Nahitaji ushauri kwa mtaji wa 40 milionI

nakupa ushauri huu usipuuze, tafuta chumba kizuri Kinachofaa kutumika kama gym,panga,kisha nunua vifaa vinavyohitajika katika gym.Kuza brand yako na fanya matangazo extensively.Toza kiwango cha bei kinachoendana na uchumi wa wateja wako na hadhi ya gym yako.
Ni ushauri wangu Tu huu!
 
Sababu bado ni mwanafunzi nakushauri usianzishe biashara maana itakusumbua usimamizi.

Kwa experince yangu chukua iyo pesa weka UTT Liquid fund ambayo kwa mwezi una uhakika wa kupata mpaka laki nne kama faida ambayo hujaifanyia kazi na haina risk. Tofauti na biashara ambayo haikupi uhakika asilimia 100 kupata iyo faida unayoihitaji kwa siku, hasa kwa iyo ya gari ambayo ina risk ya kupata ajali au kuharibika muda wowote litakupa stress ushindwe kufocus na shule. Na hayo mahesabu ya faida za Biashara za kwenye makaratasi zisikuchanganye ukahisi unachelewa kuanza au kufanikiwa.

Nimekushauri liquid fund sababu ndio mfuko unaokuruhusu kutoa pesa yako ndani ya siku tatu za kazi kama utaihitaji au utapata wazo bora la Biashara kwa wakati huo. Sikushauri kuweka fixed sababu ya Masharti ya fixed account nyingi zinataka ufix kuanzia miaka mitatu bila kutoa pesa ila faida waweza kutoa.

Biashara inakuhitaji na Inahitaji muda wako kuifatilia na kuipambania, kingine ukipata biashara wekeza angalau robo ya pesa yako maana biashara ina mambo mengi ya kujifunza ukiwa na kiasi kidogo ili kama utafeli usifeli mazima. Lakini pia sio lazima uanze na mtaji kubwa au wote ili uweze kufanikiwa unaweza kuukuza mtaji wako polepole kwa kuanza na kidogo.​

NB: Hakuna mafanikio ya haraka kila kitu kinahitaji utulivu na uvumilivu kukua mpaka kukufanikisha, kingine usimuamini mtu au ndugu akufanyie biashara akuletee faida kipindi wewe umefocus na Chuo, utalia kilio cha mbwa mdomo juu

BEST OF LUCKY
 
Daah nilivyoona tu hizo digits nikacheka😆
 
Daah yaani watu tupo vijijini tunatafuta mitaji ya kupiga pesa watu wanacheza na hizi pesa.

40M ukinipa mimi nakuwa tajiri maisha.

Njoo tufanye dili za korosho huku kusini huu ndio msimu wake aisee,tutaonana ana kwa ana tufanye kazi mguu kwa mguu mpaka mashambani then utanilipa kama mfanyakazi wako
 
Madini njoo hasa dhahabu trust me mwaka mmoja mkubwa mnoo ishu ni mentor mwaminifu ila chonde usichimbishe maduara
 
Wapi huko Uliko rafiki ang,
Na unasemea kwenda kulima shambani hayo Mazao au
kwenda kuya nunua kwa Wakulima shambani na kuuza.??
 

Achana na hiyo biashara ya gari kama huna pesa
Biashara ya magari ni angalau uanze na magari 5
Gari moja huwezi pata faida labda ukomae mwenyewe
Nayo bado ni ngumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…