Nahitaji Partner au Partners 2 Tufanye biashara ya Kuuza Kuku Pamoja

Nilikuwa na mtaji cash Mil 4.5. Nimefanya matumizi na kubakiwa na cash ya mzunguko 1.5M.

Matumizi.

Freezer 2. 800,000/-
Pikipiki 1. 1,300,000/-
Baiskel. 1. 150,000/-
Kodi. 600,000/-
Mizan n.k. 200,000/-

Total. 3,050,000/-

Wastan wa faida kwa mwezi ni Tsh 450,000- 600,000/-.
Labda kama umeficha kwenye faida. Ni ndogo mno 450k kwa kugawana watu wa wili ni kazi ngumu. Labda kama mtu akija chemba mnaweza kuongea vizur...... Is it possible mtu aweke 3.5 hadi tano then atoke. Na laki mbili na nusu kwa mwezi.???
 
Hujaelewa kaka, Capital ikiongezeka obvisiously na Faida itaongezeka...Amesema cash ya mzunguko ni 1.5M so akipata patner akaongezea mtaji basi lazima na faida itakua juu
 
Samahani, labda tumeelewa tofauti. Namaanisha kwa wastani wa capital ya 4M unaweza pata 450,000/- Hadi 600,000/- kwa mwezi Kama faida.

Yaani roughly faida huwa ni 10% ya capital yako kila mwezi.
 
Yaani roughly faida huwa ni 10% ya capital yako kila mwezi
Hujaelewa kaka, Capital ikiongezeka obvisiously na Faida itaongezeka...Amesema cash ya mzunguko ni 1.5M so akipata patner akaongezea mtaji basi lazima na faida itakua juu
Asante kwa ufafanuzi zaidi Mkuu! Ni kweli, capital ikiongezeka na faida automatically itapanda.
 
Samahani, labda tumeelewa tofauti. Namaanisha kwa wastani wa capital ya 4M unaweza pata 450,000/- Hadi 600,000/- kwa mwezi Kama faida.

Yaani roughly faida huwa ni 10% ya capital yako kila mwezi.
Nimeelewa. So hapo muwekezaji anatakiwa kujihusisha kwenye biashara moja kwa moja au anatoa hela alafu anakaa pembeni kazi inafanywa.? Yeye anachukua tu posho yake mwisho wa mwezi.
 
Karibu Sana, lengo tufanye pamoja, uwepo nawe kwenye mishe nzima aidha bandani, ofisini au kwenye ku interact na wateja, ni business yetu tuifanye pamoja.
Incase umebanwa na majukum mengine, mlete mtu tufanye kazi pamoja hii ndo lengo hasa, tuwe team moja.

Ikishindikana kabisa kuwepo au kuleta mwakilishi wako Basi unaweza ukashiriki partially na angalau kila weekend unapokuwa free unakuja ofisini, tunapeana reports za wiki na projections za wiki inayokuja. Though sio kipaumbele option hii.
 
Hongera sana, ushirikiano ni jambo zuri sana na lenye manufaa. Ukipata mwelewa mkafanya biashara kama ndugu na kuwekeza mtaji huku MUNGU akiwa pamoja nanyi mtafanikiwa.

Lakini kuna mbadala wa mawazo chanya ambayo mnaweza kuyaweka akilini:

KWAKO WEWE UNAYEVUTIWA NA KUWEKEZA

Unaweza pata maelezo ya aina hii:

"Pikipiki imegongwa na hice kuku wote" wamemwagika na kuibiwa, pikipiki imeharibika hatuwezi kufanya delivery.

"Umeme umekatika katika wiki nzima kuku wote wananuka uvundo".

"Vibaka wamevunja friji, kuku wote wameondoka nao".

"Idadi ya wauza kuku imeongezeka tupo tu hapa na kuku wetu hamna wateja n.k n.k n.k"

UWE MWELEWA YATAKAPOTOKEA NI SEHEMU YA BIASHARA PIA, USIPOTEZE MUDA POLISI AU MAHAKAMANI NI GHARAMA ZAIDI.

KWAKO WEWE MWENYE BIASHARA

Mbadala wa kualika partners ni sehemu ya hiyo faida ya 450,000 mpaka 600,000 kuirudisha kwenye mtaji.

SABABU.
Ongezeko la mtaji mpya lina gharama, mtaji zaidi gharama zaidi. Kama umetumia Tsh 1.5 kuhudumia watu wa kukupa faida ya 400k mpaka 600k kwa gharama ya 2m(Pkpk, baiskeli na kodi) basi utakapokuwa na wateja wa kukupa faida double kwa kuongeza mtaji lazima gharama nazo zitaongezeka karibu mara mbili ukiacha kodi ambayo ni mara moja.

Usifanye kosa la kufikiri kuwa pikipiki ile ile, baiskeli ile ile itafanya kazi kwa gharama zile zile kwa mtaji mkubwa na kwa faida kubwa zaidi.

Faida ukiirudisha kwenye mtaji taratibu gharama nazo zinaongezeka taratibu na ni rahisi kuona tatizo tofauti na kuingiza mtaji mkubwa kwa haraka maana gharama zitakuja juu ghafla na unaweza usione tatizo na ukumbuke unakuwa na deni la mtaji mpya la kukilipa.

KILA LA HERI.
 
