Nahitaji ushauri wa kisheria

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Nilikuwa na kesi ya ardhi ambapo mtu alivamia eneo langu na kudai ni la kwakwe hivyo kwenye baraza la kata ilimpa ushindi yeye badaye nilikata rufaa mahakama ya wilaya ambapo nilishinda kwa hoja kuwa mimi ndiye mmliki halali wa ardhi husika.

Hata hivyo mshindwa alikusudia kukata rufaa mahakama ya kuu kitengo cha ardhi ingawa kisheria alichelewa kuwasilisha ombi la kukata rufaa ambazo ni siku 90.

Hivyo aliiomba mahakama imruhusu kukata rufaa nje ya muda unaotakiwa kisheria hata hivyo mahakama ilitupilia mbali ombi lake hilo kwa sababu sababu alizozitoa za kukata rufaa nje ya muda hazikuwa na mashiko mbele ya jaji hivyo jaji alistruck out ombi lake.

Tangu rulling itolewe ni miezi zaidi ya mitatu sasa na hakuna dalili ya mshindwa kutaka kukata rufaa zaidi mahakama ya rufaa.

Sasa nimefuatilia drawing order (rulling) ya jaji nimeipata lakini nimejaribu kuuliza makarani wapale mahakamani ili waniambie ni hatua gani napaswa kufuata baada ya kushinda wakaniambia niende kwa wakili wangu atakuwa anajua hatua inayofuata. Hata hivyo nimewasiliana na wakili wangu amenimbia niende kwenye mahakama ya wilaya iliyonipa ushindi nipeleke ile rulling niwaombe watekeleze hukumu ya awali.

Binafsi sijaridhika sana na alichonishauri wakili huyo kwani nilipowasiliana na wengine walinipa ushauri tofauti tofauti hali inayonipelekea kubaki njia panda.

Hivyo nimeamua kulileta hapa jukwaani kwa wataalamu wa sheria ili waweze kunisaidi ni hatua gani napaswa kufuata ili niweze kupata haki yangu.

Pia eneo hilo lilo na mgogoro mshindwa alishawauzia watu na wameshajenga almost lote naomba ushauri wenu hapo.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Mkuu Kurunzi,msikilize na kumheshimu Wakili wako. Kinachofuata hapo ni kutekeleza hukumu. Naamini shauri lenu liliwajumuisha wale wote waliouziwa na kujenga. Kimsingi,kila mwenye maslahi kwenye eneo husika alipaswa kuwemo kwenye shauri.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kurunzi,msikilize na kumheshimu Wakili wako. Kinachofuata hapo ni kutekeleza hukumu. Naamini shauri lenu liliwajumuisha wale wote waliouziwa na kujenga. Kimsingi,kila mwenye maslahi kwenye eneo husika alipaswa kuwemo kwenye shauri.

Shauri hilo hakijumuisha waliouziwa kwani alikuwa anauza wakati shauri lilikuwa linaendelea kesi ilianza tangu mwaka 2006 mpka sept 2014 ikipotolewa hukumu mshaka kuu tingo cha ardhi.
 
Last edited by a moderator:
Shauri hilo hakijumuisha waliouziwa kwani alikuwa anauza wakati shauri lilikuwa linaendelea kesi ilianza tangu mwaka 2006 mpka sept 2014 ikipotolewa hukumu mshaka kuu tingo cha ardhi.

Mkuu Kurunzi,kulifanyika makosa. Mlipaswa kuweka zuio la muda la kutofanyika chochote katika eneo lililokuwa na mgogoro hadi pale ambapo shauri husika lingeisha. Napata kigugumizi kuona utekelezaji dhidi ya wale wasiohusishwa kwenye shauri.

Hatahivyo, waweza kuomba utekelezaji dhidi ya aliyekuwa mhusika.
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru sana mkuu ikiwa nitenda kutekelza hukumu mahakama ya wilaya vipi file lililopo mahakama kuu?

Na kama makosa yalifanyika bila kuwahusisha wadau wengine waluouziwa je hii inaweza ikapelekea waluouziwa kufungua kesi dhidi yaku kupinga utekelezaji wa hukumu hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Natamani kujua ilikuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nilisha kesi nikarudi mahama ya mkoa kukazia hukumu ambapo nilipewa pia Broker ambaye alihakisha anabomoa nyumba zote zilizojegwa hapo.

Haikuwa kazi rahisi maana watu waliandana mpaka kwa mkuu wa wilaya lakini nashukuru mkuu wa wilaya alitaka hukumu ya mahakama ifuate mkondo wake
 
Haukurogwa?
 
Haukurogwa?
Haaaaa inawezekama maana sijui ukilogwa unajisikiaje au inakuwaje...maana si kwa kondoo na kuku zilizochinjiwa pale pa nyoka mkubwa huwa anaonekana pale lakini hayo mambo mimi hayanipi shida kabisa

Nashukuru eneo limeuzwa hela nzuri tu hiyo hela tumemjengea mama nyumba nzuri maisha yanasonga mbele.
 
Hilo ndio la msingi ulilokuwa unahofia, Mtu huwezi kununua ardhi kwa mtu ambaye si mali yake, mwisho wa siku utapata hasara na itabidi urudi kwa yule aliyekuuzia mkapambane.

Ndio maana ni muhimu sana kufanya official search ili uwe salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…