mamsindo
Member
- Jan 8, 2010
- 35
- 28
Wana JF naomba ushauri kuhusu vitenge(african print) kwa wale wenye uzoefu na bidhaa hii.Nina project inayohitaji kutumia vitenge(african print) kwa wingi(kwaajili ya nguo).Tatizo nimejaribu ku-google na nimegundua kuwa kuna aina nyingi za vitenge kutoka sehemu tofauti. Awali nilidhani vitenge vizuri vinatoka Ankara (Ghana) na Congo.Nimeshangaa kuona China nao wanatengeneza vitenge na wao wanaviita "african wax" na wanatumia muundo (pattern) kama wa Ghana!Hii imenifanya nishindwe kujua vitenge vipi ni bora na imenipelekea kuja hapa kupata ushauri kutoka kwenu wana JF.Je, kuna aina zipi za african print(vitenge)? Vitenge bora ni vya kutoka wapi?Je,naweza kuvipataje kwa wingi na kwa bei nzuri na zipi ni njia salama?Natanguliza shukrani kwenu.
Ahsante.
JUU:African print kutoka Ankara(Ghana)
JUU: African print kutoka China
Ahsante.
JUU:African print kutoka Ankara(Ghana)
JUU: African print kutoka China