Nahitaji mwenza

Molina

New Member
Joined
Jul 30, 2024
Posts
3
Reaction score
23
Poleni na Shughuli za siku wana JF,

Nimekuja nikiwa na uhitaji wa kupata mwenza Mwanaume. Mwenye uhitaji na mahusiano aliechoka kua mpweke kama mimi.

Awe mwanaume mwenye umri kuanzia miaka 32 na kuendelea.
Awe anajishughulisha na shughuli halali.
Mwenye hofu ya Mungu.
Asiwe mtumiaji wa kileo,na mambo yanayofanana na ayo.
Awe Mkristo, Akiwa Mpentecoste(na yakufanana na ayo itakua vizuri).
Ni sawa akiwa na mtoto maana na mimi nina mtoto mmoja.

Mimi ni mwanamke wa miaka 30, Ni mama wa binti mmoja.
Nmeajiliwa(private sector) Ninaishi Dar es salaam.
Ninampenda Mungu, Nimekua mpweke kwa mda mrefu sasa.
Karibu Pm.

Ahsante.
 
Utaishia kuchezewa tu na mawenge yako ya kutafuta wanaume wewe kama una tabia njema utapata tu mwanaume kaa utulie ila tatizo ni kwamba kwa umri uo tena ni single mother kazi unayo ila pambana utawapata wenzako walio kata tamaa kama wewe
 
Wenzetu Dunia nyingine wanaheshimu mahusiano ndio maana wanakutana mtandaoni wanaoana, Hapa Tegemea kutumika auachike. yaani wale walioshindikana na kukatalika kwao ndio watakufuata kukutumia wakuongezee mtoto wasepe.
STUKA MAMA
 
Kwanza pole kwa upweke ila naomba nikuulize 1.Mtoto ana miaka mingapi.
2.Baba mtoto yuko mkoa gani.
3.Kuna mawasiliano na huyo baba mtoto wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…