Nahitaji mwenye ramani ya hili jengo

Nahitaji mwenye ramani ya hili jengo

Lupe Tz

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2021
Posts
259
Reaction score
910
Kwa mwenye anaweza kuwa na ramani ya haka kajumba anitafute inbox tuongee
FB_IMG_16302267464114456.jpg
 
Nilikuwa nahitaji kama hiyo niliyoshare hapo,, mkuu tunabana matumizi pesa hakuna mjini.. au kama unaweza kunichorea sample raman kama niloshare hapo, iwe na vyumba 3(1master) store jiko na dinning.... kama hiyo hapo ....... afu unambie unaweza kunichorea kwa bei gani
FB_IMG_16302267464114456.jpg

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini utumie pesa ndefu kujenga chumba na sebule? Yaani hata upendezeshe vipi haikuongezei heshima mtaani. Chumba na sebule tumia ramani ya kawaida ya mstatiri. Tena ikibidi laza bati tu.
Kwani shida yako ni nini ndugu?
Yeye anataka haka kajumba, alafu wewe unataka kumlazimisha alaze bati na hayo mamstatiri yako; Ebo!
Binadamu hamna dogo.
 
Hauko serias,mwenzio anaulizia chumba na sebule we unaleta mahekalu

Mkuu hizo ni sample kuonesha kwamba kama tunaweza kuchora hivyo vitu, hatuwezi shindwa chora nyumba yake ndogo, hakuna sehemu nimesema achague hapo!!
 
M
Nilikuwa nahitaji kama hiyo niliyoshare hapo,, mkuu tunabana matumizi pesa hakuna mjini.. au kama unaweza kunichorea sample raman kama niloshare hapo, iwe na vyumba 3(1master) store jiko na dinning.... kama hiyo hapo ....... afu unambie unaweza kunichorea kwa bei ganiView attachment 1916574

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Mkuu kiweke pande zote nikuchoree ramani yake buree utalipia karatasi TU mkuu
 
Kina choo ndani kweli hcho au choo mpk ufunge safar
 
Kwani shida yako ni nini ndugu?
Yeye anataka haka kajumba, alafu wewe unataka kumlazimisha alaze bati na hayo mamstatiri yako; Ebo!
Binadamu hamna dogo.
Mimi sina shida na matakwa yake. Lakini kutokana na uzoefu wangu kwenye mambo ya ujenzi, watu wengi huamua kujenga nyumba ndogo kutokana na hofu ya gharama. Mwisho wa siku unakuta gharama anayoitumia kujenga chumba na sebule, inakaribiana kabisa na gharama ya kujenga vyumba viwili na sebule. Zaidi sana akijipa muda akajenga taratibu anapata vyumba vitatu na sebule, ambayo ni standard kwa familia nyingi za kawaida.

Wewe mwenyewe umekaita "Kajumba". Hili ndo litageuka jina la nyumba yake, na pia jina lake, la watoto wake hadi la mifugo yake. Nyumba itageuka kero.

Binafsi mara nyingi huwa nawauliza wateja wangu, katika kipindi cha miaka mitano ijayo unataka nyumba yako iweje? Kama kunatofauti kubwa kati ya nyumba anayoitaka miaka mitano ijayo na hiyo anayopendekeza kujenga, hapo ndo nitamushauri namna ya kuanza ili afikie lengo ndani ya huo muda. Kama hakuna tofauti ya nyumba ya sasa na ile aitakayo, namwambia twende kazi.
 
kweli mkuu, ushauri ni zaidi ya pesa,,,woga unaleta madhara kwa mambo mengi

hii kauli ya nitaweza kweli iondoke vinywani mwetu kwa kweli,,,aliweza yule sisi wengine tushindwe tuna nini?
 
Nilikuwa nahitaji kama hiyo niliyoshare hapo,, mkuu tunabana matumizi pesa hakuna mjini.. au kama unaweza kunichorea sample raman kama niloshare hapo, iwe na vyumba 3(1master) store jiko na dinning.... kama hiyo hapo ....... afu unambie unaweza kunichorea kwa bei ganiView attachment 1916574

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Hii ulio-share haiwezi kuwa na facility zote hizo ulizotaja labda kama unahitaji muundo kama huo ila eneo la nyumba liongezeke.
 
Mnajua kuchora ramani/kushauri/nk lakini hivi ni kwanini mkiulizwa bei na mtu/mteja huwa hamuwezi kujibu Openly mnaishia kutoa namba za Simu mtafutwe?!

Huwa ni kwanini nyie watu wenye bei kubwa mnaogopa kutaja bei zenu za kazi zenu wazi wazi?

Mnamuogopa nani? Hamjiamini? Kama Raman ni Milioni unafunguka unasema tu Hizo bei mnazoziona kubwa kwa wengine ni vipesa vidogo sana.

Nawashauri : Mnapoulizwa bei ya jambo lolote lile bila kuhofia chochote Taja Bei iwe kwenye comment au maongezi usifiche bei ya Bidhaa/huduma unayotoa kwa kuhofia Utapoteza wateja wengine.

Huwezi kupoteza mteja kisa kasikia Una gharama na ukiona umempoteza Mteja Elewa na fahamu huyo hakua Mteja hata kama asingejua bei bado asingekua mteja wenu.

Lakini kwa kutaja bei wazi wazi itashawishi wengine wapembeni kujua na hatimae kujipanga na akiwatafuta anakua kashajua Kampuni ile kazi zao lazima niwe nimejipanga.

Itawasaidia kupata wateja walio Serious na kazi na wenye uhitaji wa kweli.

Sijui kama nimeeleweka bwana Mkubwaaa, ni ushauri tu wa hapa na pale.
 
Nile_house_designs Ramani Ya Nyumba ya ghorofa 1 yenye Master Rooms 3 Juu na sehemu ya kupumzikia kwa Juu

Chini Master rooms 2, sitting room,dining,store,Public Toilet na sehemu ya kupumzikia kwa nnje

Ramani ya nyumba ya namna hiyo mnachora kwa gharama gani?!
 
Kwa HARAKA HARAKA hapo Ni chumba self,jiko dining na sebule
 
Back
Top Bottom