baada ya kutoa kila kitu kubakia 10,000,000 basi nusu itakuwa ya muwekezaji na nusu itskuewa ya kwetu sisi

JE NIKIWA KAMA MUWEKEZAJI NA UHAKIKA GANI WA KUREJESHA MTAJI WA PESA YANGU ?
Ukiwa na swali kama hili mimi nitakujibu hivi
inawezekana kurejesha hicho kiasi kwa muda kusidio kwakuwa hii ni biashara ya kisasa japo ngeni kwa macho ya wengi ila mimi nina uzoefu nayo kwa muda wamiaka miwili sasa na bado ninaifanya mpaka sasa hivo kumbukumbu za makusanyo yote katika site zangu yapo na tunamfumo wa kisasa kusimamia biashara hii mahali popote Tanzania hivo muwekezaji anauwezo wa kuona na kutambua kila kinachoendelea katika mfumo mahali popote alipo

lakini pia tunatoa fursa ya kutembelea mradi ulipo ambapo tunapatikana Dar es salaam na baadhi ya mikoa tumefunga hivo unaweza kujionea jinsi tunavyoendesha biashara hii na namna faida inavyoweza kuaptikana

Kwa wale wenye ndugu jamaa na marafiki ambao unaimani wanamitaji ila hawaoni pa kuwekeza tunawakaribisha muweze kuuliza maswali na tutajibu kila moja na kwa yule anaehitaji kuwekeza basi usisite kuwasiliana nasi kupitia 0710020066
Umeandika vzur sana. Hzo site zako ztakua znatumia umeme au solar.....?
Kama siku umeme ukikatika inakua n Hasara kama Huna Backup yoyote.
 
N

Ni ku take risk tu kwani wazo lako umeshaanza kuzifanyia kazi ? Kama Bado Anza kulifanyia kidogo wadau watajitokezaga baadae
Asante mkuu
Mana kwa tz halipo wala hata africa mashariki hii hamna
Nawaza ni namn gan litapokelewa
Wateja watanielewa
 
Umeandika vzur sana. Hzo site zako ztakua znatumia umeme au solar.....?
Kama siku umeme ukikatika inakua n Hasara kama Huna Backup yoyote.
Hapana hamna hasara mkuu ni kwamba once umeme umekayika na mteja anafahamu umekatika na anajua it's not your fault hawana noma ila ikitokea umekatika maybe 24 hours huwa tunawapa vocha za kufidia muda ulipotea na wengi wako OK na hiyo kwao
 
Asante mkuu
Mana kwa tz halipo wala hata africa mashariki hii hamna
Nawaza ni namn gan litapokelewa
Wateja watanielewa
Let's join kama Iko practical hata kwa kidogo ilimradi iwe friendly na mazingira na watu wetu Mimi huwa na interest ya kujaribu kitu kigeni kwa sababu ni fursa zenyewe
 
Kwa wauzaji wa Internet WI-FI panua biashara yako upate faida kubwa bila kutumia nguvu nyingi kwa kutumia mfumo wa vocha unawomuwezesha kuwauzia wateja wako wifi kwa kumpa vocha na mfumo wenyewe unawawekea security, hakuna kuscan kwa mtu yeyote anapojiunga kwa vocha

Mfumo wa vocha unakazi hizi kuu:

🟢 1. Kudhibiti nani anapata intaneti
Mtumiaji hawezi kuingia moja kwa moja.
Anatakiwa:
Kupata vocha (code)
Kuingiza kwenye login page
Ndipo router inamruhusu kutumia intaneti
Hii husaidia kuepuka watu kujiunga bila kulipa.

🟢 2. Kupima muda au kiasi cha intaneti
Router inahesabu kulingana na kifurushi, mfano:
Saa 1
Masaa 24
Week
Bundle GB
Baada ya muda/GB kuisha ➜ vocha inafunga automatically.

