Nahitaji partner wa biashara vitu vya electronics. Nipo Kahama

Nahitaji partner wa biashara vitu vya electronics. Nipo Kahama

UBILUKO

Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
94
Reaction score
192
Habari wakuu , Mimi ni mtumishi hivyo katika harakati za kupambana Ili kujitafutia mkate nimeona fursa katika vitu vya electronics hasa kwa watumishi kwa kuwa mm bado sipo vizuri kwa UPANDE wa mtaji naona vema nikatafuta mfanyabiashara ambaye tutaingia partnership ambapo Mimi nitafanya yafuatayo:

1. Kutafuta wateja katika halmashauri yangu nimelenga hasa watumishi wa serikali kwa asilimia kubwa ambao nitawauzia bidhaa AMBAZO mtu tutakayeingia ubia atakuwa nazo.

2. Kufanya derivery kwa watu wote ambao wapo katika hii halmashauri for free maana usafiri wa pikipiki ninao

Kwa kuanzia mmiliki wa bidhaa atanitumia picha halisi ya bidhaa alizonazo kama zilivyo kuepusha mis understanding na wateja then Mimi namwonesha mteja akiridhia kuchukua bidhaa na bei basi Mimi nitachukua pesa kwa mteja then nitakuja kwako kuchukua bidhaa na kumpelekea so tutaenda katika mtindo huo

Ninachohitaji kutoka kwako

1. Uaminifu nikiwa na maana ya kwamba ubora wa bidhaa, mzigo kupatikana kwa wakati, uhalisia wa mzigo na kutoa lisit za bidhaa
2. Punguzo la bei Ili angalau hata mimi niweze kupata hata kiasi chochote kwa Kila bidhaa baada ya kutoa gharama ya mafuta ya pikipiki kutegemea umbali wa mteja alipo

3. Bidhaa nazopendelea uwe nazo ni kama TV, SABWOOFER, n.k

Kwa ufupi Iko hivo

Binafsi nitajitahidi kadri niwezavyo kuhakikisha mteja anapata huduma Bora na kukidhi matamanio ya muuzaji kwa kutafuta wateja wengi niwezavyo

NB: derivery zote nitazifanya kuanzia saa 8 mchana na weekend baada ya muda wa kazi

Ahsante

Mawasiliano: 0746021481 calls/ Whatsapp
 
Safi sana

Pia tafuta tender za serikali au watu binafsi katika halmashauri yako.

Vifaa vya Electronics, mifumo ya IT, security appliances, computers, servers, laptops etc

Ukipata nakupa connection chap
Naomba mawasiliano yako mkuu
 
Una roho nzuri sana kuwapatia vijana wazo la kufanya sasa wewe kaa hapo hapo usubilie msaada wenzako watende....Asante sana
Wazo alilolianza mtu mwingine ngumu sana kuimplement mtu mwingine mkuu hata kama yupo basi hamuwezi kuwa same location
 
mkuu mbona hapa kahama town apa kuna maduka kibao ya electronics si unge bonga nao?

anyway mimi niko hapa nyasubi shule ya rocken hill ngekuwa na hyo mishe tungepiga pamoja sema sipo huko
 
Wazo alilolianza mtu mwingine ngumu sana kuimplement mtu mwingine mkuu hata kama yupo basi hamuwezi kuwa same location
Kasome sababu zilizoifanya ulaya kuanguka kama kiongozi wa biashara duniani....
 
Kwa idea yako wala hukupaswa kuja hapa kutafuta pertiner. Kahama kuna maduka kibao ya electronics. Ilikuwa simple tu. Unamfuata mtu mwenye duka, awe mmoja, wawili au hata mia. Unampa wazo lako na kwa mfanyabiashara kweli hawezi kulikataa.
 
Back
Top Bottom