Nahitaji ushauri kabla ya kumkabidhi dereva chombo

Nahitaji ushauri kabla ya kumkabidhi dereva chombo

MJ18

Member
Joined
Jul 2, 2018
Posts
53
Reaction score
52
Habarini wanaJF,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu. Nataka kufanya biashara ya bodaboda na kirikuu, sasa nahitaji ushauri wa vtu vya msingi navyopaswa kuvifanya kabla ya kumkabidhi dereva chombo apart from just kuandikishana mkataba.

Sina uzoefu kabisa na hii biashara. Msaada wenu ni wa muhimu sana, natanguliza shukrani.
 
Business Made Easy....

Tafuta watu wanaofanya hiyo biashara kisha wakupe ushauri mkuu. Hapa unaweza kusaidiwa lakini ushauri wa mtu anaeijua na kuifanya hiyo biashara unatofauti sana na ushauri wa mtu wa JF anaejidai kujua kila kitu.

Ni hayo tu.
 
Karibu...kuwa mwelewa tu boss maana hesabu ya bodaboda haiwezi kuwa sawa siku zote...kwenye bodaboda kumbuka kubadilisha oil weekly...mchawi oil tu...lakini kikubwa jitahid kuwa muelewa
 
Elimu kubwa nayoweza kukusaidia wewe mgeni na wenyeji wanaolalamika biashara ina changamoto ni FUNGA GPS KWENYE CHOMBO CHAKO!. Itakusaidia
  1. Kujua dereva ameenda KMs ngapi kwa siku/wiki/mwezi/mwaka wa mkataba wenu.
  2. Matumizi bora ya chombo chako yanazingatiwa (oil, service, spidi, muda wa kazi)
  3. Usalama mara 90% ya chombo chako (tracking system)
  4. Ufanyaji kazi wake (mapato yake) kwa siku/wiki/mwezi/mwaka
Ukiamua kuifanya kiswahili biashara, tegemea matokeo ya kiswahili pia!.
 
unayemkabidhi chombo cha ussfiri amesomea na vyeti anavyo? Hali ya chombo kizima na ratiba ya matengenezo ipoie. Mafundi je wapo?
 
Back
Top Bottom