Nahitaji Scholarship ya kusoma shahada ya sheria (LL.B) nje ya nchi

Nahitaji Scholarship ya kusoma shahada ya sheria (LL.B) nje ya nchi

HOST NOT FOUND

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
1,192
Reaction score
3,486
Habari za wakati huu wapendwa wanajukwaa,

Natumaini wote mko salama.

■Kwa heshima na unyenyekevu, naomba msaada wa ushauri, taarifa au hata fursa yoyote kuhusu scholarships (ufadhili wa masomo) zinazopatikana kwa ajili ya kusomea Shahada ya Sheria (Bachelor of Laws – LL.B) nje ya nchi.

■Nina ndoto ya kusomea sheria katika mazingira ya kimataifa ili niweze kupata maarifa ya kina na ya kisasa, kisha kurejea nyumbani kulitumikia taifa katika sekta ya haki, utawala bora, na maendeleo ya kijamii.

Ningependa kujua:

=>Je, kuna taasisi, mashirika au vyuo vikuu vinavyotoa scholarships za sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika au Tanzania kwa ujumla?

=>Vigezo gani muhimu vinazingatiwa ili kupata ufadhili huo?

=>Je, kuna watu waliowahi kufaulu kupata ufadhili kama huo? Ningefurahi sana kujifunza kupitia uzoefu wao.

=>Ni nchi gani zinazopendekezwa kwa masomo ya sheria na zina fursa nzuri za ufadhili?

=>Na je, ni lini muda sahihi wa kuanza kuomba scholarship hizo?


●Mimi ni kijana mwenye malengo, moyo wa kujifunza, na dhamira ya kufanya kazi kwa bidii. Natamani sana kupata nafasi hii. Wakati wowote kuanzia sasa.

●Nitashukuru kwa msaada wowote, hata kiungo (link), jina la taasisi, au ushauri wa jumla.

Karibuni kwa ushauri, uzoefu, na fursa
 
Sio rahisi kupata mfadhili anayeweza kukufadhili kwenda kusoma nje ya nchi hasa kwa dunia ya leo halafu shahada ya kwanza ya sheria.
 
Acha kujisumbua na nje ya nchi, embu nenda hapo Udsm, ukizingatia kitabu utatoka nondo sana kuliko hata wa nje, tatizo mnadharau vya ndani
 
Back
Top Bottom