Hongera sana, ushirikiano ni jambo zuri sana na lenye manufaa. Ukipata mwelewa mkafanya biashara kama ndugu na kuwekeza mtaji huku MUNGU akiwa pamoja nanyi mtafanikiwa.

Lakini kuna mbadala wa mawazo chanya ambayo mnaweza kuyaweka akilini:

KWAKO WEWE UNAYEVUTIWA NA KUWEKEZA

Unaweza pata maelezo ya aina hii:

"Pikipiki imegongwa na hice kuku wote" wamemwagika na kuibiwa, pikipiki imeharibika hatuwezi kufanya delivery.

"Umeme umekatika katika wiki nzima kuku wote wananuka uvundo".

"Vibaka wamevunja friji, kuku wote wameondoka nao".

"Idadi ya wauza kuku imeongezeka tupo tu hapa na kuku wetu hamna wateja n.k n.k n.k"

UWE MWELEWA YATAKAPOTOKEA NI SEHEMU YA BIASHARA PIA, USIPOTEZE MUDA POLISI AU MAHAKAMANI NI GHARAMA ZAIDI.

KWAKO WEWE MWENYE BIASHARA

Mbadala wa kualika partners ni sehemu ya hiyo faida ya 450,000 mpaka 600,000 kuirudisha kwenye mtaji.

SABABU.
Ongezeko la mtaji mpya lina gharama, mtaji zaidi gharama zaidi. Kama umetumia Tsh 1.5 kuhudumia watu wa kukupa faida ya 400k mpaka 600k kwa gharama ya 2m(Pkpk, baiskeli na kodi) basi utakapokuwa na wateja wa kukupa faida double kwa kuongeza mtaji lazima gharama nazo zitaongezeka karibu mara mbili ukiacha kodi ambayo ni mara moja.

Usifanye kosa la kufikiri kuwa pikipiki ile ile, baiskeli ile ile itafanya kazi kwa gharama zile zile kwa mtaji mkubwa na kwa faida kubwa zaidi.

Faida ukiirudisha kwenye mtaji taratibu gharama nazo zinaobgezeka taratibu, ni rahisi kuona tatizo tofauti na kuingiza mtaji mwingi, gharama zinakuja juu ghafla na unaweza usione tatizo na ukumbuke unakuwa na deni la mtaji mpya.

KILA LA HERI.
Asante Sana brother. Kweli Target ni kuongeza vifaa pia sio hela yote kuingia kwenye mtaji. Hiyo collection point itakuwa na facilities zake za kujitegemea.

Asante kwa Tahadhar na Mawazo endelevu zaidi.

Kweli, kuanzia Mwezi ujao Tukijaaliwa ntaanza savings na plans za kujitanua kuelekea Kigambon, hopefully mambo yatakaa sawa.
 
Bro vp kuna hakuna hata kanafasi ka kazi hapo kwako maana mtaani spana zinatembea c mchezo
 
Habari za Leo Wanafamilia!

Pole na Majukum, Mm naitwa Hussein, naishi Tandika Magorofan, nna miaka 34, nna mke na watoto watatu.

Nnajishughulisha na Ufugaji, utengenezaji dawa za Asili za Kuku na uuzaji wa Kuku, kwa Sasa nimejikita zaidi kwenye Kuku wa nyama kwa kuwanunua directly kwa Wafugaji wengine au sokoni, kuwapack na kuwauuza mahotelini, mabuchani au kwenye migahawa kwa taratibu za kulipana on delivery au on credit ambapo wengi hupenda style hii.

Kutokana na kuongezeka kwa soko, na wateja wakubwa wakibaki wale wa credit imenilazimu kusaka mshirika wa kufanya nae hii biashara ili tugawane kwa kile kinachopatikana.

Mshirika atakuja kuongeza nguvu ya freezer mbili na capital ya kununua Kuku wastani 400 kila week. Ambapo nakusudia kuwe na collection point maeneo ya Kigambon, maana ukanda ule nao umebarikiwa Wafugaji wengi na nimeishi kule kipindi nafuga maeneo ya Dege.

Kwa wastani Mshirika atapaswa kuwa na capital ya Tsh Mil 3.5 Hadi Mil 5. Au wakipatikana Wawili itakuwa vzr zaidi kila mmoja atachangia pale mkono wake utakapoweza jikuna.

Wastani wa faida kwa mwezi tukitoa gharama za uendeshaji ni 10% ya capital ya kila Mshirika. Tunaweza fanya contract ya miezi 6 na kuendelea kulingana na mapenzi ya Mshirika.

Unaweza chukua capital yako kwa kutoa notice ya siku 30 kabla ili kwa mwezi husika usiwe included kwenye mgao wa faida.

Naimani mengine tutayaweka sawa pindi tukikaa mezani.

Natanguliza Shukran Sana.

Kwa mawasiliano Zaidi,

0784 645 900
0624 7400 12

Unaweza pitia fb na Instagram kwa Kukucaretz na Sokoni fresh Tz.

View attachment 1821287

View attachment 1821288

View attachment 1821289

View attachment 1821290

View attachment 1821292
Hongera Mr kuku, Ila mukiwapiga walimu wastaafu muwe mnakumbuka kuwa iko siku nanyi mtastaafu.
 
Back
Top Bottom