🟢 3. Kuhifadhi taarifa za watumiaji
Router huhifadhi:
Ni nani alitumia vocha gani
Muda aliotumia
Kiasi cha data kilichotumika
Hii ni muhimu kwa:
Uhasibu wa mauzo
Kufuatilia matumizi
Kuzuia wizi wa vocha

🟢 4. Kupunguza mzigo wa mtandao
Router ya vocha inaweza kuweka:
Speed limit (mf. 2Mbps per user)
Max devices per voucher
Fair usage
Hii inafanya mtandao usizidi kuchoka.

🟢 5. Kurahisisha biashara ya Wi-Fi
Ni muhimu kwa:
Wi-Fi hotspot
Cyber café
Mashule
Hostel
Mabanda ya mitaa

Inawezesha mmiliki:
Kuuza vocha
Kupanga vifurushi
Kupata faida bila kusimamia sana

🔹 Kwa kifupi
Router ya vocha:
👉 Inadhibiti upatikanaji wa intaneti
👉 Inauza na kusimamia vifurushi
👉 Inapima muda / data
👉 Inazuia watu kutumia bure
👉 Inasaidia biashara ya Wi-Fi kuwa rasmi

Karibu kwa ushauri 0710599055
 
Uzi mzuri na mawazo zuri yako hapa, ila sijaona mleta mada au yoyote akiliongelea suala la kodi na malipo ya serikali mana hii ni biashara, navojua TCRA wanatoa kibali cha kufanya hii biashara, je mleta mada anacho hichi kibali? Je unazifaham fees za tcra unazotakiwa kulipa kila mwaka kama utafanya hii biashara?
 
Hongera mkuu.
Inaonekana uko vizuri kwenye masuala ya tech,
Infact umenipiga gap hapo.

Hata hivyo hiyo siyo sababu yenye mashiko ya kuprove how inawezekana kupata ROI ya 6 months na 5M profit per month.

Mimi kama Investor ntahitaji proof, legal safeguards, audited financials na contingency plan.

Hiyo confidence yako + experience inatakiwa ilete advantage na siyo maelezo matupu.

Tatizo mkikutana na majibu ambayo hamkutarajia mnakimbilia kusema "Negative energy".
Weka hisia pembeni tujadili hoja kwa hoja.

Kama unabaki unashikilia assumptions zako bila proof kwa investor kama mimi hiyo ni high risk speculation, siyo investment yenye uhakika.
Ni kweli, ulionesha negative energy kama alivyoandika, pia umeonesha kudharau elimu kwa maneno kama "wasomi bwana", ilhali inaonyesha wewe pia ni msomi.

Kikubwa tunapaswa kutia moyo mawazo ya wengine kwakua Kila jambo tunalonufaika nalo Sasa ni matokeo ya wazo kama hili, na kikubwa zaidi katika maelezo yake inaonyesha kweli yupo field.
 
Ni kweli, ulionesha negative energy kama alivyoandika, pia umeonesha kudharau elimu kwa maneno kama "wasomi bwana", ilhali inaonyesha wewe pia ni msomi.

Kikubwa tunapaswa kutia moyo mawazo ya wengine kwakua Kila jambo tunalonufaika nalo Sasa ni matokeo ya wazo kama hili, na kikubwa zaidi katika maelezo yake inaonyesha kweli yupo field.
You're right.
But,
Hakuna negative energy,
Kuna utofauti wa uelewa katika kupokea taharifa.
 
bahati nzuri maintainance and technician nafanya mwenyewe kwakuwa namimi ni part ya mradi hivo hakuna charges kwa upande wa pango kwa muudo nao tumia huwa landlord nawapa uwakala wa kuuza vocha za wi-fi ambazo mimi nawapa voucher 10 wakiuza 5 wananipatia mwenyewe na kila vocha moja nauza 1,000 hivo anapata 10,000 kisha mimi ananipa 5,000 ndio ninavyofanyq hivo kwao inakuwa kama sehemu ya side hustle
Nielekeze vizuri na mimi kama naweza kufanya
Ila mimi sio mwekezaji naomba kujifunza tu
 
Back
Top Bottom